Monday, 7 January 2013

PICHA MBALIMBALI RAIS JK ALIPOHUDHURIA MISA YA KUSIMIKWA KWA ASKOFU WA DAYOSISI YA KANDA YA KATI SINGIDA DKT ALEX MKUMBO

Rais Jakaya Kikwete akiwa na Askofu Mteule jimbo la Singida, Dkt Mkumbo muda mfupi baada ya kusimikwa

RAIS KIKWETE KATIKATI AKIWA NA ASKOFU MKUU WA KKKT KULIA PAMOJA NA ASKOFU MTEULE WA DAYOSISI YA KATI DKT MKUMBO WA KWANZA KULIA

Rais  Jakaya Kikwete (wa tatu kushoto) akiwa kwenye picha ya pamoja na Askofu mteule wa KKKT dayosisi ya kati, Dk.Alex Mkumbo na msaidizi wake Cprian Yohana Hilinti (wa pili kulia).Akina mama hao ni wake wa askofu Dk.Mkumbo na msaidizi Hilinti. (Picha na Nathaniel Limu).

RAIS JAKAYA KIKWETE AKISALIMIANA NA ASKOFU MKUU WA KKKT ALEX MALASUSA MJINI SINGIDA JANA

RAIS KIKWETE KATIKA KIKAO CHA NDANI NA VIONGOZI WA MKOA WA TABORA

RAIS KIKWETE AKIKAGUA TAARIFA ZA MAENDELEO YA MKOA WA TABORA FATMA MWASA, RAIS KIKWETE YUKO MKOANI TABORA KWA ZIARA YA KIKAZI

RAIS KIKWETE KATIKA PICHA YA PAMOJA NA MAASKOFU WA KKKT PAMOJA NA MKUU WA MKOA WA SINGIDA PARSEKO KONE ALIYEVAA TAI NYEKUNDU PEMBENI MWA ASKOFU MKUU KKKT ALEX MALASUSA


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Dk.Jakaya Mrisho Kikwete,ameyahimiza madhehebu mbalimbali ya dini nchini, kufufua utaratibu uliokuwepo zamani wa kufanya vikao  baina yao, ambavyo pamoja na mambo mengine,vilisaidia kuimarisha mahusiano mazuri na kuheshimiana.
Dk.Kikwete ametoa wito huo jana (6/1/2013) wakati akizungumza kwenye sherehe za kusimikwa kwa askofu mteule wa Kanisa la kiinjili la kilutheri dayosisi ya kati,Dk.Alex Seif Mkumbo, kuongoza kanisa hilo kwa kipindi cha miaka mitano ijayo.  Alisema utaratibu huo uliepusha vitendo vya kukashifiana, kudharaulina na kutokuvumiliana.
Alisema hivi sasa vitendo vya kudharauliana,kuchochea vurugu na chuki baina ya madhehebu ya dini,vimechangiwa kwa kiasi kikubwa na kuachwa kwa utaratibu huo ambao ulisaidia mno kudumisha amani na utulivu.
“Hivi sasa watu wanasema sana, wala hawaogopi kusema,mambo sasa hivi ni tofauti mno.Wapo watu wanakipaji cha kuchochea chuki na kuchochea kudharauliana kwa  dhehebu moja na jingine.Bila vikao vya madhdhebu ya dini,watu hawa watasababisha hata uhuru wa kuabudu kutoweka”,alisema na kuongeza; “Utaratibu huu wa kukutana madhehebu kwa madhehebu,utaepusha taifa letu na machafuko  ya kidini”.
Dk.Kikwete alisema kutokana na ukweli huo,upo umuhimu kwa madhehebu ya dini kufufua/kuhuisha utaratibu wa kufanya vikao baina ya madhehebu  ili amani,utulivu,kuheshimiana na kuvumiliana kuweze kudumu.
Aidha,ametumia  fursa hiyo kuwahimiza viongozi wa madhehebu  kutekeleza majukumu yao bila kuchoka ikiwemo kuhimiza uadilifu na kukemea vitendo vyote viovu katika jamii.
Awali askofu mkuu wa KKKT nchni.Dk.Alex Mwalasusa, alimwahidi rais Kikwete kuwa wataendelea kushirikiana na serikali katika kuwaendeleza Watanzania kiroho na kimwili.

