Wednesday 28 November 2012

TAASISI ZA FEDHA ZAPEWA CHANGAMOTO NA JK

RAIS Jakaya Kikwete amezitaka taasisi za fedha nchini kuondoa vikwazo mbalimbali wakati wa ujazaji wa fomu kwa ajili ya kufungua akaunti kwanye mabenki kwani kwakufanya hivyo wananchi wanaweza kukaa na fedha majumbani badala ya kuzipeleka kwenye benki.
Aidha amezisihi benki kutoa mikopo zaidi kwa wananchi hususan wakulima pamoja na wafugaji ili kuwa na ongezeko kubwa la wananchi wanaojiajiri wenyewe na kupata vipato kutokana na mikopo ya bei nafuu.
Kikwete aliyasema hayo jana wakati akifungua mkutano wa 16 wa Taasisi za Fedha unaofanyika Jijini Arusha.
Alisema vikwazo ni vingi katika ufunguaji wa akaunti hali inayopelekea wananchi kushindwa kufungua akaunti na kukaa na fedha majumbani mwao na wengine kuzichimbia chini ya ardhi kwaajili ya usalama kutokana na hatua mbalimbali za ujazaji wa fomu.
“Acheni urasimu ukitaka kufungua akaunti mlolongo ni mkubwa sana mpaka unamchosha mwananchi anayetaka kufungua akaunti angalie utaratibu mwingine juu ya ufunguaji wa akaunti mkiendelea hivyo mitakosa wateja pia huduma ya utoaji wa fedha kwakutumia simu inakuwa kwa kasi kwasababu haina mlolongo mrefu kama wa mabenki”.
Alisisitiza kuwa taasisi za kibenki kuhakikisha zinatoa mikopo nafuu kwa wakulima na wafugaji ili kuwawezesha wananchi kunufaika na kilimo zaidi kwani maendeleo ya kila nchi yanatokana na kilimo cha kisasa zaidi.
Alisema hivi sasa kasi ya utumaji wa fedha kwakutumia simu za mkononi imeongezeka zaidi na wateja wengi wanaipenda njia hiyo kwasababu ni salama na haina mlolongo mrefu wa utumaji wa fedha kama vile kwenye mabenki.
Naye Gavana wa Benki Kuu (BoT), Profesa Benno Ndulu alisema Benki hiyo imezindua mfuko wa wadhamini wa Mwalimu Julius Nyerere ambao utawezesha wanafunzi wa kike na wa kiume kupata ufadhili wa masomo ya sayansi na hesabu
Akizindua mfuko huo wa wadhamini ,Rais Kikwete aliipongeza benki hiyo ,taasisi za fedha pamoja na magava wastaafu na wafanyakazi wa benki kuu kwa moyo waliouonyesha juu ya kuendeleza elimu ambayo hayati Mwali Nyerere ambaye ni baba wa Taifa alihamasisha sana elimu kwa vijana ambayo inaleta maendeleo.
Mkutano huo pia ulihudhuriwa na Mama Maria Nyerere, Gavana Mstaafu, Edward Mtei pamoja na wadau mbalimbali wa taasisi za fedha ndani na nje ya nchi.


No comments:

Post a Comment