Monday 20 June 2016

'MASTER PLAN' YA JIJI LA ARUSHA KUKAMILIKA AGOSTI MWAKA HUU

Arusha 
ZIARA ya Rais Msataafu Jakaya Kikwete aliyoifanya nchini Singapole wakati wa utawala wake imeanza kuzaa matunda katika Jiji la Arusha baada ya Mpango kabambe (Master Plan) ya Jiji la Arusha kukamilika.

Mmoja wa washiriki wa mkutano wa kujadili rasimu ya tano na sita ya mpango kabambe wa jiji la Arusha (Master Plan), Godwin Abeid akisikiliza mada kwa makini
Hayo yalielezwa jijini hapa jana kwenye mkutano wa mwisho wa uwasilishaji rasimu ya utekelezaji wa mpango kabambe kwa wadau wa maendeleo wa Halmashauri ya jiji la Arusha na viunga vyake.


Akizungumza mjini hapa Mkurugenzi Msaidizi Mpango Kabambe kutoka Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Mkazi Amulike Mahenge alisema, mpango huo umelenga katika kuboresha majiji mawili ambayo ni Mwanza kwa eneo la Nyamagana na Jiji la Arusha.
Washiriki wa Mkutano wa kujadili rasimu ya mpango kabambe wa Jiji la Arusha wakimsikiliza mtoa mada (hayupo pichani), katika ukumbi wa mikutano hoteli ya Lush Garden jijini Arusha

Wednesday 15 June 2016

TMF YAWATAKA WAANDISHI WA HABARI NCHINI KUKIMBIZANA NA TEKNOLOJIA.

MOROGORO
Waandishi wa habari nchini wametakiwa kuendelea kujifunza uandishi wa kisasa unaotumia kasi ya Teknolojia na kuacha kuandika kwa mazoea kwa kutumia mbinu za kizamani.

Wito huo umetolewa leo mjini Morogoro na mkurugenzi wa mfuko wa kusaidia vyombo vya habari nchini Ernest Sungura wakati wa ufunguzi wa mafunzo ya awali kwa waandishi wa habari waliofanikiwa kupata ruzuku ya kuandika habari za vijijini.

Sungura amesema kuwa taaluma ya uandishi wa habari kwa sasa inahitaji waandishi wanaopenda kujifunza mara kwa mara kwani maendeleo ya matumizi ya teknolojia kila siku yanabadirika.

Sambamba na hayo Sungura ameongeza kuwa mwandishi ambaye hapendi kujifunza na akaendelea na uandishi wa habari wa kizamani atakosa soko la ajira katika ulimwengu wa sasa unaokimbizana na teknolojia ya mitandao.

Katika hatua nyingine amewataka waandishi wa habari waliopata ruzuku ya kuandika habari za vijijini kuzitumia pesa hizo za ruzuku katika malengo yaliyokusudiwa ili kufanikisha kufikia malengo ya kusaidia jamii hususan za vijijini.

Kwa upande wake Afisa miradi wa mfuko wa kusaidia vyombo vya habari nchini  Dastani Kamanzi amewataka waandishi wa habari kuandika habari zenye ukweli pasipo kupendelea upande wowote.

Mafunzo ya awali ya siku tatu yanayofanyika katika ukumbi wa Hotel ya Flomi mjini Morogoro yameshirikisha waandishi wa habari thelathini waliofanikiwa kupata ruzuku ya kuandika habari za vijijini kati ya waandishi miamoja arobaini na sita waliomba nchi nzima. 
MKUREGENZI WA MFUKO WA KUSAIDIA VYOMBO VYA HABARI NCHINI (TMF) ERNEST SUNGURA ALIYESIMAMA AKIONGEA NA WAANDISHI WA HABARI KATIKA UKUMBI WA FLOMI MJINI MOROGORO.

Babake Reeva amtaka Pistorius kulipia alichotenda

Baba wa mwanamitindo wa Afrika Kusini ambaye aliuawa Reeva Steenkamp, amezungumza mahakamani kwa mara ya kwanza akisema kuwa muuaji wa Reva, Oscar Pistorius lazima alipie yale aliyoyatenda.
Akizungumza mahakamani huku amejawa na majonzi, bwana Steenkamp alisema kuwa familia yake imetaabika kutokana na kuuawa kwa Reeva.
Alisema anaamini kuwa bintiye alikuwa amegombana na Oscar Pistorius usiku ambao aliuawa miaka mitatu iliyopita.

Jarida maalum la Taasisi ya Wanyamapori Pasiansi lazinduliwa Jijini Mwanza

Serikali imeahidi kuendelea kuijengea uwezo Taasisi ya Taaluma za Wanyamapori iliyopo Pasiansi jijini Mwanza, ili kukabiliana na matukio ya ujangili ambayo yametikisa nchi miaka ya karibuni.
Akizungumza na wanahabari katika uzinduzi wa Makala Maalumu ya Maadhimisho ya miaka 50 na Jarida Maalum la taasisi hiyo, Katibu Mkuu Wizara ya Maliasili na Utalii, Meja Jenerali Gaudence Milanzi, amesema taasisi hiyo imetoa mchango mkubwa katika kufundisha askari wanyamapori ambao wamesaidia kwenye vita dhidi ya ujangili na kupunguza matukio ya ujangili nchini.
Meja Jenerali Milanzi amesema katika miaka ya karibuni Tanzania imetikiswa na matukio ya ujangili ambayo yamesababisha kuuawa kwa wanyamapori wakiwemo tembo na kuhatarisha uwepo wa wanyama hao ambao ni kivutio kikubwa cha watalii.