TUME YAKATIBA YATINGA KADA ZA VYAMA VYA SIASA, LEO WAMECHUKUA MAONI CHADEMA NA CUF

Mmoja wa Viongozi wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Andrew Chenge akiwasilisha maoni ya chama chake kuhusu Katiba Mpya katika mkutano na Tume ya Mabadiliko ya Katiba leo (Jumatatu, Jan 7, 2013) katika Ukumbi wa Karimjee jijini Dar es Salaam

Mwenyekiti wa Chama cha Wananchi (CUF) Prof. Ibrahim Lipumba akiwasilisha maoni ya chama chake kuhusu Katiba Mpya mbele ya Tume ya Mabadiliko ya Katiba leo (Jumatatu, Jan 7, 2013) katika Ofisi za Tume jijini Dar es Salaam. Kulia ni Mwenyekiti wa Tume Jaji Joseph Warioba na kulia kwa Prof. Lipumba ni Katibu wa Tume Assaa Rashid

Wajumbe wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba (kulia) wakiongozwa na Dkt. Salim Ahmed Salim waKIpokea maoni kuhusu Katiba Mpya kutoka kwa uongozi wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) ukiongozwa na Mwenyekiti wao Freeman Mbowe katika mkutano kati ya chama hicho na Tume ya Mabadiliko ya Katiba, Ukumbi wa Karimjee jijini Dar es salaam leo (Jumatatu, jan. 7, 2012).

HATA KATIKATI YA JIJI LA DAR ES SALAAM (KARIAKOO),KUNA NYUMBA ZA UDONGO

JENGO BOVU KATIKATI YA JIJI LA DSM-KARIAKOO

BIBI MPOLE AKIENDELEA KUSAKA VIWALO NDANI YA JIJI LA DSM KARIAKOO

HATA KWA WAUZA POCHI HAKUWA NYUMA, HAPA ANAONEKANA AKIENDELEA KUCHAGUA

ANAYENIFANYA KUPENDEZA KILA SIKU ALIYEVAA KITAMBAA CHA PUPLE AKICHAGUA BIDHAA KATIKATI YA KARIAKOO

JENGO HILI LIPO KATIKATI YA JIJI LA DAR ES SALAAM KARIBU NA MTAA WA KONGO

WAFANYABIASHARA KARIAKOO MTAA WA KONGO WAKIENDELEA NA SHUGHULI ZAO ZA KILA SIKU, KAMA WANAVYOONEKANA PICHANI

VICHWA VYA HABARI MAGAZETINI LEO - JUMATATU 1/07/2013


















Thursday, 3 January 2013

MDAU OMARY YUSUF CHANYIKA ALIPOAMUA KUUAGA UKAPERA NA KUFUNGA NDOA



Baba mzazi wa Omar Yusuf, Yusuf Chanyika akitoa nasaha kwa maharusi katika hafla iliyofanyika Dec 29,2012 nyumbani kwao Magila Mkumbara Mombo wilayani Korogwe, Kulia ni mke wa Yusuf Mainda.


PICHA MBALIMBALI SOKO LA MKUMBARA, MOMBO WILAYANI KOROGWE MKOANI TANGA

WAFANYABIASHARA WAKIUZA MBOGA AINA YA NGOGWE, SOKO LA MKUMBARA NI MAARUFU KWA KUUZA MBOGA HIZO AMBAZO HUTUMIKA KUTENGENEZEA MLENDA


MFANYABIASHARA AKIWA AMEPUMZIKA AKISUBIRI WATEJA KUNUNUA BIDHAA ZAKE ALIZOZITANDAZA NDANI YA SOKO LA MKUMBARA




MAANDALIZI YA UJENZI WA MABANDA

KINA MAMA WA KIMASAI WAKINUNUA BIDHAA MBALIMBALI NDANI YA SOKO LA MKUMBARA, SOKO HILI HUFANYIK KILA SIKU YA IJUMAA YA MWISHO WA MWEZI, HAPA ILIKUWA TAREHE 29/DEC/2012

