Monday, 7 January 2013

TUME YAKATIBA YATINGA KADA ZA VYAMA VYA SIASA, LEO WAMECHUKUA MAONI CHADEMA NA CUF

Mmoja wa Viongozi wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Andrew Chenge akiwasilisha maoni ya chama chake kuhusu Katiba Mpya katika mkutano na Tume ya Mabadiliko ya Katiba leo (Jumatatu, Jan 7, 2013) katika Ukumbi wa Karimjee jijini Dar es Salaam

Mwenyekiti wa Chama cha Wananchi (CUF) Prof. Ibrahim Lipumba akiwasilisha maoni ya chama chake kuhusu Katiba Mpya mbele ya Tume ya Mabadiliko ya Katiba leo (Jumatatu, Jan 7, 2013) katika Ofisi za Tume jijini Dar es Salaam. Kulia ni Mwenyekiti wa Tume Jaji Joseph Warioba na kulia kwa Prof. Lipumba ni Katibu wa Tume Assaa Rashid

Wajumbe wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba (kulia) wakiongozwa na Dkt. Salim Ahmed Salim waKIpokea maoni kuhusu Katiba Mpya kutoka kwa uongozi wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) ukiongozwa na Mwenyekiti wao Freeman Mbowe katika mkutano kati ya chama hicho na Tume ya Mabadiliko ya Katiba, Ukumbi wa Karimjee jijini Dar es salaam leo (Jumatatu, jan. 7, 2012).

No comments:

Post a Comment