Thursday, 7 February 2013

RIDHIWANI KIKWETE ALIPOIKANA TANZANIA LOAN SOCIETY

TAARIFA KWA UMMA JUU YA TANZANIA LOAN SOCIETY

Habari zenu mabibi na mabwana, marafiki zangu wa kwenye mtandao na wale wasio marafiki zangu ambao naamini kwa namna moja au nyengine mtakapo soma habari hii mtaipeleka kwa jamaii inayowazunguka ili kuweka hali vizuri .

Maisha ni kuhangaika na kwamba inataka mtu anayefahamu njia sahihi kuweza kujua kuwa nikitumia njia hii hali itakuwa sawa na pengine mambo yangu yatanyooka. Hii inaweza kuwa ndiyo maana halisi ya hangaika ufanikiwe lakini tafsiri hii haiwezi kuwa kutumia njia za kudhulumu, kukaba, kuiba au kufanya utapeli ili ufanikishe malengo yako mabaya dhidi ya mtu au kikundi fulani cha watu.

Hivi karibuni nimekuwa napokea sana emails, sms, na hata tweets juu ya kitu kinachoitwa TANZANIA LOAN SOCIETY, ambacho kwa namna moja au nyengine kinaonekana kuwa ni mradi ambao umeanzia katika mikono ya Rais Barack Obama kuja Tanzania kupitia Rais Dr. Jakaya Kikwete na sasa mimi nikishirikiana na Waziri Mkuu Mh. Mizengo Kayanza Pinda tunauendesha, jambo ambalo si la ukweli hata kidogo na naomba kutumia nafasi hii kulikanusha kabisa mbele ya umma wa Watanzania na wale wote ambao kwa namna moja au nyengine wanafuatilia ninavyotuma kwenye kurasa hii.

Kwa masikitiko makubwa sana napenda kuweka hadharani kuwa JAMBO HILI SI LA KWELI na kwamba HAKUNA KITU na kwa yeyote ambaye atakuwa ametoa hela yake basi atakuwa AMETAPELIWA.

Kwa upande wangu niwaombe ndugu zangu na vijana wenzangu watanzania kuwa makini sana na mambo haya ya mitandao maana wanaotangaza vitu kama hivi wanaweza kuwa na nia mbalimbali ikiwemo, KUTUMIA JINA LANGU ILI KUWAIBIA WATU, lakini pia KUTUMIA JINA LANGU ILI KUNICHAFUA, au kutumia NJIA HII IIKIWA NI SEHEMU YA KUJIPATIA KIPATO KISICHO HALALI.

Hivyo ni ushauri wangu kwenu vijana wenzangu ambao ninaamini kuwa muliamini kuwa jambo hili ni ukweli kuacha kuamini vitu mnavyoviona pasi kuwa na taarifa za uwakika.tuwe wepesi wa kuuliza kabla hatujajaribu maana VYENGINE NI SUMU NA HAVIONJEKI.

Nimalize kwa kuwashukuru wote ambao kwa namna moja au nyengine wamekuwa wakinipigia simu kunijulisha na hata wale walioandika ujumbe mfupi wa maneno na pia kuwapa pole wote ambao kwa namna moja au nyengine wameathiriwa na jambo hili. Haikuwa nia yangu kuona dhuruma hii ikitokea ila ni ukweli kuwa lazima uelewe vizuri kuwa uchunguzi wa kina lazima ufanyike na kujiridhisha pasipo kukurupuka maana unaweza kufanya jambo kumbe ndiyo unalikuza. Nniwaombe wale ambao kwa namna moja au nyengine kurasa zao za Face book zimetumika kurusha matangazo haya ya kiutapeli.

MIMI NDUGU YENU
RIDHIWANI JAKAYA KIKWETE

No comments:

Post a Comment