Thursday 27 December 2012

Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa halmashauri ya Singida alumbana na diwani wa viti maalum (CCM) kuhusiana na ripoti ya Sikika.





Dk.Henry Mmbando,wa ofisi ya mganga mkuu wa halmashauri ya wilaya ya Singida akitoa ufafanuzi juu ya tuhuma zilizotolewa na shirika la Sikika juu ya uwajibikaji katika kutoa huduma katika halmashauri hiyo.(Picha na Nathaniel Limu).

 Mwanakamati wa shirika lisilo la kiserikali la Sikika, diwani (CCM) Salima Kundya akimtuhumu diwani wa mkutano huo diwani Elia Digha (hayupo pichani) kwa kauli yake kuwa kamati ya Sikika haijui kitu chochote kuhusu na utoaji wa huduma ya afya katika halmashauri ya wilaya ya Singida. Salima alikuwa akitoa tuhuma hizo mbele ya mkutano wa mrejesho wa taarifa ya uwajibikaji katika utoaji wa huduma za afya iliyokuwa ikitolewa na shirika la Sikika
Na Nathaniel Limu.
Halmashauri ya wilaya ya Singida imesema haitakubali kuchonganishwa na wananchi wake na vyombo au taasisi yakiwemo mashirika yasiyo ya kiserikali (NGOs), kwa kutoa taarifa zisizofanyiwa utafiti wa kina.
Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa halmashauri hiyo Alli Juma, amesema hayo muda mfupi kabla ya mkutano wa mrejesho wa ripoti/taarifa ya shirika lisilo la kiserikali la Sikika lenye makazi yake jijini Dar-es-salaam, iliyohusu ufuatiliaji wa uwajibikaji katika utoaji wa huduma za afya, haujafungwa rasmi.
Amesema taarifa iliyotolewa na shirika la Sikika, kwa kiasi kikubwa haikufanyiwa utafiti wa kina, kitendo ambacho kinaweza kusababisha halmashauri kutokuelewana vizuri na wananchi wake.
Alli ambaye ni Afisa Utumishi amesema Sikika hawakuwa na mawasiliano wala ushirikiano mzuri na wakuu wa idara katika kupata ukweli wa taarifa mbalimbali walizokuwa wanazikusanya.
“Mimi niwaombeni tu ndugu zangu wa Sikika, fanyeni kazi kwa kufuata sheria, kanuni na taratibu, halafu mkiandika mabaya, upande wa pili andikeni pia mazuri hata kama yapo machahe”,alisema Alli.
Mkutano huo uliokuwa chini ya uenyekiti wa diwani (CCM) Elia Digha, Mwenyekiti huyo alitoa shutuma nzito kwamba wafanyakazi wa Sikika na kamati nzima iliyofuatilia uwajibikaji wa huduma za afya, haijui lolote.
“Mimi nasema timu yote iliyoleta taarifa hii, haijui lolote, naomba siku za usoni tushirikiane vizuri katika kufuatilia uwajibikaji katika sekta zote, kutoa taarifa za jumla jumla kama hii, mtaacha watu waichukie bure serikali”, alisema Digha ambaye ni diwani wa kata ya Msange jimbo la Singida Kaskazini.
Baada ya maneno hayo mazito, diwani wa viti maalum (CCM) Salima Kundya, aliyeshiriki na Sikika kufuatilia uwajibikaji katika sekta ya afya, alimtolea uvivu Mwenyekiti Digha, kuwa lengo lake ni kutaka kuficha ukweli uliopo kwenye taarifa hiyo.
“Kama sisi madiwani wawili wa CCM mliotuchagua tukashirikiane na Sikika na tukabaini yote yaliyopo kwenye taarifa ya Sikika kuwa ni ya ukweli mtupu, halafu wewe unasema hatujui lo lote, basi wewe mwenyekiti Digha na madiwani wote wa CCM walioshiriki kutachagua na ninyi wote hamjui kitu au cho chote kinachofanyika ndani ya halmashauri hii”, alisema Salima huku uso wake ukionyesha kujawa na hasira.
Baada ya maneno hayo ya diwani Salima, bila kulazimishwa, Digha ambaye pia ni msaidizi wa mbunge wa jimbo la Singida kaskazini Lazaro Nyalandu, alisimama na kuomba radhi kwa matamshi yake ambayo yalilenga kuidhalilisha kamati iliyoambatana na Sikika.
Katika mengi yaliyomo kwenye taarifa ya Sikika, kuna hoja iliyotolewa na mkaguzi mkuu wa hesabu za serikali, inaonyesha kuwa halmashauri hiyo ilikuwa na shilingi bilioni 1,686,561,960 za miradi mbalimbali ya maendeleo.
Lakini taarifa hiyo, ilionyesha kiasi cha shilingi bilioni 1.6 sawa na aslimia 61.4,hazikutumika kwa wakati, kitendo hicho kinamaanisha kuwa baadhi ya miradi ya maendeleo, ilikamilika nusu ama haijakamilika kabisa.

