Binti Rebbeca Bernardo akiwa nyumbani kwao akimuuguza mama yake aliyepooza mwili. |
Binti Rebecca Bernardo. |
Mwanafunzi
mmoja wa sekondari mkazi wa mji wa Sapeacu nchini Brazil Rebbeca
Bernardo (18) amefikia uamuzi wa kuinadi bikira yake katika mtandao ili
kupata fedha za kugharamia matibabu ya mama yake aliyepooza mwili.
Rebecca
amedai kuwa alijaribu kufanya kazi za kuuza vipodozi na pia kufanya
kazi ya uhudumu lakini kazi zote hizo hazikumpatia kipato cha kumwezesha
kumudu gharama za kumtunza mama yake.
Mwanafunzi
huyo amesema amefikia uamuzi huo baada ya kuvutiwa na jinsi mwanamke
mwingine aliyejulikana kwa jina la Catarina Migliorini mwenye umri wa
miaka 20 ambaye mwishoni mwa mwaka jana aliweza kupata kiasi cha dola
780,000 kwa kuiuza bikira yake kwenye mnada.
Rebecca
amedai kuwa Catarina alipata wadau mbalimbali kutoka kona zote za dunia
ambao walitaka kuivunja bikira yake na yeye pia anatarajia wanaume
wengi watajitokeza.
Katika
mchakato wake huo wa kuinadi bikira yake, Rebecca amedai kuwa jumla ya
wanaume watatu wameshajitokeza na dau kubwa hadi sasa ni dola 35,000.
No comments:
Post a Comment