CHAMA CHA DEMOKRASIA NA MAENDELEO –CHADEMA WILAYA (JIMBO) SINGIDA MJINI
S.L.P 260, SINGIDA. 0784 – 462729 / 0767 – 462729 / 0754 – 818146 / 0754
– 487975 Tarehe 08/02/2013
TAARIFA KWA VYOMBO VYA
HABARI JUU YA MASUALA NA KERO MBALI MBALI ZINAZOWAKABILI WANANCHI WA
SINGIDA MJINI.
Chama cha DEMOKRASIA NA MAENDELEO – CHADEMA wilaya ya
singida Mjini kimeanza kufanya mikutano ya ndani na hadhara kwenye kata
zinazounda wilaya (jimbo) hilo kuanzia tarehe 07/02/2013 na mikutano hii
kwa awamu ya kwanza itahitimishwa tarehe 15/02/2013.
Leo tarehe
07/02/2013 Chadema kimefanya mkutano wa ndani katika kata ya Mtamaa
ambapo mkutano huo ulifanyika pamoja na mambo mengine ulikuwa na lengo
la kuibua kero zinazoikabili kata hiyo na kuangalia namna ya kuzitatua,
kuandaa mkutano wa hadhara unaotarajia kufanyika wiki ijayo, kuimarisha
chama kwenye ngazi ya msingi. Mkutano huo ulihutubiwa na viongozi wa
wilaya akiwemo katibu mwenezi ndugu 1. MUTTA, Anselimi, 2. ANNA MGHWIRA
kiongozi wa bawacha jimbo la Arumeru Mashariki, 3. NIWAEL MRUMA mratibu
wa bawacha mkoa wa Singida,
4. HAMISI MTIPA kamanda wa red briged mkoa
wa Singida, Gideon mhasibu wa tawi la Chadema la uwanja wa ndege
singida. Katika mkutano uliohudhuriwa na wanachama na wafuasi zaidi ya
30, palijitokeza masuala mbali mbali yakiwemo:
1. Kukatika kwa daraja
linalounganisha barabara ya kutoka mjini hadi mtamaa, minyughe na viunga
vyake. Nikishuhudia ubovu wa mawasiliano wa barabara hiyo kutokana na
kukatika daraja hilo kufuatia mvua zinazoendelea kunyesha mkoani
singida,ni wazi wananchi wanapata taabu ya kufika na kutoka mjini hata
gari letu lilikwama kupita pale na kulazimika kupitia kwenye korongo
lililopo pembeni kitendo kilichopelekea gari kuzamisha magurudumu yake
na kushindwa kutoka hadi tulipo pata msaada wa wananchi wasamalia wema.
Sasa wananchi wanhoji kwanini mbunge tunashuhudia akigawa vitenge, kanga
nk kupitia mabalozi na mkuu wa wilaya a viongozi wengine wanaotokana na
CCM?
2. Wananchi wanalalamika kuwa mikutano ya kiserikali inapoitishwa
wananchi wengi hawapati taarifa mapema na wengine hawapati kabisa
kitendo kinachopelekea wananchi washindwe kuwahoji viongozi wao ipasavyo
juu ya masuala mbali mbali kwajili ya ujenzi wa kata na vijiji vyao.
Hivyo wanatoa wito kwa viongozi wote wa serikali akiwemo diwani
kuhakikisha wanatoa taarifa mapema juu ya mikutano hiyo ili wapate muda
kujiandaa kuhudhuria mikutano hiyo.
3. Wanamlalamikia diwani wa kata ya
mtamaa kuwa huwa hakusanyi maoni ya wananchi kabla hajaenda kuhudhuria
vikao vya baraza la madiwani na hata anapokuwa ameenda huko na akirudi
haleti mrejesho kwa wananchi wote. Hivyo wanamtaka ahakikishe anakusanya
kero za wananchi waliomchagua bila kujali vyama vya siasa na itikadi
nyingnezo.
4. Lakini wanahoji kauli ya rais Kikwete ya kusema kuwa
wananchi kujipanga barabarani kusubiria magari yanayopita yakienda
Mwanza au Dar es Salaam wawauzie mafuta yao ya zao lao la ALIZETI ndiyo
masoko. Hivyo wananchi wanataka wawe na soko moja ambalo ni la kuaminika
badala ya kusubiria magari ambayo hayaaminiki. Rais Kikwete alitoa
kauli hiyo kwenye shere za kuapishwa kwa Dr. Alex Mkumbo kuwa askofu
ambapo yeye (rais) alikuwa mgeni rasmi.
5. Lakini pia wanadai kuwa
hawana mbunge bali wanamfadhili wa CCM na ndo maana anapogawa kanga
anagawa zenye rangi ya CCM na anawapa wanaccm na sio wananchi wote.
Ndiyo maana haonekani jimboni ili kutatua kero za wananchi
akiwashirikisha juu ya utatuzi wa masuala mbali mbali na ndoiyo maana
daraja limevunjika bila yeye hadi leo kutafuta ufumbuzi bali alichokiona
kinafaa ni kugawa vitenge vyenye picha yake.
