RAIS Jakaya Kikwete
anatarajiwa kuzindua chuo kikuu cha Sayansi na na teknolojia cha Nelson
Mandela jijini Arusha utakaofanyiaka Novemba 2 mwaka huu.
Uzinduzi huo unatokana na kukamilika
kwa ukarabati na uboreshaji wa majengo ya chuo umekamilika kwa asilimia 90 na
kugharimu kiasi cha shilingi bilioni 90.
Aidha uzinduzi huo utaambatana na harambee ya kuchangia uzinduzi wa mfuko
wa dhamana wa chuo hicho utakaofanikisha chuo hicho kujiendesha
chenyewe na kwamba viongozi mbalimbali waserikali watahudhulia akiwemo makamu
wa Rais Dk.Ghalib Bilal.
Akizungumza na waandishi wa habari chuoni hapo, makamu mkuu wa chuo
hicho,Profesa Burton Mwamila alisema kuwa taratibu za uzinduzi huo zimekamilika
kwa asilimia 100 huku wageni mashuhuri duniani wakitarajiwa kuhudhulia katika
sherehe hizo .
Alisema chuo cha Nelson Mandela
kilianzishwa na serikali baada ya kuasisiwa na rais mstaafu wa Afriaka
kusini,Mzee Nelson Mandela ambaye hataweza kuhudhulia kutokana na matatizo ya
kiafya, kwa lengo la kutoa mafunzo na kufanya utafiti katika maeneo mbalimbali
ya fani ya sayansi,uhandisi na teknolojia na tayari kimeanza kupokea wanafunzi
kutoka ndani na nje ya nchi.
Alisema ukarabati na uboreshaji wa
majengo yaliyokuwa yakimilikiwa na CAMATEC ulianza Agosti 10 mwaka
2010 na ilipofika oktoba 2011 chuo hicho kilidahili kundi la kwanza la
wanafunzi wapatao 83,kati yao 30 wakichukua masomo ya uzanivu na 53 ya uzamili.
Aidha aliongeza kuwa chuo hicho kwa
sasa kina jumla ya wanafunzi 217 na kwamba katika mwaka huu wa masomo ,chuo
kimedahili wanafunzi 135 wa kundi la pili ,huku kati yao 46 wakichukua masomo
ya uzanivu na 89 wakichukua masomo ya uzamili.
Akizungumzia hali ya ubora wa elimu
unaotolewa katika chuo hicho alisema kuwa chuo kinawataalamu mbalimbali kutoka
vyuo mbalimbali hapa duniani na kwamba kimekuwa kikishirikiana kwa ukaribu na
vyuo mbalimbali vilivyoko katika nchi 10 duniani.
‘’tumeanzisha ushirikiano wa
kitaaluma na vyuo vikuu mbalimbali hapa duniani, ambapo kwa kuanzia
tunashirikiana na nchi za Marekani ,Uingereza,Sweden,Itary ,Urusi ,Korea
Kusini,India,Ubeligiji na Swazland’’alisema Prof Mwamilwa.
Alisema makubaliano na vyuo hivyo ni
kushirikiana katika kufundisha ambapo walimu waliopo kwenye vyuo hivyo wakuwa
wakija kufundisha huku pia walimu waliopo chuoni hapo wakipata fursa ya
kujifunza katika vyuo hivyo na kwamba walimu ambao hawatafika watakuwa wakiitoa
elimu kwa njia ya mtandao.
Alisisitiza kuwa kwa sasa chuo hicho
kina jumla ya maprofesa 16 wenye upeo mkubwa wa kufundisha masomo mbalimbali
kutoka nchi mbalimbali ikiwemo Rwanda na Burundi ambao wameajiriwa kwa ajili ya
kufundisha na kutoa elimu iliyobora inayokubalika kimataifa.
Aidha alisisitiza kuwa uzinduzi huo
utatanguliwa na maonyesho mbalimbali ya elimu, burudani kutoka vikundi
mbalimbali vya wasanii ,uwekaji wa jiwe la msingi utakaofanywa na Rais
Kikwete,pamoja na kutembelea majengo ya chuo.
Mwisho.