Wednesday, 28 November 2012

PICHA MBALIMBALI SAFARI YA MWISHO YA MSANII SHARO MILIONEA KUINGIA KABURINI - INA LILAH INA ILAI RAJIUN

WAUMINI WA KIISLAM WAKIUOMBEA DUA MWILI WA MAREHEMU SHARO MILIONEA KABLA YA MWILI WAKE KUZIKWA NYUMBANI KWAO MUHEZA MKOANI TANGA MAPEMA LEO JIONI
Mwili wa Marehemu Sharo Milionea ukiswaliwa mapema mchana huu kabla ya kupelekwa kwenye nyumba yake ya milele
Rafiki mkubwa wa marehemu Sharo Milionea,Mzee Majuto akiwa ameshikwa mkonona Msanii wa filamu JB wakielekea kwenye mazishi mapema mchana huu,Muheza mkoani Tanga.
WAKAZI WA TANGA KIBAONI, MUHEZA TANGA WAKIWA MAKABURINI KUMZIKA SHARO MILIONEA KATIKA MAZISHI YALIYOFANYIKA ALASIRI YA LEO  

LOWASA AENDESHA HARAMBEE YA UJENZI WA MABWENI YA WASICHANA- CHUO KIKUU CHA TEOFIL KISANJI MBEYA

 



Add caption


Waziri Mkuu mstaafu na Mbunge wa Jimbo la Monduli,Mh. Edward Lowassa akiendesha harambe ya kuchangia ujenzi wa bweni la wanafunzi wa kike katika Chuo Kikuu cha Teofilo Kisanji, kinachomilikiwa na Kanisa la Moravian nchini Tanzania,Jimbo la Kusini Magharibi,usharika wa Ruanda mjini Mbeya.Kulia ni Mkuu wa Wilaya ya Rungwe,Mh. Cripin Meela
WAZIRI Mkuu Mstaafu Edward Lowassa amewataka vijana nchini kusoma kwa bidii ili kutoa ushindani katika soko la jira la Afrika Mashariki (EAC).
Lowassa aliyasema hayo jana jijini Mbeya alipoongoza harambee ya kuchangisha fedha za ujenzi wa mabweni ya Wasichana Chuo Kikuu cha Teofilo Kisanji kinachomilikiwa na Kanisa la Moravani Tanzania.
Katika harambee hiyo Lowassa, familia na marafiki zake walichangia fedha taslimu Sh. Milioni 20, ahadi Sh. Milioni 5 na kufanya jumla alizochangia kuwa Sh. Milioni 25.
Akizungumza katika harambee hiyo alisema, unyonge wa wasichana wa kike mashuleni hauwezi kuondolewa kwa kelele za kisiasa hata siku moja.
“Unyonge wao hauwezi kuondoka kwa kelele za kiasiasa tu, bali ukombozi wao kwa sehemu kubwa upo mikononi mwao kwa maana ya elimu,” alisema Lowassa.
Alisema hivi sasa taifa la Tanzania limekuwa na idadi kubwa ya vijana ambao kwa namna yoyote wanapaswa kuandaliwa vizuri.
“Katika taifa letu vijana ndio wengi zaidi hivyo ni muhimu tuwaandae vizuri endapo tunataka kuwa na taifa madubuti,” alisema Lowassa na kuongeza:
“Mwalimu Nyerere alitufundisha; kupanga ni kuchagua.
Hivyo natoa mwito kwa wasichana mjiepushe na viwashiwi na msome kwa bidii,”alisema.
Akifafanua kuhusu umuhimu wa ujenzi wa Hosteli za wasichana mashuleni na vyuoni unatokana na wasichana wengi kukabiliwa na mazingira magumu yanayotishia mustakabli wa maisha yao.
Alisema kwa sasa Jumuiya ya Afrika Mashariki tayari imefungua mipaka yake ya ajira huria hivyo kama vijana nchini wataendelea kukosa elimu basi ushindani katika soko hilo utakuwa mgumu.
“Ndugu zangu nawaomba tuunganishe nguvu tuwasaidie vijana wetu, naamini tukitoa Mungu hata acha kutubariki na atabariki kazi zetu kuongeza riziki zetu.
“Rafiki zangu wadai mimi ni tajiri nina fedha nyingi, si kweli ninafanya jambo hili kwa kushirikisha rafiki, ndugu na jamaa zangu tangu nianze kutoa sijafirisika,” alisema Lowassa.
Awali Askofu Kiongozi wa Kanisa la Moravian Tanzania Alinikisa Cheyo akizungumza katika harambee hiyo alisema, kukamilika kwa mabweni hayo kutasaidia wasichana 348 kukaa sehemu moja kwenye vyumba 87.
“Tumejipanga kukusanya Sh.Milioni 235 katika harambee hii,” alisema Askofu Kiongozi Cheyo.
Naye Mkuu wa wilaya ya Rugwe Chrispn Meela akizungumza kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Abass Kandoro alisema, serikali itaendelea kuwa karibu katika kuhakikisha mabweni hayo yanakamilika.
“Serikali inaendelea kuunga mkono juhudi hizi kwani ni lazima tuwekeze katika elimu na kwa kutambua hilo tunatoa Sh. Milioni Moja,” alisema Meela.



