Monday, 20 June 2016

'MASTER PLAN' YA JIJI LA ARUSHA KUKAMILIKA AGOSTI MWAKA HUU

Arusha 
ZIARA ya Rais Msataafu Jakaya Kikwete aliyoifanya nchini Singapole wakati wa utawala wake imeanza kuzaa matunda katika Jiji la Arusha baada ya Mpango kabambe (Master Plan) ya Jiji la Arusha kukamilika.

Mmoja wa washiriki wa mkutano wa kujadili rasimu ya tano na sita ya mpango kabambe wa jiji la Arusha (Master Plan), Godwin Abeid akisikiliza mada kwa makini
Hayo yalielezwa jijini hapa jana kwenye mkutano wa mwisho wa uwasilishaji rasimu ya utekelezaji wa mpango kabambe kwa wadau wa maendeleo wa Halmashauri ya jiji la Arusha na viunga vyake.


Akizungumza mjini hapa Mkurugenzi Msaidizi Mpango Kabambe kutoka Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Mkazi Amulike Mahenge alisema, mpango huo umelenga katika kuboresha majiji mawili ambayo ni Mwanza kwa eneo la Nyamagana na Jiji la Arusha.
Washiriki wa Mkutano wa kujadili rasimu ya mpango kabambe wa Jiji la Arusha wakimsikiliza mtoa mada (hayupo pichani), katika ukumbi wa mikutano hoteli ya Lush Garden jijini Arusha

Wednesday, 15 June 2016

TMF YAWATAKA WAANDISHI WA HABARI NCHINI KUKIMBIZANA NA TEKNOLOJIA.

MOROGORO
Waandishi wa habari nchini wametakiwa kuendelea kujifunza uandishi wa kisasa unaotumia kasi ya Teknolojia na kuacha kuandika kwa mazoea kwa kutumia mbinu za kizamani.

Wito huo umetolewa leo mjini Morogoro na mkurugenzi wa mfuko wa kusaidia vyombo vya habari nchini Ernest Sungura wakati wa ufunguzi wa mafunzo ya awali kwa waandishi wa habari waliofanikiwa kupata ruzuku ya kuandika habari za vijijini.

Sungura amesema kuwa taaluma ya uandishi wa habari kwa sasa inahitaji waandishi wanaopenda kujifunza mara kwa mara kwani maendeleo ya matumizi ya teknolojia kila siku yanabadirika.

Sambamba na hayo Sungura ameongeza kuwa mwandishi ambaye hapendi kujifunza na akaendelea na uandishi wa habari wa kizamani atakosa soko la ajira katika ulimwengu wa sasa unaokimbizana na teknolojia ya mitandao.

Katika hatua nyingine amewataka waandishi wa habari waliopata ruzuku ya kuandika habari za vijijini kuzitumia pesa hizo za ruzuku katika malengo yaliyokusudiwa ili kufanikisha kufikia malengo ya kusaidia jamii hususan za vijijini.

Kwa upande wake Afisa miradi wa mfuko wa kusaidia vyombo vya habari nchini  Dastani Kamanzi amewataka waandishi wa habari kuandika habari zenye ukweli pasipo kupendelea upande wowote.

Mafunzo ya awali ya siku tatu yanayofanyika katika ukumbi wa Hotel ya Flomi mjini Morogoro yameshirikisha waandishi wa habari thelathini waliofanikiwa kupata ruzuku ya kuandika habari za vijijini kati ya waandishi miamoja arobaini na sita waliomba nchi nzima. 
MKUREGENZI WA MFUKO WA KUSAIDIA VYOMBO VYA HABARI NCHINI (TMF) ERNEST SUNGURA ALIYESIMAMA AKIONGEA NA WAANDISHI WA HABARI KATIKA UKUMBI WA FLOMI MJINI MOROGORO.

Babake Reeva amtaka Pistorius kulipia alichotenda

Baba wa mwanamitindo wa Afrika Kusini ambaye aliuawa Reeva Steenkamp, amezungumza mahakamani kwa mara ya kwanza akisema kuwa muuaji wa Reva, Oscar Pistorius lazima alipie yale aliyoyatenda.
Akizungumza mahakamani huku amejawa na majonzi, bwana Steenkamp alisema kuwa familia yake imetaabika kutokana na kuuawa kwa Reeva.
Alisema anaamini kuwa bintiye alikuwa amegombana na Oscar Pistorius usiku ambao aliuawa miaka mitatu iliyopita.

