Tuesday, 8 January 2013

VYAKULA VYA GMO MADUKANI KWETU

Ni vizuri pia kuelewa kuwa 'genetic modification" imekuwa ikifanyika kwa
karne nyingi sana. Kwa mfano, kitendo cha mkulima kuchagua mbegu bora toka
ktk mavuno yake kwa ajili ya kupanda msimu unaofuatia ni kwamba anafanya
"genetic selection" ambayo itabadili mazao misimu inayofuatia. Mashabiki wa
GMO wanadai kuwa tofauti ni kwamba, sasa genetic selection inafanyika
kitalaam zaidi na kwa muda mchache kuliko zamani.

Ugomvi upo kwenye laboratory selection and manipulation of genes. Wale
wanaofanya genetic modification wanadai kuwa GMO products hazina madhara
yoyote na anayedai kuwa zina madhara atoe ushahidi wa madai yake. In
English, they have shifted the burden of proof on to the GMO opposers to
prove harmful effects. Wanadai kuwa ni kawaida kwa jamii kuwa na hofu
isiyokuwa na msingi pale teknolojia mpya inapokuja. wanatumia mifano ya
zipu na vifungo, chai na kahawa, margarine na butter, n.k. Kwamba vifungo
vilikuwako kabla ya zipu na kwamba zipu si nzuri kwani zinaweza kufunguka
zenyewe na kumdhalilisha alovaa nguo yenye zipu. Kanisa katoliki likatumika
ktk kupinga ugunduzi na matumizi ya zipu. Mashabiki wa GMO wanasema, je
zipu zimewadhalilisha wavaaji? Vile vile kwamba kahawa ni kinywaji cha
shetani kwa kuwa kahawa ilikuja baada ya chai, vivyo hivyo kwa butter na
margarine, na mengineo mengi. Kwangu mimi ni ya kipuuzi tu.

Mjadala huu unaendelea na bidhaa za GMO zinazidi kuzagaa kwa walaji na
watumiaji. Baadhi ya skimu za kuhakiki kama bidhaa ni za GMO ama la,
zimegundulika kuwa na walakini mkubwa.

Mashabiki wa GMO wanadai kuwa GMO itasaidia kukabiliana na tatizo la njaa
kwa Afrika kwa kuwa zitapatikana mbegu zinazokabili ukame, magonjwa,
wadudu, na kutoa mazao mengi ambazo zinakomaa kwa muda mfupi zaidi.
Terminator seeds ni mfano mmojawapo na baadhi mnatambua athari zake za
kiuchumi, kitamaduni, kijamii n.k. Of particular importance is the
increased dependence on multi-national corporations in industrialized
nations and loss of agro-diversity (I wrote a term paper on this topic for
a class and got marked down because i was against GMO and the professor is
a pro-GMO, it got really hot. He wanted a social-scientist like myself to
prove scientific harmfull effects of GMO, and I argued that psychological
effects among consumers and effects on biodiversity are as important as
health effects that i cannot prove).

Nadhani ni wakati sasa tunahitaji taarifa zote ziwekwe hadharani ili tuweze
kujadili kwa kina.

Baadhi yetu tumejikuta tukishambuliwa sana pale tulipojaribu kuingia kwenye
mijadala dhidi ya GMO foods na kujikuta hatuna ushahidi wa kuthibitisha
madhara yake na kuonekana kana kwamba tuna wasiwasi unaotokana na hisia tu
na sio scientific proof. Nilifarijika nilipofahamu kuwa wafanyakazi wa
kampuni kubwa ya GMO iliyoko Minnesota, USA waligoma kula vyakula
vinavyozalishwa na kampuni yao na kudai wawekewe organic foods kwenye
cafeteria zao

No comments:

Post a Comment