Thursday 14 February 2013

KATIBU WA BUNGE ATOA UFAFANUZI WA MKUTANO WA BUNGE ULIOMALIZIKA DODOMA, AKIRI BAADHI YA WABUNGE KUKIUKA KANUNI.

Katibu wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Thomas Kashilila akitoa ufafanuzi kwa   waandishi wa habari kuhusu ukiukwaji wa kanuni za bunge uliofanywa na baadhi ya wabunge wakati wa   mkutano wa 10 wa bunge uliomalizika mjini Dodoma na mabadiliko yaliyofanyika kwa baadhi ya kamati kuondolewa  pamoja na uundwaji wa kamati mpya 3 zitakazoshughulikia Ushirikiano wa Afrika, Mashariki, Bajeti, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa.

Dkt. Thomas Kashilila akitoa somo kwa waandishi wa habari kuhusu umuhimu wa wabunge kuzisoma na kuzitumia ipasavyo  kanuni za bunge ili kuondoa manug'uniko yanayojitokeza pindi wanapozuiliwa na spika kuchangia mijadala au kutoa hoja bungeni kwa sababu ya kukiuka kanuni za bunge huku akiwasisitiza waandishi wa habari kuitumia ipasavyo ofisi yake kupata  taarifa sahihi za kuwasaidia katika uandishi wao. Picha na Aron Msigwa.

  Waandishi wa habari wakiendelea kupata ufafanuzi wa masuala mbalimbali ya uendeshaji wa shughuli za  Bunge kutoka kwa Katibu wa Bunge Dkt. Thomas Kashilila leo jijini Dar es salaam. Pamoja na mambo mengine amesema ofisi yake itaendelea kushirikiana na vyombo vya habari katika utoaji wa taarifa mbalimbali za bunge pamoja na uandaaji wa mafunzo ya mara kwa mara kwa waandishi wanaoandika habari za bunge.

No comments:

Post a Comment