Na: Ibrahim Bakari, Dodoma na Raymond Kaminyoge, Kigoma
SHEREHE
za miaka 36 za kuzaliwa kwa CCM jana ziliingia dosari, baada ya kuibuka
vurugu kubwa kati ya wafuasi wa chama hicho na Chadema mkoani Dodoma
wakati wakigombea eneo na mti wa kutundika bendera za vyama vyao.Vurugu
hizo
zilizotulizwa na Polisi wa Kutuliza Ghasia (FFU), zilitokea jana mchana
katika uwanja huo uliopo karibu na Baa ya Mwanga, baada ya CCM kung’oa
bendera ya Chadema iliyokuwepo uwanjani hapo, ili waweke bendera zao kwa
ajili ya mkutano ambao ulikuwa sehemu ya maadhimisho hayo.
Vurugu
zilizuka baada ya wafuasi wa Chadema kuwataka wenzao wa CCM waendelee
na mkutano katika eneo hilo kwa sharti la kurejeshwa kwa bendera
iliyong’olewa. Wafuasi wa vyama hivyo wakiwamo wabunge wa CCM
walionekana wakivutana kunyang’anyana mti wa bendera.
“Baada
ya CCM kugoma, Chadema walijaribu kurudisha bendera hiyo kwa nguvu,
jambo ambalo lilifanya wafuasi wa CCM waanze kuokota mawe na kuwarushia
wapinzani wao hao, huku Chadema nao walianza kujibu mapigo,” alisema
mmoja wa mashuhuda wa tukio hilo.
Baadhi
ya wabunge wa CCM walioshiriki katika vurugu hizo na majimbo yao kwenye
mabano ni Ismail Aden Rage (Tabora Mjini), Nyambari Nyangwine (Tarime),
Seleman Jafo (Kisarawe), Said Mtanda (Mchinga) na Mary Chatanda (Viti
Maalumu).
Baadhi
ya wafuasi wa CCM walionekana wakibeba mawe na kuwapiga wenzao wa
Chadema na kusababisha tafrani kubwa katika eneo hilo la mkutano.
Katibu
wa Chadema Wilaya ya Dodoma Mjini, Jellah Mambo alisema kuwa tukio hilo
limetokana na wafuasi wa CCM kung’oa bendera ya Chadema iliyokuwa
ikipepea eneo la Mwanga Baa kulikofanyika sherehe za chama chao (CCM).
“Kwanza
wamechukua bendera yetu. Halafu tumeshangazwa na CCM kuruhusiwa kufanya
maadhimisho yao wakati kuna agizo la Mkuu wa Mkoa na polisi kukataza
mikusanyiko ya kisiasa wakati wa Bunge.
“Kwa
nini sisi (Chadema) tuzuiwe mikutano yetu wakati wenzetu wanafanya?
Huku si kutenda haki....Tulikuwa na mikutano ya kuimarisha chama katika
kata kuanzia Ijumaa, Jumamosi na Jumapili, lakini tumezuiwa na
tukaheshimu mamlaka,” alisema katibu huyo.
Pia tulikuwa tufanye mkutano na wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Dodoma, lakini tukazuiwa na tuliheshimu amri hiyo, alisema.
Mambo alisema katika vurugu hizo wafuasi wawili wa Chadema; Idd Kizota na Anord Swai waliumizwa na kushonwa nyuzi saba usoni.
Mganga Mkuu wa Hospitali ya Mkoa wa Dodoma, Ezekiel Mpuya alisema hana taarifa za majeruhi hao.
MWANANCHI
No comments:
Post a Comment