Na Mwandishi Maalum, Arusha
Jeshi
la Polisi mkoani hapa limemkamata mtu mmoja akiwa na magunia 97 ya
madawa ya kulevya aina ya bangi ambayo yalikuwa yanasafirishwa toka
mkoani hapa kuelekea Moshi. Akithibitisha kutokea kwa tukio hilo,
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha Kamishna Msaidizi wa Polisi Liberatus
Sabas amesema.
kwamba, tukio hilo lilitokea muda wa saa 10:00 alfajiri eneo la Usa River wilayani Arumeru.
Alisema
mafanikio hayo yametokana na ushirikiano mzuri kati ya jeshi hilo na
wananchi ambapo taarifa za tukio hilo zilitolewa na raia wema ambapo
askari wa jeshi hilo waliweka mtego eneo hilo na kufanikiwa kulikamata
gari aina ya Fuso lenye namba za usajili T. 282 AAJ.
Kamanda
Sabas aliongeza kwa kusema kwamba, ndani ya bodi ya gari hilo kulikuwa
na mboga aina ya kabeji iliyosambazwa vizuri huku chini ya mboga hiyo
kukiwa na madawa hayo yaliyokuwa kwenye magunia huku yakivingirishwa
kwenye mifuko ya “plastiki” kwa ndani.
Alisema
katika gari hilo kulikuwa na watu watatu na mara baada ya askari hao
kulisimamisha dereva pamoja na msaidizi wake walifanikiwa kukimbia huku
mtu mmoja aliyejulikana kwa jina la Praygod Marick (22) Mkazi wa Dar
esalaam akikamatwa.
Jeshi
la polisi Mkoani hapa linaendelea kumhoji mtuhumiwa huyo huku
watuhumiwa wengine wakiendelea kutafutwa. Kwa mara nyingine tena Kamanda
huyo aliendelea kuwashukuru wananchi wa Mkoa huu kutokana na
ushirikiano wao mkubwa wanaoutoa kwa jeshi hilo na kuendelea
kuwasisitizia kuimarisha mahusiano na jeshi hilo.
Kwa
muda wa kipindi cha mwezi mmoja toka januari 07, 2013 mpaka hivi leo
jeshi hilo limeshakamata madawa ya kulevya aina ya mirungi magunia 372
katika magari mawili tofauti na pia limeshakamata jumla ya magunia 117
ya madawa ya kulevya aina ya bangi ambapo mwanzoni mwa wiki hii jumla ya
magunia 20 yalikamatwa yakiwa yanasafirishwa kwa kutumia wanyama aina
ya Punda maeneo ya Losoiti wilayani Longido.
No comments:
Post a Comment