Jarida maalum la Taasisi ya Wanyamapori Pasiansi lazinduliwa Jijini Mwanza

Serikali imeahidi kuendelea kuijengea uwezo Taasisi ya Taaluma za Wanyamapori iliyopo Pasiansi jijini Mwanza, ili kukabiliana na matukio ya ujangili ambayo yametikisa nchi miaka ya karibuni.
Akizungumza na wanahabari katika uzinduzi wa Makala Maalumu ya Maadhimisho ya miaka 50 na Jarida Maalum la taasisi hiyo, Katibu Mkuu Wizara ya Maliasili na Utalii, Meja Jenerali Gaudence Milanzi, amesema taasisi hiyo imetoa mchango mkubwa katika kufundisha askari wanyamapori ambao wamesaidia kwenye vita dhidi ya ujangili na kupunguza matukio ya ujangili nchini.
Meja Jenerali Milanzi amesema katika miaka ya karibuni Tanzania imetikiswa na matukio ya ujangili ambayo yamesababisha kuuawa kwa wanyamapori wakiwemo tembo na kuhatarisha uwepo wa wanyama hao ambao ni kivutio kikubwa cha watalii. 

Sunday, 29 March 2015

WAZIRI MEMBE ATEMBELEA SEKONDARI TUSIIME LEO

WAZIRI wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernard Membe,
Akisikiliza maelezo kutoka kwa mwanafunzi wa kidato cha pili sekondari ya Tusiime, Khadija Suleiman kuhusu namna ya kuchuja maji wakati Waziri alipofungua rasmi maabara ya kisasa ya sayansi na maktaba na mahafali ya tano ya kidato cha sita ya shule hiyo.

WAZIRI wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernard Membe, akipata maelezo kutoka kwa Angela Shanira wa kitado cha tano sekondari ya Tusiime Tabata kuhusu masuala mbalimbali ya kisayansi kwenye maabara ya shule hiyo wakati Waziri alipofungua rasmi maabara ya kisasa ya sayansi na maktaba na mahafali ya tano ya kidato cha sita ya shule hiyo



Na Mwandishi Wetu

WAZIRI wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernard Membe, amesema serikali inaangalia iwezekano wa kuzipa ruzuku shule binafsi ili ziweze kujiendesha vizuri huku akizimwagia sifa shule za Tusiime kwa kuendelea kufanya vizuri kwa kutoa elimu bora na katika viwango vinavyokubalika kitaifa na kimataifa.
Alitoa pongezi hizo leo alipozindua jengo la maabara za sayansi na maktaba ya shule hizo na mahafali ya tano ya kidato cha sita ambapo Membe alikuwa mgeni rasmi.
Alisema serikali imegundua umuhimu huo wa kuzipa ruzuku na imeanza kuliangalia upya suala hilo kwani litasaidia shule binafsi kupunguza ada hivyo watanzania wengi kupata fursa ya kupata elimu kwasababu gharama zinapopanda wazazi wamekuwa wakiumia.
 Alisema nguvu ya uchumi wa gesi inaonyesha kuwa Tanzania itakuwa na uwezo wa kifedha wa kutoa ruzuku kwa shule binafsi kama ilivyo kwa baadhi ya nchi duniani ambapo shule hizo hupewa ruzuku ya hadi asilimia 40.

Vile vile, Waziri Membe alisema sifa za shule hiyo ndizo zimemvutia kwenda kujionea mwenyewe mambo mazuri ambayo amemekuwa akiyasikia huko nje kwa muda mrefu.
 Alisema kwa maendeleo ya wanafunzi kitaaluma shuleni hapo ni ushahidi tosha wa dhamira ya dhati waliyonayo Tusiime kama taasisi ya kutoa elimu bora kwa vijana wa kitanzania kwani wamekuwa wakifanya vyema katika mitihani mbalimbali ya kimkoa, kikanda na kitaifa.

“Kweli nimejionea mwenyewe kwa macho yangu na nimeridhika kwamba sifa nzuri nazozisikia huko  ni ukweli mtupu na mnastahili,” alisema Membe na kuongeza.
“Kwangu kama kiongozi mwandamizi wa serikali ya awamu ya nne, inanipa faraja kuona malengo na maazimio ya serikali ya kuhakikisha watoto wetu wanapata elimu na kujengewa maarifa na ujuzi vinatekelezwa kwa vitendo. Kwa namna ya pekee nawapongeza sana walimu kwa kufanya kazi kwa bidii na weledi mkubwa katika kufundisha na kuwalea watoto hawa,” alisema Membe ambaye ni mwanadiplomasia aliyebobea na Mjumbe wa Kamati Kuu CCM.
Alisema kwa kutambua umuhimu wa elimu kwa maendeleo ya jamii, serikali itaendelea kuwekeza zaidi katika sekta ya elimu na itaendelea kushirikiana na watanzania ambao wanatumia sehemu ya mali walizojaliwa na Mungu kuandaa mazingira ya kuwaelimisha wenzao.
  