MSIMAMO WA CHAMA JUU YA
MASUALA HAYA
1. Kutokana na hali ngumu ya mawasiliano iliyosababishwa na
kukatika kwa daraja la mtamaa linalounganisha watu wa mtamaa na mjini
litafutiwe ufumbuzi haraka iwezekanavyo kwani likiaachwa na kubaki hivyo
lilivyo sasa hivi, litasababisha maafa makubwa ambayo yanaweza
kugharimu maisha ya wananchi. Tunamtaka mkuu wa Wilaya kutumia mfuko wa
maafa au kama ni mkurugenzi kuitisha kikao cha dharura cha baraza la
madiwani kujadili ni jinsi gani ya kultafutia ufumbuzi daraja hilo na
kama mvua itanyesha leo au kesho, kipande kilichosalia kinashilia
kidaraja hicho kitaondoka.
2. Pia tunamtaka mkuregenzi kutoa hadharani
gharama zilizotumika kujenga daraja hilo na kwanini livunjike mapema
namna hii.
3. Tunamtaka mkaguzi wa ndani wa hesabu za serikali kufanya
uchunguzi juu ya gharama halisi za mradi huo na ubora wa daraja hilo na
ikiwa kutabainika kuna hujuma basi wahusika hata kama watakuwa
wamehamishwa, wakamatwe na kuwekwa ndani na kulipa hasara ambayo
imejitokeza kutokana na wananchi kukosa mawasiliano ya uhakika kutokana
na kuharibika kwa daraja hilo. Ajabu ni pale ambapo ukifika hapo kuna
basi lianalosimama ng’ambo ya upande mmoja ili wakifika hapo wafaulishwe
kwenye gari linalosubiria upande wa pili na kuna vijana wanaokaa pale
wakiwasaidia abiria kama ni mizigo na kudai kulipwa kidogo.
4. Tuna
mtaka mkuu wa TAKUKURU Mkoa wa Singida kutuma makamanda wake kuchunguza
utaratibu mzima uliotumika kumpata mkandarasi wa kujenga daraja hilo,
kiasi cha fedha kilichotumika katika mradi huo na ubora/thamani ya
daraja hilo, je, lilipokabidhiwa lilitakiwa kuishi kwa muda gani wa
matumizi? Na ikibainika kulikuwa na ufisadi basi sheria ichukue mkondo
wake ili kuthibiti vitendo vya kifisadi katika miradi inayojengwa kwa
kodi za wananchi.
5. Tunawataka viongozi wa kata na vijiji wa Kata ya
Mtamaa akiwemo diwani kuhakikisha wanaitisha mikutano na kuwapa taarifa
mbali mbali wananchi na mikutano hiyo ya vijiji na baraza la kata iwe ya
wazi ili kutoa nafasi na fursa kwa wananchi kuhoji masuala mbali mbali
kwa mstakabali wa maendeleo yao.
6. Tunamtaka mbunge wa jimbo la Singida
mjini kujitokeza hadharani na kuwaambia wananchi juu ya matumizi ya
fedha za maendeleo ya mfuko wa jimbo toka ulipoanzishwa rasmi. Tunapata
wasi wasi juu ya fedha wanazonunulia kanga na vitenge na kuwagawia
wanaccm au kuandaa sherehe mbali mbali na kugawa fedha taslimu kama zile
alizowahi kuwagawia walimu wa shule za msingi na sekondari Tzs 50,000/=
kwa kila mwalimu zisijekuwa ndo hizo za mfuko wa jimbo. Haiwezekani
wananchi wachangishwe michango ya elfu 20,000/= eti wanajenga maabara
kwa amri ya rais ili hali haijulikani fedha za mfuko wa jimbo zimefanya
nini.
7. Pia tunawataka madiwani wote wa kata zetu zote hususani kata za
UTEMINI, NA MANDEWA kuwaeleza wananchi ni kwanini barabara za mitaani
kwenye kata wanazoziongoza ni mbovu kupita kiasi? Ni hatua gani
wanachukua kuhakikisha barua zinakuwa katika ubora unaotakiwa?
Vinginevyo tutaandamana kudai haki za wananchi wetu. Haya ndiyo
tunayoyataka kutafutiwa ufumbuzi na mambo mengine tutazidi kuyaweka wazi
kwa kadri tunavyoendelea na mikutano yetu ambapo leo tutakuwa kwenye
kata ya Unyamikumbi kijiji cha Ughaugha. Wito wangu kwa wananchi wa
Singida (jimbo) mjini ni “ KUONDOA UOGA, NA KUDAI HAKI ZAO”
Imetolewa
leo tarehe 08/02/2013 na: MUTTA, Anselimi (Mwl). Katibu mwenezi wa
Wilaya ya Singida Mjini.
No comments:
Post a Comment