Saturday, 27 October 2012

SIMBA YAIRARUA AZAM 3-1

Emmanuel Okwi kulia akiwania mpira na Aggrey Moris wa Azam katika pambano kali lililochezwa jana kwenye uwanja Mkuu wa Taifa Dar es saalam huku likishuhudia Simba ikiirarua Azam kwa bao 3-1 licha ya azam kuongoza kufunga. Okwi alipiga goli mbili mwenyewe katika mchezo huo. kwa matokeo hayo Simba imeendelea kushikilia usukani ikiongoza kwa point moja ikifuatiwa na watani wao wa jadi Yanga iliyopata ushindi kiduchu wa bao 1-0 jana dhidi ya JKT Oljoro ya Arusha.

JK AHUDHURIA MAZISHI YA LUTENI KANALI MUSSA MRISHO MTENGWA

Rais Jakaya Kikwete akiweka udongo kwenye kaburi la marehemu Luteni Kanali Mtengwa katika mazishi yaliyofanyika nyumbani kwake katika kijiji cha Kiwangwa, Bagamoyo Pwani. Rais alihudhuria maziko ya msiba huo akiwa kwenye mapumziko ya siku kuu ya Eid El Haji nyumbani kwake Msoga.

Rais Jakaya Kikwete akifariji familia ya marehemu Luteni Kanali Mussa Mrisho Mtengwa katika kijiji chake huko Kiwangwa, Bagamoyo Mkoani Pwani. Marehemu ambae alishawahi kushika nyadhifa mbalimbali Serikalini ameacha mjane, watoto wanne na wajukuu watatu.

RIZIKI POPOTE

Mkazi wa Mbughuni mirerani Asha Said akichekecha kokoto zenye chembechembe ya madini ya Tanzanite  akijaribu na yeye kutafuta madini hayo na kuuza kwa ajili ya mahitaji yake muhimu. kina mama wengi katika mji wa Mirerani  wamekuwa wakifanya shughuli hiyo kuendesha familia zao.

KARIBU MGENI

Mkurugenzi wa Heaven Wind Production Angie Morris akisalimiana na baadhi ya wakazi wa jamii ya kifugaji katika kijiji cha Lengasiti wilaya ya Simanjiro, Manyara juzi alipowatembelea. kwa hisani ya mireranitanzaniteblog

MAGAZETINI LEO JUMAPILI








Magazetini leo jumapili: kikubwa kilichojiri kwenye magazeti yetu leo hii ni UVCCM kutwangana. baadhi ya wajumbe walipotua tu Dar es salaam jana walikamatwa na wenzao na kuanza kupewa kichapo wakituhumiwa kutumia rushwa kushinda katika nyadhifa walizokuwa wakizigombea.
Kwa hisani ya mjengwablog

YANGA VS JKT OLJORO LEO SHEKH AMRI ABEID STADIUM

Askari wa Mbwa akiwa kamshikilia mbwa wake kisawasawa tayari kudhibiti mashabiki watakaoingia uwanjani mara baada ya mpia kumalizika. Yanga ilishinda 1-0 dhidi ya JKT Oljoto
Nurdin Bakari akishuka kwenye basi la Yanga kuingia kwenye chumba cha kubadilishia nguo wakijiandaa kwa pambano lao na Jkt Oljoro katika uwanja wa Shekh Amri Abeid Arusha. Yanga ilishinda 1-0 goli lilowekwa wavuni na Mbuyu Twite kipindi cha pili

Wachezaji wa Yanga wakiingia uwanjani wakitoka kwenye vyumba vya kubadilishia nguo  tayari kwa pambano lao na JKT Oljoro ya Arusha leo katika uwanja wa Shekh Amri Abeid Arusha. wa kwanza mbele ni Oscar Joshua, Frank Domayo, Shadrack Nsajigwa na Mbuyu Twite .  Yanga ilishinda 1-0.