Saturday 27 October 2012

SIMANZI ARUMERU

Mmoja wa wakazi wa singisi akiwa nje ya nyumba yake pamoja na watoto wake akitafakari namna ya kushi baada ya nyumba yake kubomolewa juzi usiku.
FAMILIA tano katika kata ya Sing”isi wilayani Arumeru Mashariki mkoani Arusha juzi zililazimika kulala nje kufuatia nyumba zao kubomolewa kwa kile kinachoelezwa kuwa ni amri ya wawekezaji raia wa kigeni.

Unyama huo ambao unadaiwa kufanywa na wawekezaji hao ambao ni wamiliki wa mashamba makubwa wilayani humo taarifa zaidi zinasema  Wananchi hao wametendewa unyama huo baada ya viongozi wa kata na kijiji kuhongwa.

Hatahivo,familia hizo zenye wakazi        zaidi ya 30 zinazoelezwa kuishi karibu na mashamba hayo maarufu kama mito miwili,  zimeiangukia serikali na kuitaka iingilie kati sakata hilo kwa madai kwamba wanateseka kwa kuishi na hofu ,kukosa chakula sanjari na watoto wao kutohudhuria masomo mashuleni.

Tukio hilo wakazi hao ambalo lilitokea  saa 6.30 usiku wa kuamkia Oktoba 26 imeelezwa kuwa wakiwa wamelala madalali wa wawekezaji wa kigeni wanaomiliki mashamba makubwa walivamia katika makazi yao na kisha kuwatoa nje kabla kabla ya kuanza kubomoa nyumba zao.

Wakizungumza na waandishi wa habari waliotembelea eneo hilo juzi wakazi hao walisema kwamba watu hao mara baada ya kuwatoa nje waliwakusanya na kisha kuwafungia katika chumba kimoja na kisha kuanza kubomoa nyumba zao.

Fataeli Macha na mkewe Helen Macha ni miongoni mwa wahanga wa tukio hilo ambao kwa pamoja wanasema wao ni wakazi halali wa maeneo hayo tangu miaka ya sitini baada ya kupata maeneo hayo kutoka kwa wazazi wao.

Wanasema mbali ya kubomolewa nyumba zao pia waliofanya zoezi hilo waliwapora mali mbalimbali  kama simu,radio,fedha kisha kutokomea kusikojulikana.

Kwa nyakati tofauti wakazi hao walisema kwamba watu hao kabla ya kuanza kubomoa nyumba zao waliwakuwa wakiwatamkia maneno ya kwamba kwanini wamekataa kulipwa fidia ili waondoke katika makazi hayo na kisha wwaachie wawekezaji.

“Walikuwa wanatuambia ya kwamba kwanini tumekataa kulipwa fidia ili tuhame katika makazi haya na tuwaachie wawekezaji”walisema kwa nyakati tofauti

Kwa upande wake Rehema Mohamed na Amina Idd walisema kwamba watu hao walikuwa wamevalia kofia na makoti meusi ambapo baadhi yao walipigwa na vitu vizito kabla ya zoezi la kubomolewa nyumba zao.

Kwa pamoja walimtaja mtu mmoja aliyetambulika kwa jina la Kileo kwamba ndiye dalali wa wawekezaji wa kigeni wanaomiliki mashamba makubwa yaliyopo karibu na makazi yao kwamba amekuwa akiwashawishi wao kupokea fedha za fidia ili wapishe lakini wamekataa.

katika picha mmoja wa wakazi wa singisi akionekana mwenye huzuni mara baada ya nyumba yake kubomolewa kwa kile kinachoelezwa kuwa ni amri ya wawekezaji.

No comments:

Post a Comment