Tuesday 4 December 2012

TIMU YA BUNGE ZIARANI NAIROBI NCHINI KENYA

Add caption

Kikosi kamili cha Bunge FC kina matarajio ya kufanya vizuri kutokana na maandalizi makubwa waliyoyafanya kwa kuweka kambi ya wiki tatu mkoani Arusha na kucheza mechi nne za kirafiki za majaribio bila kupoteza hata mchezo mmpja
Katika mechi ya kwanza Bunge FC ilicheza na East Africa Community na kutoka sare ya o-o kisha kuilaza TASWA FC tawi la Arusha 2-1,na kufuatiwa na mchezo dhidi ya chuo cha uandishi wa habari Arusha AJTC na kulazimishwa sare ya 2-2 na mchezo wa mwisho iliilaza Sunrise Radio 3-0
Nahodha wa BUNGE FC Idd azan amesema mazoezi waliyoyafanya pamoja na mechi za kujipima uwezo walizocheza zimewaweka fiti kwa ajili ya kufanya vizuri na kurejea na ubingwa walioupoteza mwaka jana huko Kampala nchini Uganda
Azan ameongeza kuwa wachezaji wote wapo fiti isipokuwa yeye aliyeumia katika mchezo dhidi ya TASWA lakini anaendelea vizuri na anategemea hadi kuanza kwa mashindano hayo atakuwa amepona kabisa kukaa langoni kutetea taifa lake
‘niliumia nyonga katika mechi dhidi ya TASWA lakini nashukuru mungu naendelea vizuri na nimeanza mazoezi mepesi nikitumaini kuwa fiti kabla ya kuanza kwa mashinda’alisima idd azani na kuongeza kuwa ndio maana katika mchezo dhidi ya nrise alicheza kipindi kimoja tu na kupumzika.
 habari hii imeandikwa na woindeshizza,Arusha
Mashindano hayo yataanza kutimua vumbi jijini Nairobi mwishoni mwa wiki hii kwa kushirikisha timu sita za mabunge ya Tanzania,Uganda,Rwanda,Burundi,bunge la afrika mashariki na wenyeji Kenya ambapo timu zimepangwa katika makundi mawili yatakayokuwa na timu tatu na timu mbili zitaingia nusu fainali na washindi kuingia fainali itakayopigwa desemba 16
Baadhi ya wachezaji wanaounda bunge fc ni pamoja na idd azan,wiliam ngeleja,Joshua nasari,godfrey zambi,abdall seleman,amos makala,dr kigwangala,steve ngonyani’maji marefu’ huku ikimkosa kiungo mchezeshaji Juma  nkamia aliye masomoni
Bunge fc wako chini ya benchi la ufundi linaloongozwa na makocha Kasimu Majaliwa na Abdul Mtekete

No comments:

Post a Comment