Wednesday 31 October 2012

STEPS KUSHIRIKIANA NA SERIKALI NA WAKIUKAJI WA....

Maelezo 31/10/2012 
 
KAMPUNI ya usambazaji na utengenezaji filamu nchini Steps Entertainment imeahidi kushirikiana na serikali kupambana na wanaokiuka sheria ya filamu na michezo ya kuigiza ya mwaka 1976. 

Hayo yamesemwa jana na meneja Mkuu wa Steps Entertainment Bw. Jairaj Almoradan jijini Dar es salaam wakati wa mkutano na Sekretatieti ya Bodi ya filamu Tanzania. 

Bw.Almoradan amesema kampuni yake haitapokea kazi za wasanii wasiofuata sheria kwa kutengeneza filamu zilizo kinyume na maadili na zilizo kinyume na sheria. 

Amesema kuwa sheria inawataka kutengeneza filamu zinazofuata maadili na kuwasilisha master kopi kwa ajili ya kuidhinishwa kuingia sokoni. “tutajitahidi kuwaeleza wasanii na tutakuwa wakali kutopokea filamu ambazo tunaona zipo kinyume na maadili na utamaduni wetu.”Amesema Bw. Almoradan. 

Kwa upande wake Katibu Mtendaji wa Bodi ya Ukaguzi wa Filamu Bi. Joyce Fissoo amesema bodi imekuwa ikipata malalamiko kuhusiana na baadhi ya filamu kuwa kinyume na maadili ya Mtanzania. 

“Sisi kama bodi kazi yetu ni kukagua filamu na matangazo yake kama yapo kimaadili na yamefata sheria ikiwa ni pamoja na kuzipa madaraja filamu hizo kabla hazijaenda sokoni.”amesema Bi.Fissoo.

WANANCHI KUTUMA MAONI KUHUSU KATIBA MPYA KWA NJIA YA 'SMS'


Wananchi sasa kutuma maoni kuhusu Katiba Mpya kwa ‘sms’ 

Oktoba 31, 2012 

Na Mwandishi Wetu, DSM

Tume ya Mabadiliko ya Katiba imetangaza namba nne (04) za simu za mkononi ambazo wananchi kwa sasa wanaweza kuzitumia kutuma ujumbe mfupi wa maandishi (‘sms’) kutoa maoni yao kuhusu Katiba Mpya. 

Kwa mujibu wa taarifa ya Tume hiyo kwa vyombo vya habari iliyotolewa leo (Jumatano, Oktoba 31, 2012) namba ambazo wananchi wanaweza kutuma maoni yao kwa njia ya ‘sms’ ni 0715 (Tigo) /0767 (Vodacom) / 0787 (Airtel) / 0774 (Zantel) – 08 15 08. 

“Kwa kuzingatia kuwa Watanzania wengi waliopo mijini na vijijini wanamiliki simu za mkononi, Tume ya Mabadiliko ya Katiba inaamini kuwa njia hii ni fursa nyingine muhimu kwa Watanzania kuweza kuwasilisha maoni yao kwa Tume,”
 imesema sehemu ya taarifa hiyo iliyotolewa na Katibu wa Tume hiyo Bw. Assaa Rashid.

 Ili kutuma maoni, Bw. Assaa amesema, mwananchi anapaswa kufungua ukurasa wa kutuma ujumbe mfupi wa maandishi (sms) katika simu yake na kuandika maoni yake pamoja na jina lake kamili, jinsia, mahali anapoishi, umri, elimu na kazi na kutuma kwenda kwenye namba yoyote kati ya zilizotolewa. 

Kwa mujibu wa Bw. Assaa, baada ya kutumwa, maoni hayo yatakwenda kwa Tume ya Mabadiliko ya Katiba ambapo yatafanyiwa kazi pamoja na maoni yanayokusanywa kwa njia nyingine. 

Uanzishwaji wa njia hii ya ujumbe mfupi wa maandishi unalenga kuwapa fursa nyingine wananchi kutoa maoni yao. Tume ya Mabadiliko ya Katiba pia inapokea maoni ya wananchi kupitia mikutano ya ana kwa ana; barua pepe (maoni@katiba.go.tz); njia za posta (S.L.P. 1681, Dar es Salaam au S.L.P. 2775, Zanzibar); ukurasa wa ‘facebook’ (Tume ya Mabadiliko ya Katiba) na tovuti (http://www.katiba.go.tz/). 

