Tuesday 22 January 2013

Makamu wa Rais Dkt. Bilal ahudhuria maziko ya Makamu wa Rais wa Zimbabwe

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal kushoto akizungumza na Rais Robert Mugabe wa Zimbabwe alipomtembelea  Ikulu ya Harare  jana  kwa lengo la  kumfariji kutokana na kifo cha
Makamu wa Rais wa nchi hiyo Marehemu  Dkt.  Landa John Nkoma kilichotokea mwanzoni mwa wiki iliyopita na kuzikwa jana katika Makaburi ya Mashujaa jijini Harare. Katikati  ni Balozi wa Tanzania nchini Zimbabwe  Adadi Rajabu.


Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiweka shada la maua kwenye kaburi la Makamu wa Rais wa Zimbabwe Marehemu Dkt. Landa John Nkomo wakati wa mazishi yake yaliyofanyika jana  kwenye Makaburi ya Mashujaa jijini Harare. (Picha na OMR)

No comments:

Post a Comment