Makamu wa Rais Dkt. Bilal afungua rasmi kituo cha Polisi cha Kiboje Zanzibar.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akimkabidhi Cheti, Saleh Ahmed Said, kutoka Migoz Supermarket, ambaye ni mmoja kati ya watu waliochangia ujenzi  wa Kituo hicho cha Polisi cha Kiboje, wakati wa hafla za ufunguzi wa kituo hicho zilizofanyika leo Desemba 26, 2012 Wilaya Kati Mkoa wa Kusini Unguja.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisaliminana na maofisa wa Usalama wa Wilaya ya Kati, wakati alipowasili eneo hilo kwa ajili ya kufungua rasmi Kituo cha Polisi cha Kiboje, kilichpo Mkoa wa Kusini Unguja.

 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilala na Kamishina wa Polisi wa Zanzibar, Mussa Ali Mussa, wakifunua kwa pamoja kitambaa kuashiria ufunguzi rasmi wa Kituo cha Polisi cha Kiboje, baada ya kukamilika kwa ujenzi wa kituo hicho ulioanza Februari 14, 2012 na kuzinduliwa Desemba 26, wakati wa hafla ya uzinduzi huo iliyofanyika Kiboje Wilaya ya Kati Mkoa wa Kusini Unguja

 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akikata utepe  kuashiria ufunguzi rasmi wa Kituo cha Polisi cha Kiboje, baada ya kukamilika kwa ujenzi wa kituo hicho ulioanza Februari 14, 2012 na kuzinduliwa leo Desemba 26, 2012, wakati wa hafla ya uzinduzi huo iliyofanyika Kiboje Wilaya ya Kati Mkoa wa Kusini Unguja.

 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisikiliza maelezo kutoka kwa Kamishina wa Polisi Zanzibar, Mussa Ali Mussa, wakati akitembelea kukagua jengo la Kituo cha Polisi cha Kiboje, baada ya kufungua rasmi jengo hilo lililoanza kujengwa Februari 14, 2012 na kuzinduliwa Desemba 26, 2012, wakati wa hafla ya ufunguzi huo iliyofanyika Wilaya ya Kati, Mkoa wa Kusini Unguja.

 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilala, akisikiliza maelezo kutoka kwa Kamishina wa Polisi Zanzibar, Mussa Ali Mussa, wakati akitembelea kukagua jengo la Kituo cha Polisi cha Kiboje, katika Chumba cha Mawasiliano baada ya kufungua rasmi jengo hilo lililoanza kujengwa Februari 14, 2012 na kuzinduliwa leo Desemba 26, 2012, wakati wa hafla ya ufunguzi huo iliyofanyika Wilaya ya Kati, Mkoa wa Kusini Unguja.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilala, akisikiliza maelezo kutoka kwa Kamishina wa Polisi Zanzibar, Mussa Ali Mussa (kulia) wakati akitembelea kukagua jengo la Kituo cha Polisi cha Kiboje katika Chumba cha Ofisi ya Polisi Jamii, baada ya kufungua rasmi jengo hilo lililoanza kujengwa Februari 14, 2012 na kuzinduliwa Desemba 26, 2012, wakati wa hafla ya ufunguzi huo iliyofanyika Wilaya ya Kati, Mkoa wa Kusini Unguja.

Kikundi cha Sanaa cha Polisi kikitoa burudani ya maigizo.

Kikundi cha ngoma cha Tukulanga kikitoa burudani wakati wa hafla hiyo.
PICHA ZOTE KWA HISANI YA OFISI YA MAKAMU WA RAIS

vichwa vya habari magazetini leo ALHAMISI 27/12/012











Wednesday 26 December 2012

WAZIRI MKUU MSTAAFU EDWARD LOWASA ASHEREHEKEA X-MASS ZANZIBAR

Waziri Mkuu Mstaafu na Mbunge wa Monduli,Mh. Edward  Lowassa na mkewe Mama Regina Lowassa wakiungana na Wakristo wengine  kwenye ibada ya Sikukuu ya Krismas iliyofanyika leo kwenye Kanisa la  Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT),Mwanakwerekwe  Zanziba

Waziri Mkuu Mstaafu na Mbunge wa Monduli,Mh. Edward  Lowassa akitoa salaam za Xmas kwenye Kanisa la Kiinjili la  Kilutheri Tanzania (KKKT),Mwanakwerekwe Zanzibar mara baada ya ibada ya  Sikukuu hiyo leo.Mh. Lowassa;yuko visiwani humo kwa mapumziko  ya sikukuu hiyo,ambapo amewataka watanzania kusherehekea sikukuu hizi za  krismas na mwaka mpya kwa amani na upendo huku tukilinda umoja na  mshikamano uliojengwa na waasisi wetu Mwalimu Julius Nyerere na Sheikh  Abeid Karume.

