Rais Jakaya Kikwete akiwa na Askofu Mteule jimbo la Singida, Dkt Mkumbo muda mfupi baada ya kusimikwa |
RAIS KIKWETE KATIKATI AKIWA NA ASKOFU MKUU WA KKKT KULIA PAMOJA NA ASKOFU MTEULE WA DAYOSISI YA KATI DKT MKUMBO WA KWANZA KULIA |
RAIS JAKAYA KIKWETE AKISALIMIANA NA ASKOFU MKUU WA KKKT ALEX MALASUSA MJINI SINGIDA JANA |
RAIS KIKWETE KATIKA KIKAO CHA NDANI NA VIONGOZI WA MKOA WA TABORA |
RAIS KIKWETE AKIKAGUA TAARIFA ZA MAENDELEO YA MKOA WA TABORA FATMA MWASA, RAIS KIKWETE YUKO MKOANI TABORA KWA ZIARA YA KIKAZI |
RAIS KIKWETE KATIKA PICHA YA PAMOJA NA MAASKOFU WA KKKT PAMOJA NA MKUU WA MKOA WA SINGIDA PARSEKO KONE ALIYEVAA TAI NYEKUNDU PEMBENI MWA ASKOFU MKUU KKKT ALEX MALASUSA |
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Dk.Jakaya Mrisho Kikwete,ameyahimiza
madhehebu mbalimbali ya dini nchini, kufufua utaratibu uliokuwepo
zamani wa kufanya vikao baina yao, ambavyo pamoja na mambo
mengine,vilisaidia kuimarisha mahusiano mazuri na kuheshimiana.
Dk.Kikwete
ametoa wito huo jana (6/1/2013) wakati akizungumza kwenye sherehe za
kusimikwa kwa askofu mteule wa Kanisa la kiinjili la kilutheri dayosisi
ya kati,Dk.Alex Seif Mkumbo, kuongoza kanisa hilo kwa kipindi cha miaka
mitano ijayo. Alisema utaratibu huo uliepusha vitendo vya kukashifiana,
kudharaulina na kutokuvumiliana.
Alisema
hivi sasa vitendo vya kudharauliana,kuchochea vurugu na chuki baina ya
madhehebu ya dini,vimechangiwa kwa kiasi kikubwa na kuachwa kwa
utaratibu huo ambao ulisaidia mno kudumisha amani na utulivu.
“Hivi
sasa watu wanasema sana, wala hawaogopi kusema,mambo sasa hivi ni
tofauti mno.Wapo watu wanakipaji cha kuchochea chuki na kuchochea
kudharauliana kwa dhehebu moja na jingine.Bila vikao vya madhdhebu ya
dini,watu hawa watasababisha hata uhuru wa kuabudu kutoweka”,alisema na
kuongeza; “Utaratibu huu wa kukutana madhehebu kwa madhehebu,utaepusha
taifa letu na machafuko ya kidini”.
Dk.Kikwete
alisema kutokana na ukweli huo,upo umuhimu kwa madhehebu ya dini
kufufua/kuhuisha utaratibu wa kufanya vikao baina ya madhehebu ili
amani,utulivu,kuheshimiana na kuvumiliana kuweze kudumu.
Aidha,ametumia
fursa hiyo kuwahimiza viongozi wa madhehebu kutekeleza majukumu yao
bila kuchoka ikiwemo kuhimiza uadilifu na kukemea vitendo vyote viovu
katika jamii.
Awali
askofu mkuu wa KKKT nchni.Dk.Alex Mwalasusa, alimwahidi rais Kikwete
kuwa wataendelea kushirikiana na serikali katika kuwaendeleza Watanzania
kiroho na kimwili.
No comments:
Post a Comment