Askofu
wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania Dayosisi ya
Kaskazini.Askofu Thomas Laizer amefariki duniaalasiri ya leo katika
Hospitali ya Rufaa ya Selelian ya Mjini Arusha. Februari 6, 2013 Waziri
Mkuu Mizengo Pinda,
alimtembelea na kumjulia hali Askofu Thomas Laizer wa Kanisa la
Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) Dayosisi ya Kaskazini Kati.
Taarifa
zilipasha kuwa Askofu Laizer alilazwa Hospitalini hapo kwa zaidi ya
mwezi mmoja, na hakuna daktari wala ndugu aliye tayari kusema ugonjwa
unaomsibu.
Pinda
alikwenda hospitalini hapo jana saa 9 alasiri na kukaa zaidi ya nusu
saa, huku waandishi wa habari wakizuiwa kuingia katika chumba alimolazwa
cha wagonjwa wanaohitaji uangalizi maalumu.
Hata
hivyo, baada ya kutoka katika chumba hicho kama ilivyo ada ya viongozi
kuzungumzia hali ya mgonjwa, Pinda hakuzungumza na waandishi wa habari
na kulikuwa na ulinzi mkali ambapo pia waandishi wa habari walizuiwa
kuzungumza naye.
No comments:
Post a Comment