Mbunge wa Ubungo John Mnyika akimwomba Spika Anne Makinda kuilazimisha Serikali kutolea kauli tatizo la uhaba wa mafuta nchini jana bungeni mjini Dodoma . |
Waziri Mkuu Mizengo Pinda akijibu hoja ya Mbunge wa Ubungo John Mnyika kuhusu kauli ambayo Serikali itatoa hivi karibuni juu ya mkakati wa kukabiliana na uhaba wa mafuta nchini |
KUTOKA DODOMA.
Mbunge
wa Ubungo (CHADEMA) John Mnyika akihoji kiti cha spika juu ya serikali
kushindwa kuleta bungeni kauli ya serikali juu ya mkakati wa serikali
kukabiliana na uhaba wa mafuta nchini Tanzania.
Uhaba
wa mafuta leo umewakimbiza kwenye kikao cha bunge mjini Dodoma asubuhi,
Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo na naibu mawaziri
wake George Simbachawene na Steven Masele.
Waziri
huyo na naibu mawaziri wake hawakuwepo bungeni leo wakati Mbunge wa
Ubungo (CHADEMA) John Mnyika alitaka serikali itoe sababu ya kutokuja
bungeni leo kutoa tamko la serikali ya jinsi inavyoshughulikia swala la
uhaba wa mafuta nchini.
Spika
wa Bunge Anne Makinda alimlazimisha Waziri kuu Mizengo Pinda kusimama
na kujibu hoja ya Mnyika aliyemtaka Spika kulazimisha serikali ijibu
hoja yake pamoja na mkakati wa serikali wa kutatua uhaba wa mafuta
nchini.
Waziri
Mkuu Mizengo Pinda alilazimika kunyanyuka nakusema kwa ufupi kuwa
serikali ilikuwa ikijiandaa na kuja na hoja nzito ya kueleza umma
mikakati kabambe ya kutatua uhaba wa mafuta nchini.
No comments:
Post a Comment