Friday 18 January 2013

JK amteua Prof. Msambichaka Mwenyekiti Bodi Bandari, *Severine Kaombwe kuongoza TRL

 

JK amteua Prof. Msambichaka Mwenyekiti Bodi Bandari,
*Severine Kaombwe kuongoza TRL

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania , Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete, amefanya uteuzi wa Wenyeviti wapya wa Mamlamka ya Bandari Tanzania (TPA) na Kampuni ya Reli Tanzania (TRL) .

Katika uteuzi huo Rais Kikwete amemteua Prof. Joseph Msambichaka kuwa Mwenyekiti wa TPA na kutengua uteuzi wa Bwana Raphael Mollel, ambaye alikua anashikilia wadhifa huo. Prof. Msambichaka ni Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Mbeya.

Rais Vilevile amemteua Bwana Severine M.A Kaombwe, kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya TRL. Bwana Kaombwe ni Mtaalam wa Usafirishaji (East Africa Corridor Diagnostic Study for Northern and Central Corridors).

Kulingana na Kaimu Katibu Mkuu Kiongozi Bw. Peniel Lyimo, uteuzi huu unaanza tarehe 16 Januari, 2013.

Imetolewa na:
Premi Kibanga,
Mwandishi wa Habari wa Rais, Msaidizi,
Ikulu
Dar-Es-Salaam

18 Januari, 2013

No comments:

Post a Comment