Maelezo
31/10/2012
KAMPUNI ya usambazaji na utengenezaji filamu nchini Steps Entertainment imeahidi
kushirikiana na serikali kupambana na wanaokiuka sheria ya filamu na michezo ya kuigiza ya
mwaka 1976.
Hayo yamesemwa jana na meneja Mkuu wa Steps Entertainment Bw. Jairaj Almoradan jijini Dar
es salaam wakati wa mkutano na Sekretatieti ya Bodi ya filamu Tanzania.
Bw.Almoradan amesema kampuni yake haitapokea kazi za wasanii wasiofuata sheria kwa
kutengeneza filamu zilizo kinyume na maadili na zilizo kinyume na sheria.
Amesema kuwa sheria inawataka kutengeneza filamu zinazofuata maadili na kuwasilisha master
kopi kwa ajili ya kuidhinishwa kuingia sokoni.
“tutajitahidi kuwaeleza wasanii na tutakuwa wakali kutopokea filamu ambazo tunaona zipo
kinyume na maadili na utamaduni wetu.”Amesema Bw. Almoradan.
Kwa upande wake Katibu Mtendaji wa Bodi ya Ukaguzi wa Filamu Bi. Joyce Fissoo amesema
bodi imekuwa ikipata malalamiko kuhusiana na baadhi ya filamu kuwa kinyume na maadili ya
Mtanzania.
“Sisi kama bodi kazi yetu ni kukagua filamu na matangazo yake kama yapo kimaadili
na yamefata sheria ikiwa ni pamoja na kuzipa madaraja filamu hizo kabla hazijaenda
sokoni.”amesema Bi.Fissoo.
No comments:
Post a Comment