Makamu wa Rais Dkt. Bilal ahudhuria maziko ya Makamu wa Rais wa Zimbabwe
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal
kushoto akizungumza na Rais Robert Mugabe wa Zimbabwe alipomtembelea
Ikulu ya Harare jana kwa lengo la kumfariji kutokana na kifo cha
Makamu wa Rais wa nchi hiyo Marehemu Dkt. Landa John Nkoma
kilichotokea mwanzoni mwa wiki iliyopita na kuzikwa jana katika Makaburi
ya Mashujaa jijini Harare. Katikati ni Balozi wa Tanzania nchini
Zimbabwe Adadi Rajabu.
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal,
akiweka shada la maua kwenye kaburi la Makamu wa Rais wa Zimbabwe
Marehemu Dkt. Landa John Nkomo wakati wa mazishi yake yaliyofanyika jana
kwenye Makaburi ya Mashujaa jijini Harare. (Picha na OMR)
No comments:
Post a Comment