Monday 7 January 2013

CHIKU ABWAO ATANGAZA KUWANI UBUNGE KWA LUKUVI, NI JIMBO LA ISIMANI

MBUNGE wa Viti Maalumu Mkoa wa Iringa, Chiku Abwao (Chadema) ametangaza rasmi kuwania ubunge jimbo la Isimani, wilayani Iringa.

Mwana Mama huyo mahiri katika siasa za vyama vingi, alitangaza azma yake hiyo hivi karibuni wakati chama chake kikinadi sera zake, mjini Iringa katika mkutano uliohudhuriwa na Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu.

Akishangiliwa na umati mkubwa uliohudhuria mkutano huo uliofanyika katika uwanja wa Mwembetogwa mjini Iringa, Abwao alisema "Nia ninayo, nguvu ninayo na uwezo ninao."

Alisema William Lukuvi amekuwa mbunge wa jimbo hilo kwa zaidi ya miaka kumi na tano, jambo linaloongeza kero kwa wananchi.

"Kwanini awe mbunge wa maisha wakati kero za wananchi katika jimbo hilo katika sekta mbalimbali zikiwemo za maji, kilimo, afya zinazidi kuongezeka?" alisema.

Alisema Lukuvi ambaye pia ni Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera) anatakiwa kupumzika kwa kuliachia jimbo hilo mikononi mwa Chadema inayozidi kujiimarisha.

Kutagazwa kwa azma hiyo kumefuta ile min'ong'ono iliyokuwepo mjini hapa kwamba Mbunge huyo wa Viti Maalumu anajipanga kuwania Jimbo la Iringa Mjini ambalo kwasasa linaongozwa na mwanaChadema mwenzake, Mchungaji Peter Msigwa.

No comments:

Post a Comment