TAASISI ZA FEDHA ZAPEWA CHANGAMOTO NA JK

RAIS Jakaya Kikwete amezitaka taasisi za fedha nchini kuondoa vikwazo mbalimbali wakati wa ujazaji wa fomu kwa ajili ya kufungua akaunti kwanye mabenki kwani kwakufanya hivyo wananchi wanaweza kukaa na fedha majumbani badala ya kuzipeleka kwenye benki.
Aidha amezisihi benki kutoa mikopo zaidi kwa wananchi hususan wakulima pamoja na wafugaji ili kuwa na ongezeko kubwa la wananchi wanaojiajiri wenyewe na kupata vipato kutokana na mikopo ya bei nafuu.
Kikwete aliyasema hayo jana wakati akifungua mkutano wa 16 wa Taasisi za Fedha unaofanyika Jijini Arusha.
Alisema vikwazo ni vingi katika ufunguaji wa akaunti hali inayopelekea wananchi kushindwa kufungua akaunti na kukaa na fedha majumbani mwao na wengine kuzichimbia chini ya ardhi kwaajili ya usalama kutokana na hatua mbalimbali za ujazaji wa fomu.
“Acheni urasimu ukitaka kufungua akaunti mlolongo ni mkubwa sana mpaka unamchosha mwananchi anayetaka kufungua akaunti angalie utaratibu mwingine juu ya ufunguaji wa akaunti mkiendelea hivyo mitakosa wateja pia huduma ya utoaji wa fedha kwakutumia simu inakuwa kwa kasi kwasababu haina mlolongo mrefu kama wa mabenki”.
Alisisitiza kuwa taasisi za kibenki kuhakikisha zinatoa mikopo nafuu kwa wakulima na wafugaji ili kuwawezesha wananchi kunufaika na kilimo zaidi kwani maendeleo ya kila nchi yanatokana na kilimo cha kisasa zaidi.
Alisema hivi sasa kasi ya utumaji wa fedha kwakutumia simu za mkononi imeongezeka zaidi na wateja wengi wanaipenda njia hiyo kwasababu ni salama na haina mlolongo mrefu wa utumaji wa fedha kama vile kwenye mabenki.
Naye Gavana wa Benki Kuu (BoT), Profesa Benno Ndulu alisema Benki hiyo imezindua mfuko wa wadhamini wa Mwalimu Julius Nyerere ambao utawezesha wanafunzi wa kike na wa kiume kupata ufadhili wa masomo ya sayansi na hesabu
Akizindua mfuko huo wa wadhamini ,Rais Kikwete aliipongeza benki hiyo ,taasisi za fedha pamoja na magava wastaafu na wafanyakazi wa benki kuu kwa moyo waliouonyesha juu ya kuendeleza elimu ambayo hayati Mwali Nyerere ambaye ni baba wa Taifa alihamasisha sana elimu kwa vijana ambayo inaleta maendeleo.
Mkutano huo pia ulihudhuriwa na Mama Maria Nyerere, Gavana Mstaafu, Edward Mtei pamoja na wadau mbalimbali wa taasisi za fedha ndani na nje ya nchi.