Katika taarifa yake hiyo, Tume imewaomba wananchi kutumia namba hizo kutuma maoni yao binafsi kuhusu Katiba Mpya bila kushawishiwa na watu, makundi, vyama au taasisi yoyote na kufafanua kuwa Tume inatarajia kuanza kupokea maoni ya makundi, vyama na taasisi mara baada ya kumaliza kukusanya maoni binafsi ya wananchi katika awamu ya nne na ya mwisho itakayomalizika mwezi Desemba, 2012.

TANAPA YAHAMISHA, YATEUA WAKURUGENZI WAPYA

Na Seif Mangwangi, Arusha.

SHIRIKA la hifadhi za Taifa nchini (TANAPA) kupitia bodi yake ya   udhamini, imefanya mabadiliko ya nafasi za kazi kwa baadhi ya  watumishi wake kwa kuteua wakurugenzi wapya wawili na kuwahamisha
wengine vituo vya kazi.

Katika taarifa yake kwa waandishi wa habari jana  Afisa uhusiano wa  Tanapa Paschal Shelutete, nafasi zilizofanyiwa mabadiliko ni pamoja na  nafasi mbili za wakurugenzi wa idara na wakuu wanne wa hifadhi za
Taifa.

Wakurugenzi walioteuliwa ni pamoja na  Martine Loibooki ambaye anakuwa  Mkurugenzi  wa Uhifadhi makao makuu ya shirika mjini Arusha,kabla ya hapo alikuwa mkuu wa hifadhi ya Tarangire, Witness Shoo anayekuwa mkurugenzi wa  utumishi na utawala, kabla ya uteuzi huo alikuwa mkurugenzi msaidizi
kwenye mfuko wa millennia (Millenium Challenge Account).

Wakuu wa hifadhi waliohamishwa vituo vya kazi ni pamoja na Steven Qolli anayetoka Ruaha kwenda Tarangire,Wiliam Mwakilema aliyekuwa  hifadhi ya Mikumi anakwenda Serengeti na Noelia Myonga kutoka Gombe  kwenda Kitulo.

Mabadiliko hayo pia yamewagusa baadhi ya watumishi waliokuwa makao  makuu ya shirika ambapo Christopher Timbuka kutoka makao makuu  ameteuliwa kuwa mkuu mpya wa hifadhi ya taifa Ruaha.

Akizungumzia lengo la kufanya mabadiliko hayo Shelutete alisema  ni  zoezi la kawaida ndani ya shirika hilo lengo kuu likiwa ni kuongeza  utoaji wa huduma na ufanisi wa majukumu ya kila siku ya shirika hilo.

“Mabadiliko ni ya kawaida na yamelenga kuongeza ufanisi na kuongeza  ubora wa huduma zetu na si vinginevyo, kwa kuwa hifadhi zetu zote zina   hadhi sawa hakuna ambayo ni muhimu kuzidi nyingine” alisema.

wakati huo huo aliwataka watumishi wa shirika hilo kutangaza utalii wa ndani ili kuvutia watanzania wengi kutembelea hifadhi za Taifa ili kuliongezea shirika mapato yatokanayo na watalii wa ndani.

“Kwa muda mrefu mapato ya shirika yametokana na watalii wanaotoka nje  ya nchi lakini sasa tumewaelekeza watumishi na hasa wakuu wa hifadhi kutangaza utalii wa ndani ili wananchi wapate fursa ya kuzitembelea hifadhi za taifa”

Kuhusu ujangili na uwindaji haramu, Shelutete alisema kuwa shirika hilo limeongeza nguvu kubwa katika doria zake ili kupunguza au kutokomeza kabisa ujangili.

“Tumewaambia wakuu wa hifadhi pamoja na kutangaza utalii wa ndani lakini pia wahakikishe kuwa wanapambana kwa nguvu zote na ujangili na wawindaji haramu”

EXCHANGE RATE JUZI JIJINI ARUSHA






MAGAZETINI LEO JUMATANO 31/10/2012









Tuesday 30 October 2012

MAANDALIZI YA JIJI - JK KUFANYIA UZINDUZI KATIKA MNARA HUU WA AZIMIO LA ARUSHA

Mafundi wakiendelea na ukarabati wa Mnara wa Mwenge ikiwa ni maandalizi ya uzinduzi wa jiji la Arusha mapema Novemba 2, 2012 na Rais Jakaya Kikwete. pembeni ni viongozi wa Wilaya ya Arusha wakijadiliana kuhusu maendeleo ya ukarabati huo.

