Thursday, 7 February 2013

RIDHIWANI KIKWETE ALIPOIKANA TANZANIA LOAN SOCIETY

TAARIFA KWA UMMA JUU YA TANZANIA LOAN SOCIETY

Habari zenu mabibi na mabwana, marafiki zangu wa kwenye mtandao na wale wasio marafiki zangu ambao naamini kwa namna moja au nyengine mtakapo soma habari hii mtaipeleka kwa jamaii inayowazunguka ili kuweka hali vizuri .

Maisha ni kuhangaika na kwamba inataka mtu anayefahamu njia sahihi kuweza kujua kuwa nikitumia njia hii hali itakuwa sawa na pengine mambo yangu yatanyooka. Hii inaweza kuwa ndiyo maana halisi ya hangaika ufanikiwe lakini tafsiri hii haiwezi kuwa kutumia njia za kudhulumu, kukaba, kuiba au kufanya utapeli ili ufanikishe malengo yako mabaya dhidi ya mtu au kikundi fulani cha watu.

Hivi karibuni nimekuwa napokea sana emails, sms, na hata tweets juu ya kitu kinachoitwa TANZANIA LOAN SOCIETY, ambacho kwa namna moja au nyengine kinaonekana kuwa ni mradi ambao umeanzia katika mikono ya Rais Barack Obama kuja Tanzania kupitia Rais Dr. Jakaya Kikwete na sasa mimi nikishirikiana na Waziri Mkuu Mh. Mizengo Kayanza Pinda tunauendesha, jambo ambalo si la ukweli hata kidogo na naomba kutumia nafasi hii kulikanusha kabisa mbele ya umma wa Watanzania na wale wote ambao kwa namna moja au nyengine wanafuatilia ninavyotuma kwenye kurasa hii.

Kwa masikitiko makubwa sana napenda kuweka hadharani kuwa JAMBO HILI SI LA KWELI na kwamba HAKUNA KITU na kwa yeyote ambaye atakuwa ametoa hela yake basi atakuwa AMETAPELIWA.

Kwa upande wangu niwaombe ndugu zangu na vijana wenzangu watanzania kuwa makini sana na mambo haya ya mitandao maana wanaotangaza vitu kama hivi wanaweza kuwa na nia mbalimbali ikiwemo, KUTUMIA JINA LANGU ILI KUWAIBIA WATU, lakini pia KUTUMIA JINA LANGU ILI KUNICHAFUA, au kutumia NJIA HII IIKIWA NI SEHEMU YA KUJIPATIA KIPATO KISICHO HALALI.

Hivyo ni ushauri wangu kwenu vijana wenzangu ambao ninaamini kuwa muliamini kuwa jambo hili ni ukweli kuacha kuamini vitu mnavyoviona pasi kuwa na taarifa za uwakika.tuwe wepesi wa kuuliza kabla hatujajaribu maana VYENGINE NI SUMU NA HAVIONJEKI.

Nimalize kwa kuwashukuru wote ambao kwa namna moja au nyengine wamekuwa wakinipigia simu kunijulisha na hata wale walioandika ujumbe mfupi wa maneno na pia kuwapa pole wote ambao kwa namna moja au nyengine wameathiriwa na jambo hili. Haikuwa nia yangu kuona dhuruma hii ikitokea ila ni ukweli kuwa lazima uelewe vizuri kuwa uchunguzi wa kina lazima ufanyike na kujiridhisha pasipo kukurupuka maana unaweza kufanya jambo kumbe ndiyo unalikuza. Nniwaombe wale ambao kwa namna moja au nyengine kurasa zao za Face book zimetumika kurusha matangazo haya ya kiutapeli.

MIMI NDUGU YENU
RIDHIWANI JAKAYA KIKWETE

VICHWA VYA HABARI MAGAZETINI LEO ALHAMISI 7/01/013


Monday, 4 February 2013

TASWIRA ZAIDI HAPPY BIRTHDAY YA CCM

Vijana wa Chipukizi wakiimba wimbo wa Kwaya katika maadhimisho hayo

Vijana wa Chipukizi wa CCM wakipita kwa Gwaride la Heshima na Utii mbele ya Rais Jakaya Kikwete.

Wananchi wakiwa wamefurika kwenye uwanja wa Lake Tanganyika.

Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdurahman Kinana akizungumza katika maadhimisho hayo.

Kikundi cha ngoma kutoka nchini Burundi kikitumuiza katika maadhimisho hayo yaliyofanyika leo kwenye uwanja wa Lake Tanganyika.

Katibu wa Halmashauri Kuu ya CCM Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akizungumza katika maadhimisho hayo katika uwanja wa Lake Taganyika.

Msanii Diamond akiongoza kundi lake katika kutoa burudani kwa wananchi waliojitokeza katika maadhimisho hayo.

Waziri wa Uchukuzi Dk. Harrison Mwakyembe akizungumzia mikakati ya Serikali katika maadhimisho hayo juu ya urejeshaji wa huduma za treni katika kituo cha Reli ya Kati cha Kigoma.