PICHA MBALIMBALI UZINDUZI WA JENGO LA UMOJA WA AFRIKA MASHARIKI JIJINI ARUSHA LEO

SPIKA WA BUNGE LA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA ANNE MAKINDA AKISALIMIANA NA RAIS KIKWETE MUDA MFUPI KABLA YA KUZINDUA JENGO LA JUMUIYA YA AFRIKA MASHARIKI ZITAKAZOKUWEPO OFISI ZA JUMUIYA HIYO JIJINI ARUSHA LEO.


TASWIRA YA JENGO LA AFRIKA MASHARIKI INAVYOONEKANA KWA MBELE


KIKUNDI CHA NGOMA KUTOKA UGANDA KIKITUMBUIZA WAKATI WA HAFLA YA UZINDUZI WA JENGO AMBALO LITAKUWA LIKITUMIKA KWA OFISI ZA AFRIKA MASHARIKI LEO JIJINI ARUSHA

Tuesday, 27 November 2012

SHARO MILIONEA HATUNAE TENA- KALALE PEMA PEPONI KAMANDA

Kamanda wa Polisi mkoani Tanga, Constatine Masawe amekiri kutokea kwa msiba wa Hussein Mkieti ‘Sharo Milionea’, baada ya kupata ajali katika kijiji cha Lusanga, Muheza akiwa katika gari lenye namba za usajili T478 BVR Toyota Harrier, majira ya saa mbili usiku, ambapo pia ndio nyumbani kwao.

MWILI WA SHARO MILIONARE UKIWA UMELAZWA MOCHWARI
Sasa naweza kusema R.I.P Sharomilonea. Maiti ya Sharo Milionea imehifadhiwa hospitali ya Teule Muheza.

kutoka magazetini leo jumanne 27/11/2012









Friday, 23 November 2012

WIZARA YA KILIMO NA CHAKULA YASHINDWA KULIPA MAMILIONI VIBARUA WAKE



WIZARA YA KILIMO NA CHAKULA YASHINDWA KULIPA MAMILIONI VIBARUA WAKE

WIZARA ya Kilimo, Chakula na Ushirika inadaiwa kushidwa kulipa Mamilioni ya fedha za Vibarua  wanaofanya kazi katika Kituo cha kueneza Teknolojia za Kilimo ATTC, cha kanda ya Kaskazini kilicho Themi jijini Arusha kwa miezi sita sasa.

Vibarua hao Saba  wamesema hawajalipwa madai yao tangia Mwezi marchi mwaka huu hadi sasa na hivyo wameonyesha wasi wasi kuwa huenda fedha hizo ambazo zimetengwa kwa ajili ya malipo yao zimechachuliwa  hali inayowafanya wao waishi katika mazingira magumu na kwa matumaini kama wagonjwa wa Ukimwi ambao wajui lini watapona.

Vibarua hao wakizungumza na vyombo vya habari katika ofisi za Idara habari maelezo, mkoa wa Arusha, wamesema kuwa hawajalipwa Ujira wao tangia mwezi Marchi mwaka huu hivyo wao wanashindwa kulipia kodi za nyumba, kugharimia matunzo ya familia ,kugharimia matibabu .

Wamesema kuwa wanajipanga kukifanyia uharibifu mkubwa katika   kituo hicho kutokana na kutolipwa ujira wao kwani wamevumilia lakini sasa uzalendo umewashinda.

