Release No. 189
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Desemba 3, 2012
KILIMANJARO STARS KUCHEZA NUSU FAINALI ALHAMISI
Tanzania
Bara (Kilimanjaro Stars) itacheza nusu fainali ya michuano ya Kombe la
Chalenji 2012 Alhamisi (Desemba 6 mwaka huu) kwenye Uwanja wa Mandela
ulioko Namboole jijini Kampala, Uganda.
Kilimanjaro
Stars ambayo itacheza mechi hiyo na mshindi wa robo fainali ya kesho
(Desemba 4 mwaka huu) kati ya wenyeji Uganda na Ethiopia imeingia hatua
hiyo baada ya kuitoa Rwanda. Mechi imechezwa leo (Desemba 3 mwaka huu)
Uwanja wa KCC ulioko Lugogo, Kampala.
Mabao
ya Amri Kiemba dakika ya 33 na John Bocco dakika ya 53 ndiyo
yaliyoifanya Kilimanjaro Stars itinge nusu fainali na kuifungisha virago
Rwanda (Amavubi) inayofundishwa na Milutin ‘Micho’ Sredojovic kutoka
Serbia.
Vijana
wa Kilimanjaro Stars wanaonolewa na Kim Poulsen walitawala pambano
hilo, hasa kipindi cha kwanza kwa pasi fupi fupi. Kilimanjaro Stars
imefungwa bao moja katika mechi nne ilizocheza tangu michuano hiyo
ilipoanza Novemba 24 mwaka huu jijini Kampala.
Kilimanjaro
Stars ambayo katika michuano hiyo iliyofanyika Dar es Salaam mwaka jana
iliishia hatua ya nusu fainali iliwakilishwa na; Juma Kaseja, Erasto
Nyoni, Amir Maftah, Shomari Kapombe, Kelvin Yondani, Amri Kiemba, Salum
Abubakar/Athuman Idd, Frank Domayo, Mwinyi Kazimoto, John Bocco na
Mrisho Ngasa.
MICHUANO YA KOMBE LA UHAI KUANZA DESEMBA 7
Michuano
ya Kombe la Uhai inayoshirikisha timu za U20 za klabu za Ligi Kuu ya
Vodacom inatarajia kuanza Desemba 7 mwaka huu na kumalizika Desemba 22
mwaka huu.
Wachezaji
watakaoshiriki michuano hiyo ni wale tu ambao usajili wao umefanyika
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) na kupata leseni. Hakutakuwa
na usajili mwingine wowote mbali na ule uliofanyika sambamba na wa Ligi
Kuu.
Taratibu zote za michuano hiyo zitafahamishwa kwa klabu husika ikiwemo ratiba ya michuano hiyo.
Boniface Wambura
Ofisa Habari
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF)
Kampala, Uganda
+255 76 7310242
No comments:
Post a Comment