Na Nathaniel Limu.
Halmashauri
ya wilaya ya Singida imesema haitakubali kuchonganishwa na wananchi
wake na vyombo au taasisi yakiwemo mashirika yasiyo ya kiserikali
(NGOs), kwa kutoa taarifa zisizofanyiwa utafiti wa kina.
Kaimu
Mkurugenzi Mtendaji wa halmashauri hiyo Alli Juma, amesema hayo muda
mfupi kabla ya mkutano wa mrejesho wa ripoti/taarifa ya shirika lisilo
la kiserikali la Sikika lenye makazi yake jijini Dar-es-salaam,
iliyohusu ufuatiliaji wa uwajibikaji katika utoaji wa huduma za afya,
haujafungwa rasmi.
Amesema
taarifa iliyotolewa na shirika la Sikika, kwa kiasi kikubwa
haikufanyiwa utafiti wa kina, kitendo ambacho kinaweza kusababisha
halmashauri kutokuelewana vizuri na wananchi wake.
Alli
ambaye ni Afisa Utumishi amesema Sikika hawakuwa na mawasiliano wala
ushirikiano mzuri na wakuu wa idara katika kupata ukweli wa taarifa
mbalimbali walizokuwa wanazikusanya.
“Mimi
niwaombeni tu ndugu zangu wa Sikika, fanyeni kazi kwa kufuata sheria,
kanuni na taratibu, halafu mkiandika mabaya, upande wa pili andikeni pia
mazuri hata kama yapo machahe”,alisema Alli.
Mkutano
huo uliokuwa chini ya uenyekiti wa diwani (CCM) Elia Digha, Mwenyekiti
huyo alitoa shutuma nzito kwamba wafanyakazi wa Sikika na kamati nzima
iliyofuatilia uwajibikaji wa huduma za afya, haijui lolote.
“Mimi
nasema timu yote iliyoleta taarifa hii, haijui lolote, naomba siku za
usoni tushirikiane vizuri katika kufuatilia uwajibikaji katika sekta
zote, kutoa taarifa za jumla jumla kama hii, mtaacha watu waichukie bure
serikali”, alisema Digha ambaye ni diwani wa kata ya Msange jimbo la
Singida Kaskazini.
Baada
ya maneno hayo mazito, diwani wa viti maalum (CCM) Salima Kundya,
aliyeshiriki na Sikika kufuatilia uwajibikaji katika sekta ya afya,
alimtolea uvivu Mwenyekiti Digha, kuwa lengo lake ni kutaka kuficha
ukweli uliopo kwenye taarifa hiyo.
“Kama
sisi madiwani wawili wa CCM mliotuchagua tukashirikiane na Sikika na
tukabaini yote yaliyopo kwenye taarifa ya Sikika kuwa ni ya ukweli
mtupu, halafu wewe unasema hatujui lo lote, basi wewe mwenyekiti Digha
na madiwani wote wa CCM walioshiriki kutachagua na ninyi wote hamjui
kitu au cho chote kinachofanyika ndani ya halmashauri hii”, alisema
Salima huku uso wake ukionyesha kujawa na hasira.
Baada
ya maneno hayo ya diwani Salima, bila kulazimishwa, Digha ambaye pia ni
msaidizi wa mbunge wa jimbo la Singida kaskazini Lazaro Nyalandu,
alisimama na kuomba radhi kwa matamshi yake ambayo yalilenga
kuidhalilisha kamati iliyoambatana na Sikika.
Katika
mengi yaliyomo kwenye taarifa ya Sikika, kuna hoja iliyotolewa na
mkaguzi mkuu wa hesabu za serikali, inaonyesha kuwa halmashauri hiyo
ilikuwa na shilingi bilioni 1,686,561,960 za miradi mbalimbali ya
maendeleo.
Lakini
taarifa hiyo, ilionyesha kiasi cha shilingi bilioni 1.6 sawa na aslimia
61.4,hazikutumika kwa wakati, kitendo hicho kinamaanisha kuwa baadhi ya
miradi ya maendeleo, ilikamilika nusu ama haijakamilika kabisa.
No comments:
Post a Comment