Kutokana na Wizara hiyo  kushindwa kuwalipa kiasi cha shilingi milioni 4,200,000, wanazodai tangia Marchi hadi Novemba mwaka huu, wanaona kuwa hawatendewi haki na kuna uwezekano fungu hilo limechakachuliwa ,na wajanja wa wizara hiyo wasiokitakia kituo hicho mafanikio katika maonyesho ya kila mwaka ya Nane nane.

Kituo hicho kilianzishwa na wizara hiyo mwaka 2008 na kiliingia mkataba na vibarua hao kwa ajili ya kuendesha Vishamba vidogo vidogo vya mafunzo ya mazao mbalimbali ya kilimo kwa kipindi chote cha mwaka. Hivyo wakapendekeza Kituo hicho kifungwe kwa sababu wamechoka kufanya kazi bila kulipwa kwa wakati.

”Inashangaza kila tukitaka kulipwa lazima twende kwenye vyombo vya habari vinginevyo hatulipwi hali hii itaendelea mpaka lini ni bora kituo hiki kifungwe vinginevyo tutafanya uharibifu mkubwa  ”, walisema vibarua hao.

Vibarua hao wamekuwa wakifanya kazi ya kuhudumia vipando vya mazao mbalimbali yakiwemo mazao ya mizizi ,migomba, vikolezo na miti ya matunda.

Vibarua hao wamekuwa wakitoa mafunzo endelevu kwa mwaka mzima kwa watu mbalimbali wanaotembelea kituo hicho kwa kutumia teknolojia na mbinu zitakazowawezesha wakulima kulima kilimo chenye  tija na kupata faida kubwa

Vibarua hao wamesema wanashangazwa na hatua ya Wizara hiyo kuingia mkataba na kampuni binafsi ya Ulinzi ya SGS,kulinda Kituo hicho  ,ambayo imekuwa inalipwa kila mwezi ,lakini wao hawalipwi .

Wamesema kuwa wao wanafanya kazi kubwa ya kutunza vipando,na na wao ndio husababisha Wizara hiyo kupata ushindi kila mwaka katika maonyesho hayo ya Nane nane lakini hawathaminiwi  licha ya mchango mkubwa wanaoutoa wa kutunza vipando hivyo.

Msimamizi wa kituo hicho, Elias Ernest, alipoulizwa kuhusiana na madai hayo alikiri na kueleza kuwa ameshawasilisha Wizarani
 .
Ameongeza  kuwa Vibarua hao wamekuwa wakitumia lugha za vitisho ikiwa ni kushinikiza walipwe madai yao pia wamepoteza moyo wa kufanya kazi .


KESI INAYOMKABILI LEMA SASA DESEMBA 4, MWAKA HUU



KESI INAYOMKABILI LEMA SASA DESEMBA 4, MWAKA HUU

Kesi Uchaguzi inayomkabili aliyekuwa mbunge wa jimbo la Arusha mjini Godbless Lema wa tiketi ya Chama Cha Demokrasia na Maendeleo{CHADEMA} itasikilizwa desemba 4  mwaka huu katika mahakama ya rufaa Jijini Dar es salaamu.

Awali mahakama ya rufaa yenye majaji watatu wakiongozwa na Jaji Mkuu Othmani Chande novemba 8 mwaka huu iliamuru mkata rufaa Leman a wakili wake Method Kimomogolo kurekebisha rufaa yao iliyokuwa na makosa mengi ya kisheria ndani ya siku 14.

Chande akiwa na majaji wengine Salumu Masati na Nathalie Kimaro walimtaka lema kuwalipa mawakili wawili Alute Mungway na Modesti Akida gharama zao za kuja Jijini Dar es salaamu kuja kusikiliza kesi hiyo .

Kwa mujibu wa hukumu hiyo ya pingamizi iliyotolewa siku hiyo pia Mbunge huyo wa zamani ametakiwa pia kuwalipa gharama zote wanachama watatu wa Chama Cha Mapinduzi[CCM} waliofungua kesi hiyo kwa kwenda Jijini Dar es salaamu.


