Tuesday 30 October 2012

JK KUZINDUA CHUO KIKUU CHA MANDELA IJUMAA WIKI HII



RAIS  Jakaya  Kikwete  anatarajiwa kuzindua chuo kikuu cha Sayansi na  na teknolojia cha Nelson Mandela jijini Arusha utakaofanyiaka Novemba 2 mwaka huu.

Uzinduzi huo unatokana na kukamilika kwa ukarabati na uboreshaji wa majengo ya chuo umekamilika kwa asilimia 90 na kugharimu kiasi cha shilingi bilioni 90.

Aidha uzinduzi huo utaambatana na harambee ya kuchangia uzinduzi wa mfuko wa  dhamana  wa chuo hicho utakaofanikisha chuo hicho kujiendesha chenyewe na kwamba viongozi mbalimbali waserikali watahudhulia akiwemo makamu wa Rais Dk.Ghalib Bilal.


Akizungumza na waandishi wa habari chuoni hapo, makamu mkuu wa chuo hicho,Profesa Burton Mwamila alisema kuwa taratibu za uzinduzi huo zimekamilika kwa asilimia 100 huku wageni mashuhuri duniani wakitarajiwa kuhudhulia katika sherehe hizo .

Alisema chuo cha Nelson Mandela kilianzishwa na serikali baada ya kuasisiwa na rais mstaafu wa Afriaka kusini,Mzee Nelson Mandela ambaye hataweza kuhudhulia kutokana na matatizo ya kiafya, kwa lengo la kutoa mafunzo na kufanya utafiti katika maeneo mbalimbali ya fani ya sayansi,uhandisi na teknolojia na tayari kimeanza kupokea wanafunzi kutoka ndani na nje ya nchi.

Alisema ukarabati na uboreshaji wa majengo yaliyokuwa yakimilikiwa na CAMATEC  ulianza Agosti  10 mwaka 2010 na ilipofika oktoba 2011 chuo hicho kilidahili kundi la kwanza la wanafunzi wapatao 83,kati yao 30 wakichukua masomo ya uzanivu na 53 ya uzamili.

Aidha aliongeza kuwa chuo hicho kwa sasa kina jumla ya wanafunzi 217 na kwamba katika mwaka huu wa masomo ,chuo kimedahili wanafunzi 135 wa kundi la pili ,huku kati yao 46 wakichukua masomo ya uzanivu na 89 wakichukua masomo ya uzamili.

Akizungumzia hali ya ubora wa elimu unaotolewa katika chuo hicho alisema kuwa chuo kinawataalamu mbalimbali kutoka vyuo mbalimbali hapa duniani na kwamba kimekuwa kikishirikiana kwa ukaribu na vyuo mbalimbali vilivyoko katika nchi 10 duniani.

‘’tumeanzisha ushirikiano wa kitaaluma na vyuo vikuu mbalimbali hapa duniani, ambapo kwa kuanzia tunashirikiana na nchi za Marekani ,Uingereza,Sweden,Itary ,Urusi ,Korea Kusini,India,Ubeligiji na Swazland’’alisema Prof Mwamilwa.

Alisema makubaliano na vyuo hivyo ni kushirikiana katika kufundisha ambapo walimu waliopo kwenye vyuo hivyo wakuwa wakija kufundisha huku pia walimu waliopo chuoni hapo wakipata fursa ya kujifunza katika vyuo hivyo na kwamba walimu ambao hawatafika watakuwa wakiitoa elimu kwa njia ya mtandao.

Alisisitiza kuwa kwa sasa chuo hicho kina jumla ya maprofesa 16 wenye upeo mkubwa wa kufundisha masomo mbalimbali kutoka nchi mbalimbali ikiwemo Rwanda na Burundi ambao wameajiriwa kwa ajili ya kufundisha na kutoa elimu iliyobora inayokubalika kimataifa.

Aidha alisisitiza kuwa uzinduzi huo utatanguliwa na maonyesho mbalimbali ya elimu, burudani kutoka vikundi mbalimbali vya wasanii ,uwekaji wa jiwe la msingi utakaofanywa na Rais Kikwete,pamoja na kutembelea majengo ya chuo.

Mwisho.

No comments:

Post a Comment