Thursday 14 February 2013

WAZIRI MKUU MIZENGO PINDA NA MKURUGENZI MKUU WA SHIRIKA LA NGUVU ZA ATOMIKI DUNIANI (IAEA) YUKIYA AMANO WAZINDUA JENGO JIPYA LENYE VIFAA VYA KISASA KUSHUGHULIKIA MAGONJWA YA KANSA NCHINI .

Waziri Mkuu Mh. Mizengo Pinda akiongea na waandishi wa habari (hawapo pichani)  jijini Dar es salaam mara baada ya kuzindua jengo jipya la Taasisi ya Kansa Ocean Road lililojengwa na serikali ya Tanzania lenye uwezo wa kuhudumia wa 257 kwa gharama ya shilingi bilioni 7.2 huku Shirika la nguvu za Atomiki Duniani (IAEA) likichangia mashine 2 za kutambua sehemu zilizoathiriwa na ugonjwa wa kansa katika mwili wa binadamu zenye uwezo wa kuhudumia wagonjwa 1600 kila moja kwa mwaka.

 Baadhi ya wataalam wa Taasisi ya Kansa ya Ocean Road  wakiwa ndani ya moja ya chumba cha  jengo jipya lililozinduliwa jijini Dar es salaam chenye moja ya mashine yenye uwezo wa kuwahudumia wagonjwa 1600 kwa mwaka. Mashine hiyo imetolewa na Shirika la Kimataifa la Nguvu za Atomiki (IAEA).

Mkurugenzi mkuu wa Shirika la Kimataifa la nguvu za Atomiki  Duniani Yukiya Amano  akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani)  jijini Dar es salaam mara baada ya kuzinduliwa kwa jengo jipya la Taasisi ya Kansa Ocean Road lililojengwa na serikali ya Tanzania huku  shirika hilo likitoa msaada wa mashine mbili kwa za kutambua athari za ugonjwa wa kansa kwenye mwili wa binadamu.

Waziri mkuu wa Tanzania Mh. Mizengo Pinda (katikati) akiwaonyesha wageni mbalimbali waliohudhuria uzinduzi wa jengo jipya la kuwahudumia wagonjwa wa kansa  katika Hospitali ya Kansa Ocean Road  kitabu cha Mkakati wa taifa wa Kudhibiti na kupambana na Kansa nchini.
Waziri mkuu wa Tanzania Mh. Mizengo Pinda (katikati) akikata utepe kwa kushirikiana na Mkurugenzi mkuu wa Shirika la Kimataifa la nguvu za Atomiki  Duniani Yukiya Amano (wa pili kutoka kushoto) kuashiria uzinduzi rasmi wa  jengo jipya lenye  vifaa vya kisasa kwa ajili ya  kuwahudumia wagonjwa wa kansa katika Taasisi ya Kansa leo Ocean Road jijini Dar es salaam. Wengine ni Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia Prof. Makame Mbarawa (kushoto), Mkurugenzi mkuu wa Taasisi ya Kansa Ocen Road Prof. Twalib Ngoma (wa tatu kutoka kushoto) na Naibu Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii Dr. Seif Rashid.

No comments:

Post a Comment