Mmoja wa wakazi wa singisi akiwa nje ya nyumba yake pamoja na watoto wake akitafakari namna ya kushi baada ya nyumba yake kubomolewa juzi usiku. |
FAMILIA tano katika kata ya Sing”isi wilayani Arumeru
Mashariki mkoani Arusha juzi zililazimika kulala nje kufuatia nyumba zao
kubomolewa kwa kile kinachoelezwa kuwa ni amri ya wawekezaji raia wa kigeni.
Unyama huo ambao unadaiwa kufanywa na wawekezaji hao ambao
ni wamiliki wa mashamba makubwa wilayani humo taarifa zaidi zinasema Wananchi hao wametendewa unyama huo baada ya
viongozi wa kata na kijiji kuhongwa.
Hatahivo,familia hizo zenye wakazi zaidi ya 30 zinazoelezwa
kuishi karibu na mashamba hayo maarufu kama mito miwili, zimeiangukia serikali na kuitaka iingilie kati
sakata hilo kwa madai kwamba wanateseka kwa kuishi na hofu ,kukosa chakula
sanjari na watoto wao kutohudhuria masomo mashuleni.
Tukio hilo wakazi hao ambalo lilitokea saa 6.30 usiku wa kuamkia Oktoba 26 imeelezwa
kuwa wakiwa wamelala madalali wa wawekezaji wa kigeni wanaomiliki mashamba
makubwa walivamia katika makazi yao na kisha kuwatoa nje kabla kabla ya kuanza
kubomoa nyumba zao.
Wakizungumza na waandishi wa habari waliotembelea eneo hilo
juzi wakazi hao walisema kwamba watu hao mara baada ya kuwatoa nje
waliwakusanya na kisha kuwafungia katika chumba kimoja na kisha kuanza kubomoa
nyumba zao.
Fataeli Macha na mkewe Helen Macha ni miongoni mwa wahanga
wa tukio hilo ambao kwa pamoja wanasema wao ni wakazi halali wa maeneo hayo
tangu miaka ya sitini baada ya kupata maeneo hayo kutoka kwa wazazi wao.
Wanasema mbali ya kubomolewa nyumba zao pia waliofanya zoezi
hilo waliwapora mali mbalimbali kama
simu,radio,fedha kisha kutokomea kusikojulikana.
Kwa nyakati tofauti wakazi hao walisema kwamba watu hao
kabla ya kuanza kubomoa nyumba zao waliwakuwa wakiwatamkia maneno ya kwamba
kwanini wamekataa kulipwa fidia ili waondoke katika makazi hayo na kisha
wwaachie wawekezaji.
“Walikuwa wanatuambia ya kwamba kwanini tumekataa kulipwa
fidia ili tuhame katika makazi haya na tuwaachie wawekezaji”walisema kwa
nyakati tofauti
Kwa upande wake Rehema Mohamed na Amina Idd walisema kwamba watu hao
walikuwa wamevalia kofia na makoti meusi ambapo baadhi yao walipigwa na vitu
vizito kabla ya zoezi la kubomolewa nyumba zao.
Kwa pamoja walimtaja mtu mmoja aliyetambulika kwa jina la
Kileo kwamba ndiye dalali wa wawekezaji wa kigeni wanaomiliki mashamba makubwa
yaliyopo karibu na makazi yao kwamba amekuwa akiwashawishi wao kupokea fedha za
fidia ili wapishe lakini wamekataa.
katika picha mmoja wa wakazi wa singisi akionekana mwenye huzuni mara baada ya nyumba yake kubomolewa kwa kile kinachoelezwa kuwa ni amri ya wawekezaji. |
No comments:
Post a Comment