KESI INAYOMKABILI LEMA
SASA DESEMBA 4, MWAKA HUU
Kesi Uchaguzi
inayomkabili aliyekuwa mbunge wa jimbo la Arusha mjini Godbless Lema wa tiketi
ya Chama Cha Demokrasia na Maendeleo{CHADEMA} itasikilizwa desemba 4
mwaka huu katika mahakama ya rufaa Jijini Dar es salaamu.
Awali mahakama ya
rufaa yenye majaji watatu wakiongozwa na Jaji Mkuu Othmani Chande novemba 8
mwaka huu iliamuru mkata rufaa Leman a wakili wake Method Kimomogolo
kurekebisha rufaa yao iliyokuwa na makosa mengi ya kisheria ndani ya siku 14.
Chande akiwa na
majaji wengine Salumu Masati na Nathalie Kimaro walimtaka lema kuwalipa
mawakili wawili Alute Mungway na Modesti Akida gharama zao za kuja Jijini Dar
es salaamu kuja kusikiliza kesi hiyo .
Kwa mujibu wa hukumu
hiyo ya pingamizi iliyotolewa siku hiyo pia Mbunge huyo wa zamani ametakiwa pia
kuwalipa gharama zote wanachama watatu wa Chama Cha Mapinduzi[CCM} waliofungua
kesi hiyo kwa kwenda Jijini Dar es salaamu.
Akizungumza na gazeti
hili jana Mussa Mkanga alisema kuwa tayari amepewa hati ya kuitwa katika
mahakama ya rufaa siku hiyo na wao wameshaanda gharama ya kesi hiyo kama
walivyoamuriwa na Mahakama hiyo lakini hakuwa tayari kutaja kiasi cha gharama
hiyo kwa madai kuwa mpaka itakapowasilishwa katika mahakama hiyo.
‘’Nafikiri
wamesharekebisha rufaa yao kwani walipewa muda wa siku 14 kuirekebisha na muda
umeshapita na sisi tumeshapewa hati ya kuitwa katika mahakama hiyo kusikiliza
kesi hiyo na tayari tumeshakamilisha mahesabu yetu ya gharama zetu’’ alisema
Mkanga
Wakati huo huo Mkanga
pia alizungumzia uvumi ulioenea Jijini Arusha hususani katika mitandao ya kijamii
kuwa amepooza mwili mzima baada ya kuendelea kufuatilia sana kesi hiyo na
kueleza kuwa maneno hayo sio ya kweli kwani yeye ni mzima wa afya na hana
ugonjwa wowote hata ‘’homa ya mafua’’.
Alisema wale wote
wenye nia mbaya ya kumwombea yeye kupata ugonjwa huo iko siku mungu atawalipiza
wao kwani siku zote mungu hapendi mcha mungu kumwombea mwenzake mabaya.
No comments:
Post a Comment