JK amteua Prof. Msambichaka Mwenyekiti Bodi Bandari, *Severine Kaombwe kuongoza TRL
JK amteua Prof. Msambichaka Mwenyekiti Bodi Bandari,
*Severine Kaombwe kuongoza TRL
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania , Mheshimiwa Jakaya Mrisho
Kikwete, amefanya uteuzi wa Wenyeviti wapya wa Mamlamka ya Bandari
Tanzania (TPA) na Kampuni ya Reli Tanzania (TRL) .
Katika uteuzi huo Rais Kikwete amemteua Prof. Joseph Msambichaka kuwa
Mwenyekiti wa TPA na kutengua uteuzi wa Bwana Raphael Mollel, ambaye
alikua anashikilia wadhifa huo. Prof. Msambichaka ni Mhadhiri wa Chuo
Kikuu cha Mbeya.
Rais Vilevile amemteua Bwana Severine M.A
Kaombwe, kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya TRL. Bwana Kaombwe ni Mtaalam wa
Usafirishaji (East Africa Corridor Diagnostic Study for Northern and
Central Corridors).
Kulingana na Kaimu Katibu Mkuu Kiongozi Bw. Peniel Lyimo, uteuzi huu unaanza tarehe 16 Januari, 2013.
Imetolewa na:
Premi Kibanga,
Mwandishi wa Habari wa Rais, Msaidizi,
Ikulu
Dar-Es-Salaam
18 Januari, 2013
No comments:
Post a Comment