Monday 5 November 2012

KAULI YA MNYIKA NA WAZIRI MKUU BUNGENI DODOMA JANA NOV5/2012

Mbunge wa Ubungo John Mnyika akimwomba Spika Anne Makinda kuilazimisha Serikali kutolea kauli tatizo la uhaba wa mafuta nchini jana bungeni mjini Dodoma .

Waziri Mkuu Mizengo Pinda akijibu hoja ya Mbunge wa Ubungo John Mnyika kuhusu kauli ambayo Serikali itatoa hivi karibuni juu ya mkakati wa kukabiliana na uhaba wa mafuta nchini

KUTOKA DODOMA.

Mbunge wa Ubungo (CHADEMA) John Mnyika akihoji kiti cha spika juu ya serikali kushindwa kuleta bungeni kauli ya serikali juu ya mkakati wa serikali kukabiliana na uhaba wa mafuta nchini Tanzania.
 
Uhaba wa mafuta leo umewakimbiza kwenye kikao cha bunge mjini Dodoma asubuhi, Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo na naibu mawaziri wake George Simbachawene na Steven Masele.
 
Waziri huyo na naibu mawaziri wake hawakuwepo bungeni leo wakati Mbunge wa Ubungo (CHADEMA) John Mnyika alitaka serikali itoe sababu ya kutokuja bungeni leo kutoa tamko la serikali ya jinsi inavyoshughulikia swala la uhaba wa mafuta nchini.
 
Spika wa Bunge Anne Makinda alimlazimisha Waziri kuu Mizengo Pinda kusimama na kujibu hoja ya Mnyika aliyemtaka Spika kulazimisha serikali ijibu hoja  yake pamoja na mkakati wa serikali wa kutatua uhaba wa mafuta nchini.
 
Waziri Mkuu  Mizengo Pinda alilazimika kunyanyuka nakusema kwa ufupi kuwa serikali ilikuwa ikijiandaa na kuja na hoja nzito ya kueleza umma mikakati kabambe ya kutatua uhaba wa mafuta nchini.

No comments:

Post a Comment