JK KUZINDUA CHUO KIKUU CHA MANDELA IJUMAA WIKI HII



RAIS  Jakaya  Kikwete  anatarajiwa kuzindua chuo kikuu cha Sayansi na  na teknolojia cha Nelson Mandela jijini Arusha utakaofanyiaka Novemba 2 mwaka huu.

Uzinduzi huo unatokana na kukamilika kwa ukarabati na uboreshaji wa majengo ya chuo umekamilika kwa asilimia 90 na kugharimu kiasi cha shilingi bilioni 90.

Aidha uzinduzi huo utaambatana na harambee ya kuchangia uzinduzi wa mfuko wa  dhamana  wa chuo hicho utakaofanikisha chuo hicho kujiendesha chenyewe na kwamba viongozi mbalimbali waserikali watahudhulia akiwemo makamu wa Rais Dk.Ghalib Bilal.


Akizungumza na waandishi wa habari chuoni hapo, makamu mkuu wa chuo hicho,Profesa Burton Mwamila alisema kuwa taratibu za uzinduzi huo zimekamilika kwa asilimia 100 huku wageni mashuhuri duniani wakitarajiwa kuhudhulia katika sherehe hizo .

Alisema chuo cha Nelson Mandela kilianzishwa na serikali baada ya kuasisiwa na rais mstaafu wa Afriaka kusini,Mzee Nelson Mandela ambaye hataweza kuhudhulia kutokana na matatizo ya kiafya, kwa lengo la kutoa mafunzo na kufanya utafiti katika maeneo mbalimbali ya fani ya sayansi,uhandisi na teknolojia na tayari kimeanza kupokea wanafunzi kutoka ndani na nje ya nchi.

Alisema ukarabati na uboreshaji wa majengo yaliyokuwa yakimilikiwa na CAMATEC  ulianza Agosti  10 mwaka 2010 na ilipofika oktoba 2011 chuo hicho kilidahili kundi la kwanza la wanafunzi wapatao 83,kati yao 30 wakichukua masomo ya uzanivu na 53 ya uzamili.

Aidha aliongeza kuwa chuo hicho kwa sasa kina jumla ya wanafunzi 217 na kwamba katika mwaka huu wa masomo ,chuo kimedahili wanafunzi 135 wa kundi la pili ,huku kati yao 46 wakichukua masomo ya uzanivu na 89 wakichukua masomo ya uzamili.

Akizungumzia hali ya ubora wa elimu unaotolewa katika chuo hicho alisema kuwa chuo kinawataalamu mbalimbali kutoka vyuo mbalimbali hapa duniani na kwamba kimekuwa kikishirikiana kwa ukaribu na vyuo mbalimbali vilivyoko katika nchi 10 duniani.

‘’tumeanzisha ushirikiano wa kitaaluma na vyuo vikuu mbalimbali hapa duniani, ambapo kwa kuanzia tunashirikiana na nchi za Marekani ,Uingereza,Sweden,Itary ,Urusi ,Korea Kusini,India,Ubeligiji na Swazland’’alisema Prof Mwamilwa.

Alisema makubaliano na vyuo hivyo ni kushirikiana katika kufundisha ambapo walimu waliopo kwenye vyuo hivyo wakuwa wakija kufundisha huku pia walimu waliopo chuoni hapo wakipata fursa ya kujifunza katika vyuo hivyo na kwamba walimu ambao hawatafika watakuwa wakiitoa elimu kwa njia ya mtandao.

Alisisitiza kuwa kwa sasa chuo hicho kina jumla ya maprofesa 16 wenye upeo mkubwa wa kufundisha masomo mbalimbali kutoka nchi mbalimbali ikiwemo Rwanda na Burundi ambao wameajiriwa kwa ajili ya kufundisha na kutoa elimu iliyobora inayokubalika kimataifa.

Aidha alisisitiza kuwa uzinduzi huo utatanguliwa na maonyesho mbalimbali ya elimu, burudani kutoka vikundi mbalimbali vya wasanii ,uwekaji wa jiwe la msingi utakaofanywa na Rais Kikwete,pamoja na kutembelea majengo ya chuo.

Mwisho.

MATAYARISHO YA ARUSHA KUWA JIJI- BARABARA ZAENDELEA KUMALIZIWA



BARABARA MBALIMBALI ZA KATIKATI YA MJI WA ARUSHA ZIKIENDELEA KUKAMILISHWA. IJUMAA WIKI HII RAIS KIKWETE ATAZINDUA RASMI MJI WA ARUSHA KUWA JIJI

USAFIRI WA TRENI DSM JANA

Jana baadhi ya wakazi wa jiji la Dar-es-Salaam wameanza rasmi matumizi ya usarifi wa kutumia treni. Una maoni yeyote juu ya usafiri wa treni jijini?