Akizungumza na gazeti hili jana Mussa Mkanga alisema kuwa tayari amepewa hati ya kuitwa katika mahakama ya rufaa siku hiyo na wao wameshaanda gharama ya kesi hiyo kama walivyoamuriwa na Mahakama hiyo lakini hakuwa tayari kutaja kiasi cha gharama hiyo kwa madai kuwa mpaka itakapowasilishwa katika mahakama hiyo.


‘’Nafikiri wamesharekebisha rufaa yao kwani walipewa muda wa siku 14 kuirekebisha na muda umeshapita na sisi tumeshapewa hati ya kuitwa katika mahakama hiyo kusikiliza kesi hiyo na tayari tumeshakamilisha mahesabu yetu ya gharama zetu’’ alisema Mkanga


Wakati huo huo Mkanga pia alizungumzia uvumi ulioenea Jijini Arusha hususani katika mitandao ya kijamii kuwa amepooza mwili mzima baada ya kuendelea kufuatilia sana kesi hiyo na kueleza kuwa maneno hayo sio ya kweli kwani yeye ni mzima wa afya na hana ugonjwa wowote hata ‘’homa ya mafua’’.

Alisema wale wote wenye nia mbaya ya kumwombea yeye kupata ugonjwa huo iko siku mungu atawalipiza wao kwani siku zote mungu hapendi mcha mungu kumwombea mwenzake mabaya.

WANAFUNZI WAPANGIWA UTARATIBU WA KUCHANGIA JAMII



WANAFUNZI WAPANGIWA UTARATIBU WA KUCHANGIA JAMII 

WANAFUNZI wa kidato cha nne,tano na sita katika shule binafsi ya Mtakatifu Costantine ya jijini Arusha wamepangiwa utaratibu na uongozi wa shule hiyo wa  kuchangia jamii inayowazunguka kabla ya kupata cheti cha kuhitimu elimu yao.

Katika kuitia wito huo wanafunzi wanne wa shule hiyo wa kidatu cha sita Novemba 16 mwaka huu wamechanga jumla ya shilingi milioni 4,155,000 ambazo zitawasaidia wanafunzi wa nyumba tatu za watoto yatima ambao wako sekondari wa Jijini Arusha

Wanafunzi waliojitoa na kuamua kuonyesha njia na kuitikia wito wa uongozi wa shule ni pamoja na Aljawaad Hassanali,Kush Lodhia ,Nuzhat Hatema na Shilia Patalia.

Akizungumza mara baada ya kukusanywa kwa fedha hizo taslimu ,Hassanali alisema mbali ya kusaidia nyumba tatu za watoto yatima pia fedha hizo zitapelekwa kwa wanafunzi 6 wa sekondari wenye mtindo wa akili (kwenye shule maalumu za walemavu).

Alisema kuna wanafunzi 90 wa kidatu cha nne, tano na sita katika shule ya Constantino na wote wametakiwa kusaidia jamii vinginevyo huruhusiwi kupata cheti cha kumaliza shule mpaka utimize lengo hilo ambalo sisi wanafunzi tunakumbushwa kusaidia jamii isiyi jiweza ambayo inayotuzunguka.

‘’hatuna shida na kuchangia hilo kwani ni jukumu la kina mwanadamu na uongozi wa shule ulipoamua na kupitisha hilo hakuna mzazi wala mwanafunzi aliyebisha na kinachotakiwa ni kujipanga na kuangalia wapi kwa kusaidia ‘’alisema

Mmoja wa wazazi wa mtoto anayesoma katika shule hiyo ambaye aliombakutotajwa jina alisema kuwa mpango huo unawajenga wanafunzi kuwa na ukarimu kwa jamii wakiwa wadogo na hiyo itasaidia sana wanafunzi hao.

