Wafanyakazi
wa kampuni ya uchimbaji madini ya African Barrick Gold (ABG)
wakiongozwa na afisa wa kampuni hiyo, Blandina Munghezi (wa pili
kushoto), wakikabidhi sehemu ya msaada wa vitu mbalimbali yakiwemo
maboksi ya sabuni za kufulia na kuogea, mafuta ya kula, jozi za khanga
na vitenge kwa Afisa Muuguzi wa Taasisi ya Saratani ya Ocean Road
(ORCI), Sophia Kissuda Lesso, kwa ajili ya kuwasaidia wagonjwa wanawake
waliolazwa katika taasisi hiyo, jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki
iliyopita, ikiwa ni shemu ya Maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani. |