WANAFUNZI KWENYE MDAHALO


Baadhi ya wanafunzi wa shule ya msingi Bassotu Wilaya ya Hanang’ Mkoani Manyara wakiwa kwenye mdahalo wa mabadiliko ya tabia nchi na namna ya kupunguza athari zake ulioendeshwa na Mtandao wa Asasi za kijamii mkoani Manyara (MACSNET) kwa udhamini wa The Foundation For Civil Society

MAGAZETINI LEO JUMANNE 30/10/2012
















Sunday 28 October 2012

CHADEMA MOTO ARUSHA, YAIGARAGAZA CCM MAENEO MENGINE

Umati wa wafuasi wa Chadema wakisikiliza viongozi mbalimbali siku ya mwisho ya ufungaji wa kampeni katika kata ya daraja mbili. katika uchaguzi huo uliomalizika jana, diwani wa Chadema aliibuka mshindi kwa kura nyingi.
Na mwandishi wetu

CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kimeendelea kuonyesha imani yake kubwa kwa watanzania baada ya jana mgombea wake kuibuka mshindi katika kata ya Daraja mbili.

uchaguzi huo wa Daraja mbili ulikuwa unarudiwa baada ya diwani wake wa awali kwa tiketi ya (CCM) Bashir Msangi kufariki dunia ghafla mapema mwaka huu.

Matokeo katika Kata hiyo ya Daraja Mbili, yalionyesha CHADEMA ineweza kujikusanyia kura 2192 dhidi ya 1315 za mgombea wa chama tawala.

Hata hivyo uchaguzi huo ambao ulifanyika kwenye kata 29 katika halmashauri mbalimbali nchini, umemalizika huku vurugu kubwa zikitawala na kusababisha wafuasi wa vyama hivyo kuumizana.

Hadi sasa matokeo ya kata 14 yanaonyesha kuwa CCM ilikuwa imefanikiwa kurejesha kata zake saba, huku CHADEMA ikinyakua kata sita, ambapo mbili zilikuwa za kwao na nne imewanyang’anya CCM na CUF ikiwa na kata moja.


matokeo ya udiwani katika baadhi ya kata yalikuwa yakiendelea kutolewa huku CHADEMA ikiendelea kuikaba CCM kwa kuzitwaa baadhi ya zilizokuwa kata zake.

CHADEMA wameweza kuzirejesha kata zao mbili za Nangerea jimboni Rombo, ambapo mgombea wao Frank Sarakana alijizolea kura 2370 dhidi ya 1134 za Dysmas Silayo wa CCM pamoja na ile ya Mtibwa, mkoani Morogoro.


Wilayani Sikonge katika kata ya Ipole, CCM walipoteza kata hiyo kwa CHADEMA iliyopata kura 577 dhidi ya 372 za washindani wao, na vilevile kuitwaa kata nyingine ya Lengali wilayani Ludewa iliyokuwa ya CCM.


CHADEMA pia ilikuwa ikiongoza katika kata ya Mpwapwa, mkoani Dodoma, hadi tunakwenda mitamboni usiku.


Nayo CCM ilifurukuta kwa kuzirejesha kata zake za Msalato ya mkoani Dodoma, Bang’ata ya Arumeru Magharibi kwa kuwa 1177 dhidi ya 881 za CHADEMA, Mletele ya Songea CCM ilishinda kwa kura 950 na CHADEMA ilipata 295.


Pia CCM iliweza kutetea kata zake za Mwawaza mjini Shinyanga, Lwenzela mkoani Geita, Bungala wialayni Kahama na Bagamoyo mkoani Pwani kwa kuibwaga CHADEMA wakati Chama cha Wananchi (CUF) kilishinda kata ya Newala.

JK AWASILI SAME



Kina Mama waliovaa mavazi ya CCM wakiimba nyimbo mbalimbali kutumbuiza mara baada ya Rais Jakaya Kikwete kutua katika uwanja wa KIA, Mkoa Kilimanjaro, Rais anafanya ziara ya kikazi ya siku nne mkoani Kilimanjaro na jana alianzia ziara yake wilayani Same.

Viongozi mbalimbali wa Mkoa wa Kilimanjaro wakisubiri kumpokea Rais Jakaya Kikwete katika uwanja wa ndege wa KIA jana.