Add caption |
Kikosi
kamili cha Bunge FC kina matarajio ya kufanya vizuri kutokana na
maandalizi makubwa waliyoyafanya kwa kuweka kambi ya wiki tatu mkoani
Arusha na kucheza mechi nne za kirafiki za majaribio bila kupoteza hata
mchezo mmpja
Katika
mechi ya kwanza Bunge FC ilicheza na East Africa Community na kutoka
sare ya o-o kisha kuilaza TASWA FC tawi la Arusha 2-1,na kufuatiwa na
mchezo dhidi ya chuo cha uandishi wa habari Arusha AJTC na kulazimishwa
sare ya 2-2 na mchezo wa mwisho iliilaza Sunrise Radio 3-0
Nahodha
wa BUNGE FC Idd azan amesema mazoezi waliyoyafanya pamoja na mechi za
kujipima uwezo walizocheza zimewaweka fiti kwa ajili ya kufanya vizuri
na kurejea na ubingwa walioupoteza mwaka jana huko Kampala nchini Uganda
Azan
ameongeza kuwa wachezaji wote wapo fiti isipokuwa yeye aliyeumia katika
mchezo dhidi ya TASWA lakini anaendelea vizuri na anategemea hadi
kuanza kwa mashindano hayo atakuwa amepona kabisa kukaa langoni kutetea
taifa lake
‘niliumia
nyonga katika mechi dhidi ya TASWA lakini nashukuru mungu naendelea
vizuri na nimeanza mazoezi mepesi nikitumaini kuwa fiti kabla ya kuanza
kwa mashinda’alisima idd azani na kuongeza kuwa ndio maana katika mchezo
dhidi ya nrise alicheza kipindi kimoja tu na kupumzika.
habari hii imeandikwa na woindeshizza,Arusha
Mashindano
hayo yataanza kutimua vumbi jijini Nairobi mwishoni mwa wiki hii kwa
kushirikisha timu sita za mabunge ya
Tanzania,Uganda,Rwanda,Burundi,bunge la afrika mashariki na wenyeji
Kenya ambapo timu zimepangwa katika makundi mawili yatakayokuwa na timu
tatu na timu mbili zitaingia nusu fainali na washindi kuingia fainali
itakayopigwa desemba 16
Baadhi
ya wachezaji wanaounda bunge fc ni pamoja na idd azan,wiliam
ngeleja,Joshua nasari,godfrey zambi,abdall seleman,amos makala,dr
kigwangala,steve ngonyani’maji marefu’ huku ikimkosa kiungo mchezeshaji
Juma nkamia aliye masomoni
Bunge fc wako chini ya benchi la ufundi linaloongozwa na makocha Kasimu Majaliwa na Abdul Mtekete
No comments:
Post a Comment