Naye Mkuu wa shule ya sekondari Tusiime, Emil Rugambwa, alisema shule hiyo kama kawaida yake ni moja kati ya shule chache za binafsi zinazofanya vizuri zikiwa na idadi kubwa ya watahiniwa kulinganisha na shule zingine zinazofanya vizuri zikiwa na idadi ndogo ya Watahiniwa.  
Alisema katika kuhakikisha Tusiime inatoa elimu bora na kukuza kiwango cha ufaulu, mafanikio yamekuwa yakiongezeka mwaka hadi mwaka na hilo linathibitika kupitia wanafunzi waliohitimu kidato cha sita mwaka  jana (2014)  ambao idadi yao ilikuwa 256, idadi ambayo ni kubwa zaidi ukilinganisha na miaka iliyopita lakini wanafunzi wote walifaulu kati ya daraja I - III na kujiunga na vyuo Vikuu mbalimbali vya elimu ya juu ndani na nje ya nchi.
Vilevile, alisema mwaka 2014 shule ilikuwa  na wanafunzi 208 wa kidato cha nne na wote wamefaulu mitihani yao kwa alama za juu kwa ufaulu wa daraja la kwanza, la pili na wachache walipata daraja la tatu na kwamba mafanikio hayo ndiyo yanayoifanya shule hiyo kukua kwa kasi.
“Kutokana na juhudi hizi za ndani ya shule tumejikuta tukienenda vema na kuzingatia mpango wa serikali wa “Matokeo makubwa sasa” (Big Result Now) maarufu kama BRN kwani shule ilishakuwa na mikakati na mipango yake ambayo kimsingi inatuweka katika nafasi nzuri ya kutekeleza na kupata matokeo makubwa sasa,” alisema Rugambwa.
WAZIRI wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernard Membe, akizungumza na wanafunzi wa shule ya sekondari Tusiime kuhusu masuala mbalimbali ya kitaifa na kimataifa ambapo wanafunzi hao walipata nafasi ya kumuuliza maswali na kuyajibu kabla hajafungua maabara ya sayansi na maktaba na mahafali ya tano ya kidato cha sita ya shule hiyo. Wengine wanaoonekana ni wageni alioambatana nao na walimu wa Tusiime.

WAZIRI wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernard Membe, akikata utepe kuzindia maabara ya kisasa ya sayansi na maktaba ya shule ya sekondari Tusiime kabla yajatoa vyeti kwa wahitimu wa kitado cha tano wa shule hiyo. Wengine ni kushoto ni Mwenyekiti wa Bodi, Dk. John Mbogoma kulia kwa Waziri ni  Mkurugenzi wa shule hizo, Albert Katagira, Meneja wa shule Jane Katagira, na Mkuu wa shule ya sekondari Tusiime, Emil Rugambwa.

Monday, 11 March 2013

SIKU WAFANYAKAZI WA AFRICAN BARRICK GOLD MINNING WALIPOTOA MSAADA KWA WAGONJWA WA SARATANI IKIWA NI MAADHIMISHO YA SIKU YA MWANAMKE DUNIANI

kampuni ya uchimbaji madini ya African Barrick Gold (ABG) wakikabidhi msaada wa vitu mbalimbali yakiwemo maboksi ya sabuni za kufulia na kuogea, mafuta ya kula, jozi za khanga na vitenge kwa wagonjwa waliolazwa kwenye Taasisi ya Saratani ya Ocean Road (ORCI) iliyopo jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki iliyopita, ikiwa ni shemu ya Maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani.

Wafanyakazi wa kampuni ya uchimbaji madini ya African Barrick Gold (ABG) wakiongozwa na afisa wa kampuni hiyo, Blandina Munghezi (wa pili kushoto), wakikabidhi sehemu ya msaada wa vitu mbalimbali yakiwemo maboksi ya sabuni za kufulia na kuogea, mafuta ya kula, jozi za khanga na vitenge kwa Afisa Muuguzi wa Taasisi ya Saratani ya Ocean Road (ORCI), Sophia Kissuda Lesso, kwa ajili ya kuwasaidia wagonjwa wanawake waliolazwa katika taasisi hiyo, jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki iliyopita, ikiwa ni shemu ya Maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani.

Wafanyakazi wa kampuni ya uchimbaji madini ya African Barrick Gold (ABG) wakiongozwa na afisa wa kampuni hiyo, Blandina Munghezi (wa pili kushoto), wakikabidhi msaada wa kitenge kwa Mgonjwa Asha Ramadhani mkazi wa Songea mkoani Ruvuma aliyelazwa katika  Taasisi ya Saratani ya Ocean Road (ORCI), wakati wafanyakazi wa kampuni hiyo, walipotoa msaada wa vitu mbalimbali yakiwemo maboksi ya sabuni za kufulia na kuogea, mafuta ya kula, jozi za khanga na vitenge kwa ajili ya kuwasaidia wagonjwa wanawake waliolazwa katika taasisi hiyo, jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki iliyopita, ikiwa ni shemu ya Maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani.

KLM YAPATA AJALI TANGA, LILIKUWA LIKITOKEA DAR KWENDA ARUSHA

Basi mali ya Kilimanjaro Express namba za usajili T860 BVA lililokuwa likitokea Dar es salaam kwenda Arusha likiwa limepata ajali katika eneo la segera, abiria wachache walipata majeraha na kuwahishwa hospitali