MDAU, ALLY KANJU AKIKATIZA MITAA YA SOKO LA MKUMBARA ALIPOKUWA LIKIZO YA MAPUMZIKO YA X-MASS NA MWAKA MPYA PAMOJA NA KUHUDHURIA HARUSI YA MDAU OMARI YUSUF CHANYIKA ILIYOFANYIKA NYUMBANI MKUMBARA

MAANDALIZI YA SOKO, WAFANYABIASHARA WAKIJENGA VIBANDA KWA AJILI YA KUWEKA BIDHAA ZAO KATIKA SOKO LA MKUMBARA


WANUNUZI NA WAFANYABIASHARA WAKIENDELEA NA SHUGHULI NDANI YA SOKO LA MKUMBARA LILILOKO KATIKA KIJIJI CHA MAGILA, MOMBO WILAYANI KOROGWE


Tuesday, 1 January 2013

HATIMAYE MWENYEZI MUNGU AMEMPENDA ZAIDI SAJUKI - INALILAH INAILAH RAJIUN




Baada ya kuugua kwa muda mrefu, hatimaye aliyekuwa muigizaji wa filamu nchini, Juma Kilowoko maarufu kama Sajuki amefariki dunia leo alfajiri katika hospitali ya Muhimbili jijini Dar es Salaam.


Kwa mujibu wa Katibu wa chama cha waongoza Filamu Wilaya ya Ilala, Rajabu Amiri hivi karibuni Sajuki alikuwa anasumbuliwa na tatizo la upungufu wa damu,mgongo na  kansa  ya ngozi

Sajuki alikuwa akitakiwa kurejea tena nchini India kwaajili ya kuendelea na matibabu ya tatizo lililokuwa likimsumbua ambapo jumla ya shilingi milioni 28 zilikuwa zikihitajika.

Hivi karibuni ilidaiwa kuwa alikuwa ameshakusanya shilingi milioni saba tu zilizotokana na michango ya watu na show alizokuwa akizifanya kukusanya fedha hizo. Show ya mwisho aliifanya jijini Arusha ambako alianguka kwenye stage.

Kifo hicho cha Sajuki kimepokelewa kwa masikitiko makubwa kutoka kwa watu mbalimbali wakiwemo mastaa wa Tanzania waliotumia mitandao ya kijamii kuelezea masikitiko yao.

Mwasiti Almas
Tunapolala na kuamka tunasema AHSANTE kwa mungu,tunapopoteza pia tunaowapenda tuseme AHSANTE… alichokileta ALLAH chini ya jua atakichukua

Salama A. Jabir
Mwenyezi Mungu Akusamehe Makosa Yako Ndugu Yetu Juma Kilowoko..Ucheshi Wako Ntaukumbuka Milele. Pumzika Kwa Amani Rafiki. #RIPSajuki

Jokate Mwegelo
Nimesikia hii habari sasa. Sad lakini kazi ya Mungu haina makosa tunazidi kumtumainia yeye na kumshukuru. Upumzike kwa amani sajuki. Amen!!

Zitto Zuberi Kabwe
Hali ya Afya ya Sajuki ndiyo ilinisukuma sana kuanza kusaidia wasanii nchini kupata kipato stahili na kazi Yao. Kifo chake kimeniondolea Mtu niliyemtazama kama kishawishi Cha Mimi kupigania haki za Watanzania walio kwenye entertainment industry. Sajuki left an indelible mark in my politics. Pumzika Kwa Amani Juma.
Masanja ‏Mkandamizaji
Duniani si nyumbani kwetu. Ni njia tu.

Hemedy Suleiman
R.I.P SAJUKI……..daaaaaah this is painful!!

Arnold Kayanda
Pamoja na kuwa Msiba wowote unanisikitisha ila wa Sajuki unanisikitisha zaidi kila napoikumbuka Historia yake na Mkewe!