Friday 15 February 2013

RAIS KIKWETE AONGOZA VIONGOZI WA SERIKALI MAZISHI YA ASKOFU DKT THOMAS LAIZER, AKEMEA VIONGOZI WA DINI WANAOENEZA KAULI ZA CHUKI, MARAIS WASTAAFU NA WENYEWE WAHUDHURIA

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete akitia saini kitabu cha maombolezo ya Askofu Thomas Laizer wa Dayosisi ya Kaskazini Kati, la Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), kwenye Kanisa Kuu la KKKT mjini Arusha kabla ya kutoa heshima zake za mwisho kwa mwili wa Askofu.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete akiifariji familia ya Askofu Thomas Laizer wa Dayosisi ya Kaskazini Kati nyumbani kwa Askofu mara baada ya kutoa heshima zake za mwisho kwa mwili wa marehemu kwenye Kanisa Kuu la KKKT jijini Arusha, Alhamisi, Februari 14, 2013. Picha zote na Fredy Maro wa Ikulu
Na Mwandishi Wetu, Arusha





Alisema watu wengi ndani ya dayosisi  na nje wamenufaika na miradi ambayo imeweza kubuniwa na Marehemu ikiwemo ujenzi wa hoteli, hospitali, kanisa, shule na miradi ya maji vijijini.
“ Marehemu alikuwa mpenda amani na mhubiri mkubwa wa amani na tuige mfano wa kauli zake zilizokuwa na amani na upendo kwa kila mtu,”alisema.
Wakati huo huo Mkurugenzi Mtendaji wa benki ya biashara  ya CRDB Dkt. Charles Kimei amekiri kuwa Kanisa hilo kudaiwa na benki hiyo fedha nyingi ilizokopa kugharamia ujenzi wa hoteli ya Corridor Spring iliyopo jijini Arusha.
Hata hivyo alisema ucheleweshwaji wa ulipaji wa deni hilo umetokana na mtikisiko wa uchumi duniani ambapo wageni ambao ilitegemea kuwalaza wameshidwa kufika.
Aliwataka waumini kuboresha miradi yote iliyoachwa na marehemu ili kumuenzi mawazo yake jitihada alizokuwa akizifanya kwa ajili ya kusaidia jamii ya kanisa lake na nchi kwa ujumla.
Kwa upande wake Kiongozi wa kambi ya upinzani bungeni na mwenyekiti wa Chadema Freeman Mbowe, aliwataka viongozi wa siasa na Serikali kuhubiri unyenyevu ndani ya kanisa na nje.
Alisema viongozi wengi wamekuwa wakihubiri unyenyekevu ndani ya kanisa lakini suala hilo wamelisahau kulifanya nje ya kanisa jambo ambalo ni hatari kwa amani ya nchi.
“ kupitia msiba huu wa mpendwa wetu, ni wakati sasa kwa viongozi wa dini kuwaeleza ukweli viongozi wa Kiserikali pale wanapokosea…hii itasaidia kujirekebisha na kutuacha kuishi kwa hofu,”alisema Mbowe.
Mwenyekiti wa kituo cha demokrasia nchini, James Mbatia aliwataka viongozi wa dini kukaa chini pamoja kujadili amani badala ya kulalamika kuwa amani imekuwa ikitoweka.
Alisema kulalamika sio suluhu ya matatizo yanayolikabili Taifa la Tanzania, lakini kwa kukaa pamoja na suluhu ya kuonyana na kuelimisha mambo mbalimbali yatakayoisaidia nchi kuendeleza amani na utulivu iliyokuwa nayo.
Akitoa salamu za Umoja wa madhehebu ya kikristo nchini (CCT), Askofu Victor Kitula aliitaka Serikali kutolea tamko mauaji ya mchungaji yaliyotokea Geita hivi karibuni kutokana na kile kilichoelezwa kuwa ni vurugu za kujinja.
Alisema kanisa limesikitishwa na kitendo cha Serikali kunyamazia mauaji hayo ambayo wao kikanisa ni makubwa kufuatia aliouawa kuwa ni mchungaji ambae amekuwa akiongoza wakristo jimboni humo.
Ends…


ASKOFU MKUU KKKT TANZANIA, MALASUSA AKIOMBEA KABURI KABLA YA KUSHUSHWA KWA MWILI WA MAREHEMU ASKOFU WA JIMBO LA KKKT DAYOSISI YA KASKAZINI KATI DKT THOMAS LAISER KATIKA MISA ILIYOFANYIKA USHARIKA WA MJINI KATI. MAREHEMU ALIYEFARIKI FEBRUARI 7 MWAKA HUU AMEZIKWA NDANI YA UZIO WA KANISA HILO

RAIS MSTAAFU WA AWAMU YA PILI, ALLI HASSAN MWINYI PAMOJA NA MKEWE WAKIWEKA MASHADA YA MAUA KATIKA KABURA LA ASKOFU DKT LAIZER LEO JIJINI ARUSHA

MWENYEKITI WA KITUO CHA DEMOKRASIA JAMES MBATIA AKIWEKA SHADA LA MAUA

HILI NDILO KABURI ALIMOZIKWA ASKOFU DKT LAIZER LINAVYOONEKANA BAADA YA ZOEZI LA KUWEKA MASHADA KUMALIZIKA

WAUMINI WAKIENDELEA KUPIGA PICHA MBELE YA KABURA ALIMOZIKWA ASKOFU LAZER NA WENGINE WAKISHANGAA
RAIS MSTAAFU BENJAMIN MKAPA WA KWANZA, MAMA ANNA MKAPA, REGINA LOWASA, NA WAZIRI MKUU MSTAAFU EDWARD LOWASA WAKIFUATILIA KWA KARIBU MISA YA MAZISHI YA ASKOFU LAIZER

ASKOFU MKUU KANISA LA ANGLIKANA NCHINI MOKIWA NA YEYE ALIKUWEPO

ASKOFU MALASUSA AKISOMA MATANGAZO MBALIMBALI WAKATI WA MISA HIYO

MKURUGENZI WA MAKAMPUNI YA IPP, REGINALD MENGI NA YEYE ALIKUWEPO, AMBAPO HATA HIVYO ALISHINDWA KUZUIA HISIA ZAKE NA KUTOKWA MACHOZI KATIKA MAZISHI HAYO

MBUNGE WA SIMANJIRO, CHRISTOPHER OLE SENDEKA NA YEYE PIA ALIKUWEPO

MBUNGE DEOGRATIUS FILIKUNJOMBE AKIFUATILIA MISA YA MAZISHI YA ASKOFU LAIZER KWA MAKINI

NDEWARIO ISSANGYA MTUMISHI WA KANISA LA INTERNATIONAL EVANGELISM AKIFUATILIA MISA YA MAZISHI

KABURI LA ALIMOZIKWA ASKOFU LAIZER

KIONGOZI WA KAMBI YA UPINZANI BUNGENI MWENYEKITI WA CHADEMA NA MBUNGE WA JIMBO LA HAI MKOANI KILIMANJARO, FREEMAN MBOWE AKIWAPA MIKONO YA POLE FAMILI YA MAREHEMU ASKOFU LAIZER MARA BAADA YA KUTOA SALAMU ZAKE, NYUMA YAKE NI MBUNGE WA ARUSHA MJINI GODBLESS LEMA ALIYESEMA MAREHEMU KABLA YA KIFO CHAKE ALIMSISITIZA KUSIMAMIA HAKI ZA WANACHI WA JIMBO LA ARUSHA NA TANZANIA KWA UJUMLA

No comments:

Post a Comment