Tuesday 12 February 2013

TANZANIA KINARA VIVUTIO VYA MAAJABU SABA YA ASILI AFRIKA, YAINGIZA MLIMA KIILMANJARO, SERENGETI NA NGORONGORO

Wadau kutoka TTB ambao pia walikuwa ni miongoni mwa wanakamati ya maandalizi wakiwa katika picha ya pamoja

Vikundi wa ngoma kutoka makabila ya mkoa wa Arusha vilipamba hafla hiyo kamavinavyoonekana.

Mkurugenzi wa Bodi ya Utalii TTB Dk. Aloyce Nzuki akisalimiana na Mbunge wa Jimbo la Iringa mjini Mchungaji Msigwa, Kushoto ni Mh Shah kutoka Mafia na mmoja wa wajumbe wa bodi ya Utalii TTB

Mbunge wa Geita na Mwenyekiti wa kamati ya Utalii, maliasili na mazingira James Lembeli akisalimiana na Bw. Mike Teylor, mfanyabiashara maarufu wa utalii nchini walipokutana katika hafla hiyo.

Mwanamuziki Mrisho Mpoto na Kundi lake wakitumbuiza wakati wa utoaji wa tuzo hizo.

Viongozi mbalimbali wa dini walihudhuria pia.

Kikundi cha ngoma kikitumbuiza katika hafla hiyo.

Waziri wa Maliasili na Utalii Balozi Khamis Kagasheki akizungumza na Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Bibi Maimuna Tarishi katikati ni msaidizi wake Bw. Miskanji.

Waziri wa Maliasili na Utalii Balozi Khamis Kagasheki akizungumza jambo na Mkurugenzi wa Bodi ya Utalii Tanzania (TTB) Dk. Aloyce Nzuki.

Mama Tunu Pinda wa pili kutoka kushoto akiwa katika hafla hiyo, kulia ni Mkurugenzi wa Bodi ya Utalii Tanzania (TTB) Dk Aloyce Nzuki na katikati ni Lynn Imler kutoka Seven Natural Wonders.

Waziri Mkuu akiwa meza kuu pamoja na viongozi wengine wakati wa utoaji wa tuzo hizo za Seven Natural Wonders jijini Arusha jana jioni., kutoka kulia ni Magesa Mulongo mkuu wa Mkoa wa Arusha, Agness Agunyu Waziri wa Utalii kutoka nchini Uganda na kutoka kushoto ni Bw. Philip Imler kutoka Taasisi ya Seven Natural Wonders na Waziri wa Maliasili na Utalii Balozi Khamis Kagasheki.

Mkurugenzi wa TANAPA  Allan Kijazi kushoto akiwa na wadau wengine katika hafla hiyo.

Mabalozi mbalimbali waliohudhuria katika hafla hiyo wa kwanza kutoka kulia ni Balozi Mutinda Mutiso Balozi wa Kenya Nchini Tanzania.

Mkurugenzi wa Bodi ya Utalii nchini Tanzania (TTB)  Dk. Aloyce Nzuki akiongea katika hafla hiyo.

Mwanzilishi na muandaaji wa shindano la Seven Naturaral Wonders Bw.Phillip Imler akizungumza katika hafla hiyo.

Waziri Mkuu Mizengo Pinda akizungumza katika hafla hiyo iliyofanyika jana kwenye hoteli ya Mount Meru jijini Arusha.

Tuzo ya mlima Kilimanjaro ikapokelewa na mhifadhi wa mlima huo kulia ni Waziri Mkuu Mizengo Pinda na Philip Imler kushoto.

Waziri Mkuu Mizengo Pinda akimkabidhi zawadi ya picha ya Ngorongoro Crates  muanzilishi na muandaaji wa shindano la Seven Naturaral Wonders Bw.Phillip Imler mara baada ya kumalizika kwa hafla ya kutangaza maajabu saba ya asili ya Afrika iliyofanyika jana jioni kwenye Hoteli ya Mount Meru jijini Arusha.

Balozi wa Kenya nchini Tanzania akizungumza na Balozi Charles Sanga Mwenyekiti wa Bodi ya Utalii nchini Tanzania TTB na Mkurugenzi wa bodi hiyo Dk. Aloyce Nzuki wakati wa hafla hiyo.

No comments:

Post a Comment