Saturday, 27 October 2012

JK AHUDHURIA MAZISHI YA LUTENI KANALI MUSSA MRISHO MTENGWA

Rais Jakaya Kikwete akiweka udongo kwenye kaburi la marehemu Luteni Kanali Mtengwa katika mazishi yaliyofanyika nyumbani kwake katika kijiji cha Kiwangwa, Bagamoyo Pwani. Rais alihudhuria maziko ya msiba huo akiwa kwenye mapumziko ya siku kuu ya Eid El Haji nyumbani kwake Msoga.

Rais Jakaya Kikwete akifariji familia ya marehemu Luteni Kanali Mussa Mrisho Mtengwa katika kijiji chake huko Kiwangwa, Bagamoyo Mkoani Pwani. Marehemu ambae alishawahi kushika nyadhifa mbalimbali Serikalini ameacha mjane, watoto wanne na wajukuu watatu.

No comments:

Post a Comment