Wednesday 28 November 2012

LOWASA AENDESHA HARAMBEE YA UJENZI WA MABWENI YA WASICHANA- CHUO KIKUU CHA TEOFIL KISANJI MBEYA

 



Add caption


Waziri Mkuu mstaafu na Mbunge wa Jimbo la Monduli,Mh. Edward Lowassa akiendesha harambe ya kuchangia ujenzi wa bweni la wanafunzi wa kike katika Chuo Kikuu cha Teofilo Kisanji, kinachomilikiwa na Kanisa la Moravian nchini Tanzania,Jimbo la Kusini Magharibi,usharika wa Ruanda mjini Mbeya.Kulia ni Mkuu wa Wilaya ya Rungwe,Mh. Cripin Meela
WAZIRI Mkuu Mstaafu Edward Lowassa amewataka vijana nchini kusoma kwa bidii ili kutoa ushindani katika soko la jira la Afrika Mashariki (EAC).
Lowassa aliyasema hayo jana jijini Mbeya alipoongoza harambee ya kuchangisha fedha za ujenzi wa mabweni ya Wasichana Chuo Kikuu cha Teofilo Kisanji kinachomilikiwa na Kanisa la Moravani Tanzania.
Katika harambee hiyo Lowassa, familia na marafiki zake walichangia fedha taslimu Sh. Milioni 20, ahadi Sh. Milioni 5 na kufanya jumla alizochangia kuwa Sh. Milioni 25.
Akizungumza katika harambee hiyo alisema, unyonge wa wasichana wa kike mashuleni hauwezi kuondolewa kwa kelele za kisiasa hata siku moja.
“Unyonge wao hauwezi kuondoka kwa kelele za kiasiasa tu, bali ukombozi wao kwa sehemu kubwa upo mikononi mwao kwa maana ya elimu,” alisema Lowassa.
Alisema hivi sasa taifa la Tanzania limekuwa na idadi kubwa ya vijana ambao kwa namna yoyote wanapaswa kuandaliwa vizuri.
“Katika taifa letu vijana ndio wengi zaidi hivyo ni muhimu tuwaandae vizuri endapo tunataka kuwa na taifa madubuti,” alisema Lowassa na kuongeza:
“Mwalimu Nyerere alitufundisha; kupanga ni kuchagua.
Hivyo natoa mwito kwa wasichana mjiepushe na viwashiwi na msome kwa bidii,”alisema.
Akifafanua kuhusu umuhimu wa ujenzi wa Hosteli za wasichana mashuleni na vyuoni unatokana na wasichana wengi kukabiliwa na mazingira magumu yanayotishia mustakabli wa maisha yao.
Alisema kwa sasa Jumuiya ya Afrika Mashariki tayari imefungua mipaka yake ya ajira huria hivyo kama vijana nchini wataendelea kukosa elimu basi ushindani katika soko hilo utakuwa mgumu.
“Ndugu zangu nawaomba tuunganishe nguvu tuwasaidie vijana wetu, naamini tukitoa Mungu hata acha kutubariki na atabariki kazi zetu kuongeza riziki zetu.
“Rafiki zangu wadai mimi ni tajiri nina fedha nyingi, si kweli ninafanya jambo hili kwa kushirikisha rafiki, ndugu na jamaa zangu tangu nianze kutoa sijafirisika,” alisema Lowassa.
Awali Askofu Kiongozi wa Kanisa la Moravian Tanzania Alinikisa Cheyo akizungumza katika harambee hiyo alisema, kukamilika kwa mabweni hayo kutasaidia wasichana 348 kukaa sehemu moja kwenye vyumba 87.
“Tumejipanga kukusanya Sh.Milioni 235 katika harambee hii,” alisema Askofu Kiongozi Cheyo.
Naye Mkuu wa wilaya ya Rugwe Chrispn Meela akizungumza kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Abass Kandoro alisema, serikali itaendelea kuwa karibu katika kuhakikisha mabweni hayo yanakamilika.
“Serikali inaendelea kuunga mkono juhudi hizi kwani ni lazima tuwekeze katika elimu na kwa kutambua hilo tunatoa Sh. Milioni Moja,” alisema Meela.



No comments:

Post a Comment