Nchi tatu zimekabidhiwa Tunzo kutokana na ubunifu wao
katika Sekta ya Umma .
Nchi hizo zilizoshinda na kupewa Tunzo na Jumuiya ya
Utumishi wa Umma katika Afrika na Uongozi AAPAM ni pamoja na Kenya, Mauritius na
Ghana
Tunzo hizo zimetokana na kuwa wabunifu katika masuala
mbalimbali ambapo Kenya imekuwa mshindi wa Kwanza kwa kupata medali ya dhahabu
ikifuatiwa na Mauritius iliyopata Medali ya Fedha na Ghana iliyopata Medali ya
Shaba.
Wakati huo huo Mkutano wa 34 wa AAPAM uliomalizika hivi
leo hapa Zanzibar na kufungwa rasmi na Makamu wa Pili wa Rais Zanzibar Balozi
Seif Ali Idd umetoa maazimio mbalimbali yanayohusu Mkutano huo.
Miongoni mwa maazimio hayo ni kuwa na Mfumo bora na mzuri
wa Utawala, kuimarisha mazingira juu ya nchi na Uongozi, Kuwashirikisha wadau
wengine katika kuimarisha Utawala Bora na siyo Serikali kujipangia wao wenyewe
tu.
Kwa mujibu wa Katibu Mkuu wa AAPAM ameeleza kuwa Mkutano
huo wa 34 umefanikiwa sana kutokana na mahudhurio ambapo Wajumbe 420
walihudhuria kutoka nchi 35 za Afrika na nje ya Afrika.
Mwaka jana Mkutano kama huo wa AAPAM uliofanyika nchini
Malawi nchi 35 zilihudhuria ambapo wajumbe wapatao 210 ndio
walioshiriki.
Katibu huyo wa AAPAM ameeleza kuwa tangu kufanyika
Mikutano hiyo hii ni mara ya kwanza kwa wajumbe wengi kuhudhuria katika Mkutano
huo na kuwa wa mafanikio makubwa.
Mkutano wa AAPAM hapo mwakani umeamuliwa kufanyika mjini
Kigali,Rwanda.
Wajumbe kadhaa waliohudhuria Mkutano huo wameshaanza
kuondoka hapa Zanzibar kurejea nyumbani.
IMETOLEWA NA IDARA YA HABARI MAELEZO ZANZIBAR.
No comments:
Post a Comment