Monday, 28 January 2013

NGILISHO MIKONONI MWA TAKUKURU

BREAKING NEWS!!!!!!!!!!!!!!!
TAARIFA ZILIZOTUFIKIA HIVI PUNDE, YULE MWANDISHI WA HABARI ANAYETESA SANA WATU HAPA ARUSHA KWA KUTUMIA VIBAYA CHEO HICHO JOSEPH NGILISHO AMEKAMATWA NA TAKUKURU KATIKA HOTELI YA AFRICAN TULIP CORIDOR AREA, (UZUNGUNI) MJINI ARUSHA AKIPOKEA RUSHWA KUTOKA KWA MMOJA WA WAFANYAKAZI WA EAC, KIASI CHA Tsh 500,000 IKIWA NI KIANZIO CHA Tsh 2,000,000/- ALIZOTAKA KUPEWA. ALIPOZIPOKEA NA KUTEREMKA NDANI YA GARI YA KIONGOZI HUYO WA EAC, ALIJARIBU KUKIMBIA LAKINI ALINASWA BAADA YA KUINGIA OFISI ZA USALAMA WA TAIFA KUJIFICHA BILA MAFANIKIO. IMEELEZWA KUWA ALIPOFIKA OFISI HIZO ZA USALAMA WA TAIFA ALIJITAHIDI KUTOA FEDHA HIZO CHAFU KUZITUPA LAKINI HATA HIVYO ILISHINDIKANA. ...


HABARI ZAIDI ZINAELEZA KUWA NGILISHO ALIPOKAMATISHWA FEDHA HIZO NA KUGUNDUA KUWA ULIKUWA NI MTEGO ALIANZA KUKIMBIA AKIWA NA BURUNGUTU LA FEDHA MFUKONI NDIPO MAOFISA WA TAKUKURU  NA WENYEWE WALIPOANZA KUMFUKUZA ILI WAMTIE HATIANI.

INAELEZWA KUWA MBINU YA MAOFISA HAO YA KURUSHA RISASI HEWANI NDIO ILIYOMFANYA NGILISHO KUTAFUTA SEHEMU YA KARIBU YA KUJIFICHA AKIOGOPA KUPIGWA RISASI LAKINI HATA HIVYO ENEO ALILOKIMBILIA KATIKA OFISI ZA USALAMA WA TAIFA HAPAKUWA MAHALI PAZURI KWAKE.

HATIMAYE ALIKAMATWA NA KUPELEKWA MOJA KWA MOJA OFISI ZA TAKUKURU MKOA WA ARUSHA KWA MAHOJIANO ZAIDI KABLA YA KUFIKISHWA KITUO KIKUU CHA POLISI MKOA NA KUWEKWA SERO.

KWA HABARI ZAIDI ENDELEA KUFUATILIA HAPA HAPA

No comments:

Post a Comment