Alisema uongozi wa shule umebuni mkakati mzuri sana kwa wanafunzi wanasoma katika shule hiyo wa vidatu hivyo kuwa na ukarimu kwa jamii kwa kusaidia watoto wengine hususani wenye uwezo mdogo,walemavu na yatima.


RC ARUSHA: WAKAZI KUWENI TAYARI KUPOKEA MAENDELEO





RC ARUSHA: WAKAZI KUWENI TAYARI KUPOKEA MAENDELEO 

MKUU wa mkoa wa Arusha Magessa Mulongo amewataka wakazi wa jiji la Arusha kujiweka tayari kuendana na maendeleo yanayojitokeza ikiwemo uwepo wa taasisi mbalimbali za kimataifa jiji hapo.

Mulongo amesema hayo leo alipokua akizungumza na vyombo vya habari kuhusu uzinduzi wa jingo la kisasa la makao makuu ya jumuiya ya Afrika Mashariki unaotarajiwa kufanyika mnamo Novemba 28 mwaka huu.

Alisema kuwepo kwa makao hayo makuu ya jumuiya hiyo kunaendana sambamba na ongezeko la watu watakaokua watumishi wa jumuiya hiyo kutoka nchi mbalimbali ambao watahitaji pia malazi yaliyo bora pamoja na mahitaji mengine mengi.

Kufuatia kauli hiyo aliwataka wakazi hao kuboresha majengo yao yaliyo jirani na maeneo ya mijini ili yaendane na kasi hiyo pamoja na ukarabati mkubwa uliofanywa na serikali kama hatua za mapokezi ya ujio huo wa jumuiya hiyo.

Katika hatua nyingine Mulongo alisema maandalizi yote ya uzinduzi wa jingo hilo yamekamilika na kinachosubiriwa na ujio wa Marais wote wan chi zinazounda jumuiya hiyo watakaokutana mkoani Arusha.

Mulongo alisema mara baada ya kukamilika kwa shughuli hiyo viongozi hao wataondoka mkoani hapa kuelekea jijini Nairobi nchini Kenya ambapo watahudhuria kongamano la kujadili masuala mbalimbali yahusuyo muungano huo.

Hata hivyo viongozi hao wakiwa nchini Kenya watafanya shughuli ya uzinduzi wa barabara kuu ya Afrika Mashariki kutokea Tanzania hadi Nairobi nchini Kenya ambayo kwa upande wa Tanzania tayari jiwe la msingi la ujenzi huo lilishawekwa.

Akizungumzia mikakati ya mkoa wa Arusha katika kuboresha mazingira na kuwa katika hali nzuri alisema tayari ofisi yake imeshawaelekeza viongozi wa jiji la Arusha kuandaa mipango miji mizuri ikiwa ni pamoja na utaratibu mzuri wa ujenzi.

Alisema mkakati huo utawakumba baadhi ya watu ambao watapaswa kufidiwa kupisha uboreshaji huo na kwamba kwasasa mpango madhubuti unaandaliwa ili kuwezesha kupatikana kwa fedha zitakazotumika kuwafidia wahanga hao.

Pia alisema katika kuhakikisha msongamano wa magari unaondoka katika maeneo ya kati ya jiji tayari mkakati umekamilika wa upanuzi wa barabara kuu ya Moshi-Arusha ili kuwezesha kutembea magari manne kwa wakati mmoja kuanzia eneo la Mianzini hadi Tengeru mradi unaofadhiliwa na fedha za mfuko wa jumuiya ya Afrika Mashariki.

Pia alisema mpango mwingine ni ule wa ujenzi wa barabara mpya ya mzunguko kutoka eneo la Ngaramtoni hadi uwanja wa ndege wa Arusha kazi inayofanywa na serikali ya Tanzania na hatimaye awamu ya pili ni kuunganisha barabara hiyo hadi eneo la Tengeru ambapo ukikamilika utawezesha kuondoa msongamano huo kwakua mtu hatakua na haja ya kuingia mjini kama ana safari ya nje ya mji.