Alisema watu
wengi ndani ya dayosisi na nje
wamenufaika na miradi ambayo imeweza kubuniwa na Marehemu ikiwemo ujenzi wa
hoteli, hospitali, kanisa, shule na miradi ya maji vijijini.
“ Marehemu
alikuwa mpenda amani na mhubiri mkubwa wa amani na tuige mfano wa kauli zake
zilizokuwa na amani na upendo kwa kila mtu,”alisema.
Wakati huo
huo Mkurugenzi Mtendaji wa benki ya biashara
ya CRDB Dkt. Charles Kimei amekiri kuwa Kanisa hilo kudaiwa na benki
hiyo fedha nyingi ilizokopa kugharamia ujenzi wa hoteli ya Corridor Spring
iliyopo jijini Arusha.
Hata hivyo
alisema ucheleweshwaji wa ulipaji wa deni hilo umetokana na mtikisiko wa uchumi
duniani ambapo wageni ambao ilitegemea kuwalaza wameshidwa kufika.
Aliwataka
waumini kuboresha miradi yote iliyoachwa na marehemu ili kumuenzi mawazo yake
jitihada alizokuwa akizifanya kwa ajili ya kusaidia jamii ya kanisa lake na
nchi kwa ujumla.
Kwa upande
wake Kiongozi wa kambi ya upinzani bungeni na mwenyekiti wa Chadema Freeman
Mbowe, aliwataka viongozi wa siasa na Serikali kuhubiri unyenyevu ndani ya
kanisa na nje.
Alisema
viongozi wengi wamekuwa wakihubiri unyenyekevu ndani ya kanisa lakini suala hilo
wamelisahau kulifanya nje ya kanisa jambo ambalo ni hatari kwa amani ya nchi.
“ kupitia
msiba huu wa mpendwa wetu, ni wakati sasa kwa viongozi wa dini kuwaeleza ukweli
viongozi wa Kiserikali pale wanapokosea…hii itasaidia kujirekebisha na kutuacha
kuishi kwa hofu,”alisema Mbowe.
Mwenyekiti
wa kituo cha demokrasia nchini, James Mbatia aliwataka viongozi wa dini kukaa
chini pamoja kujadili amani badala ya kulalamika kuwa amani imekuwa ikitoweka.
Alisema
kulalamika sio suluhu ya matatizo yanayolikabili Taifa la Tanzania, lakini kwa
kukaa pamoja na suluhu ya kuonyana na kuelimisha mambo mbalimbali
yatakayoisaidia nchi kuendeleza amani na utulivu iliyokuwa nayo.
Akitoa
salamu za Umoja wa madhehebu ya kikristo nchini (CCT), Askofu Victor Kitula
aliitaka Serikali kutolea tamko mauaji ya mchungaji yaliyotokea Geita hivi
karibuni kutokana na kile kilichoelezwa kuwa ni vurugu za kujinja.
Alisema
kanisa limesikitishwa na kitendo cha Serikali kunyamazia mauaji hayo ambayo wao
kikanisa ni makubwa kufuatia aliouawa kuwa ni mchungaji ambae amekuwa akiongoza
wakristo jimboni humo.
Ends…
No comments:
Post a Comment