BREAKING NEWS- PADRI APIGWA RISASI HUKO ZANZIBAR

Kwa mujibu wa Breaking News  toka Radio One, Padre  anayejulikana kwa jina la Ambrose Mkenda amepigwa Risasi na Watu  wasiofahamika kwenye gate la nyumbani kwake wakati akifunguliwa gate  aingie nyumbani kwake maeneo Kitomondo Mjini Zanzibar, ambako ndiko  makazi yake yalipo akiwa ndani ya gari aliyokuwa akiendesha pekee yake.

Hali yake sio nzuri kwani Risasi aliyopigwa imemdhuru maeneo ya mdomoni.

Waliompiga Risasi Padre huyo inasemekana ni watu waliokuwa kwenye  pikipiki, ambao walimvamia akisubilia afunguliwe gate kuingia nyumbani  kwake.

Kutoka Jamiiforums

HAPPY HOLIDAYS



RAIS JK ASHEREHEKEA X-MASS SERENGETI KWA KUWA MGENI RASMI MECHI ZA UJIRANI MWEMA

Mabingwa  wa Kombe la Ujirani Timu ya hoteli ya Seronera wakifurahia ushindi  baada ya kuilaza kwa mabao 5-4 hoteli ya Four Seasons Safari Lodge   katika Uwanja wa Kifaru katika Hifadhi ya Serengeti mkoani Mara .  Hadi mechi inaisha timu hizo zilitoka sare ya 1-1 kabla kupigwa mikwaju  ya penati ambapo Serena walifunga mabao 4 na dhidi ya 3 ya wapinzani  wao.

Nahodha  wa hoteli ya Seronera Jamali Kitongo akifurahia baada ya kukabidhiwa  kombe la Ujirani mwema na Rais Jakaya Kikwetebaada ya timu yake kuilaza  kwa mabao 5-4 hoteli ya Four Seasons Safari Lodge katika Uwanja wa  Kifaru katika Hifadhi ya Serengeti mkoani Mara Hadi mechi inaisha  timu hizo zilitoka sare ya 1-1 kabla kupigwa mikwaju ya penati ambapo  Serena walifunga mabao 4 na dhidi ya 3 ya wapinzani wao.

Rais  Jakaya Mrisho Kikwete akimkabidhi nahodha wa timu ya hoteli ya Seronera  Jamali Kitongo kombe la Ujirani mwema baada ya timu hiyo  kuilaza kwa  mabao 5-4 hoteli ya Four Seasons katika Uwanja wa Kifaru katika Hifadhi  ya Serengeti mkoani Mara  Hasdi mechi inaisha timu hizo zilitoka sare  ya 1-1 kabla kupigwa mikwaju ya penati ambapo Serena walifunga mabao 4  na dhidi ya 3 ya wapinzani wao.

Rais  Jakaya Mrisho Kikwete katika picha ya pamoja na timu ya hoteli ya  Four  Seasons Safari Lodge kabla ya kucheza na hoteli ya Serena katika Uwanja  wa Kifaru katika Hifadhi ya Serengeti mkoani Mara. hadi mechi  inaisha timu hizo zilitoka sare ya 1-1 kabla kupigwa mikwaju ya penati  ambapo Serena walifunga mabao 4 na dhidi ya 3 ya wapinzani wao.

Rais  Jakaya Mrisho Kikwete akikagua  timu ya hoteli ya  Serena  kabla ya  kucheza na hoteli ya Four Seasons Safari Lodge katika Uwanja wa Kifaru  katika Hifadhi ya Serengeti mkoani Mara.  hadi mechi inaisha timu  hizo zilitoka sare ya 1-1 kabla kupigwa mikwaju ya penati ambapo Serena  walifunga mabao 4 na dhidi ya 3 ya wapinzani wao.              Picha na IKULU

vichwa vya habari magazetini leo jumatano 26/12/012










kwa msaada wa mjengwa.blogspot.com