Saturday, 17 November 2012

ZOEZI SAFISHA JIJI - WAMACHINGA WAKAMATWA KATIKATI YA JIJI LA ARUSHA

Bidhaa mbalimbali zikiwa zimepakiwa juu ya gari la Halmashauri baada ya kukamatwa.


Mgambo wakijiandaa kupatikia bidhaa walizokamata jana katika mtaa wa majengo karibu na stendi kuu ya mabasi makubwa jijini Arusha

Mgambo na watumishi wa Halmashauri wakipakia bidhaa za wamachinga walizozikamata jana.

Watendaji wa Halmashauri ya jiji la Arusha pamoja na Askari Mgambo wakipakia bidhaa za wafanyabiashara ndogondogo(wamachinga), wanaofanyabiashara zao kwa mikokoteni jana kwenye gari lao, katika zoezi la kuondoa wamachinga katikati ya jiji.

Mgambo wa jiji la Arusha pamoja na watendaji wa Halmashauri hiyo wakisukuma mkokoteni wa mmoja wa wamachinga waliokamatwa wakifanya biashara zao jana  pembezoni mwa barabara za kuingia stendi kubwa eneo  ambalo limekatazwa kufanyiabiashara ndogongogo jijini Arusha, ,kushoto ni gari la Polisi PT 1434 likihakikisha usalama unakuwepo wakati wa utekelezaji wa zoezi hilo.

No comments:

Post a Comment