Rais Jakaya Kikwete akiangalia picha zilizochorwa zikimuonesha yeye na Hayati Baba wa Taifa Mwalimu Julius K. Nyerere wakati alipotembelea mabanda ya maonyesho katika maadhimisho ya miaka 36 ya CCM

Rais Jakaya Kikwete akiangalia ndizi zinazozalishwa mkoani Kigoma katika banda la wakulima wa ndizi kutoka mkoa huo.
Rais wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania na Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi Dk. Jakaya Kikwete akihutubia wananchi katika sherehe za miaka 36 ya CCM zilizofanyika jioni ya leo kwenye uwanja wa Lake Tanganyika Mkoani Kigoma na kuhudhuriwa  na wananchi mbalimbali waliojitokeza kushiriki katika sherehe hizo.


Rais Jakaya Kikwete akiwapungia mkono wananchi wa mkoa wa Kigoma waliojitokeza kwenye maadhimisho ya miaka 36 ya CCM kwenye uwanja wa Lake Tanganyika

Wananchi mbalimbali wakiwa wamejitokeza kwenye uwanja wa Lake Tanganyika.

Katibu wa Halmashauri kuu ya CCM Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akimtunza mmoja wa wasanii wadogo wa kikundi cha ngoma kutoka nchini Burundi kilichoshiriki katika maadhimisho ya miaka 36 ya CCM.
PICHA KWA HISANI YA  mjengwablog

WAFUASI CCM/CHADEMA NGOMA WAPOPOANA KWA MAWE DODOMA

Na: Ibrahim Bakari, Dodoma na Raymond Kaminyoge, Kigoma 
SHEREHE za miaka 36 za kuzaliwa kwa CCM jana ziliingia dosari, baada ya kuibuka vurugu kubwa kati ya wafuasi wa chama hicho na Chadema mkoani Dodoma wakati wakigombea eneo na mti wa kutundika bendera za vyama vyao.Vurugu hizo
zilizotulizwa na Polisi wa Kutuliza Ghasia (FFU), zilitokea jana mchana katika uwanja huo uliopo karibu na Baa ya Mwanga, baada ya CCM kung’oa bendera ya Chadema iliyokuwepo uwanjani hapo, ili waweke bendera zao kwa ajili ya mkutano ambao ulikuwa sehemu ya maadhimisho hayo.
Vurugu zilizuka baada ya wafuasi wa Chadema kuwataka wenzao wa CCM waendelee na mkutano katika eneo hilo kwa sharti la kurejeshwa kwa bendera iliyong’olewa. Wafuasi wa vyama hivyo wakiwamo wabunge wa CCM walionekana wakivutana kunyang’anyana mti wa bendera.
“Baada ya CCM kugoma, Chadema walijaribu kurudisha bendera hiyo kwa nguvu, jambo ambalo lilifanya wafuasi wa CCM waanze kuokota mawe na kuwarushia wapinzani wao hao, huku Chadema nao walianza kujibu mapigo,” alisema mmoja wa mashuhuda wa tukio hilo.
Baadhi ya wabunge wa CCM walioshiriki katika vurugu hizo na majimbo yao kwenye mabano ni Ismail Aden Rage (Tabora Mjini), Nyambari Nyangwine (Tarime), Seleman Jafo (Kisarawe), Said Mtanda (Mchinga) na Mary Chatanda (Viti Maalumu).
Baadhi ya wafuasi wa CCM walionekana wakibeba mawe na kuwapiga wenzao wa Chadema na kusababisha tafrani kubwa katika eneo hilo la mkutano.
Katibu wa Chadema Wilaya ya Dodoma Mjini, Jellah Mambo alisema kuwa tukio hilo limetokana na wafuasi wa CCM kung’oa bendera ya Chadema iliyokuwa ikipepea eneo la Mwanga Baa kulikofanyika sherehe za chama chao (CCM).
“Kwanza wamechukua bendera yetu. Halafu tumeshangazwa na CCM kuruhusiwa kufanya maadhimisho yao wakati kuna agizo la Mkuu wa Mkoa na polisi kukataza mikusanyiko ya kisiasa wakati wa Bunge.
“Kwa nini sisi (Chadema) tuzuiwe mikutano yetu wakati wenzetu wanafanya? Huku si kutenda haki....Tulikuwa na mikutano ya kuimarisha chama katika kata kuanzia Ijumaa, Jumamosi na Jumapili, lakini tumezuiwa na tukaheshimu mamlaka,” alisema katibu huyo.
Pia tulikuwa tufanye mkutano na wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Dodoma, lakini tukazuiwa na tuliheshimu amri hiyo, alisema.
Mambo alisema katika vurugu hizo wafuasi wawili wa Chadema; Idd Kizota na Anord Swai waliumizwa na kushonwa nyuzi saba usoni.
Mganga Mkuu wa Hospitali ya Mkoa wa Dodoma, Ezekiel Mpuya alisema hana taarifa za majeruhi hao.
MWANANCHI

vichwa vya habari magazetini leo 4/02/2013















Sunday, 3 February 2013

LEMA AFANIKISHA UNUNUZI WA HEKARI TATU ZA KUJENGEA HOSPITALI YA MAMA NA MTOTO JIJINI ARUSHA

MWENYEKITI WA CHADEMA, FREEMAN MBOWE, AKITOA HOTUBA FUPI KATIKA ENEO LA KIWANJA CHA HEKARI TATU ILIYONUNUA CHADEMA  KATIKA SHAMBA LA BURKA KWAAJILI YA UJENZI WA HOSPITALI YA MAMA NA MTOTO JIJINI ARUSHAI