Madiwani, Mkurugenzi, Makatibu waenda jela
Na Mwandishi Wetu
Mahakama ya Hakimu Mkazi jijini Mwanza imewatia hatiani viongozi watano wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) wakiwamo madiwani wawili kwa kosa la kukaidi amri ya Mahakama.
Na Mwandishi Wetu
Mahakama ya Hakimu Mkazi jijini Mwanza imewatia hatiani viongozi watano wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) wakiwamo madiwani wawili kwa kosa la kukaidi amri ya Mahakama.
Viongozi waliotiwa hatiani ni madiwani Dan
Kahungu wa Kata ya Kirumba na Josephat Manyerere wa Kata ya Nyakato
ambaye kabla ya kuondolewa kwa kupigiwa kura ya kutokuwa na imani naye
alikuwa ndiye Meya wa Jiji la Mwanza.
Viongozi wengine wa Chadema waliotiwa
hatiani na Mahakama hiyo ni Mkurugenzi wa Oganaizesheni na Mafunzo wa
Chadema Taifa, Benson Kigaila, Katibu wa Chadema Wilaya ya Ilemela, John
Anajus na Katibu Mwenezi wa wilaya hiyo, Carlos Majura.
Hakimu Mkazi Mfawidhi wa Mahakama hiyo,
Angelo Rumisha, ndiye aliyewatia hatiani viongozi hao, lakini hakutamka
adhabu watakayotumikia kwa kile kilichoelezwa kwamba ni kutokana na
baadhi ya watuhumiwa kutokuwepo mahakamani hapo.
Diwani Kahungu na Katibu wa Chadema Wilaya
ya Ilemela, Anajus ndio waliokuwepo mahakamani wakati Hakimu Rumisha
akitangaza kuwatia hatiani na aliamuru wapelekwe rumande hadi wenzao
watatu watakapokamatwa na kufikishwa mahakamani.
Mbali na kuwatia hatiani viongozi hao wa
Chadema, Hakimu Rumisha alisema kwamba maamuzi ya awali yaliyotolewa na
Mahakama ya kutengua hatua ya Matata na mwenzake kuvuliwa uanachama
yatabaki kama yalivyo hadi itakapoamuliwa vinginevyo katika kesi ya
msingi.
Hatua hiyo ya Mahakama ya Hakimu Mfawidhi
jijini Mwanza kuwatia hatiani viongozi hao wa Chadema, inafuatia tukio
la Kamati Kuu ya Chadema kuwavua uanachama madiwani Henry Matata wa Kata
ya Kitangiri na Adam Chagulani wa Kata ya Igoma.
Baada ya madiwani hao kuvuliwa uanachana,
Matata alifungua kesi ya kupinga hatua hiyo na Mahakama ya Hakimu Mkazi
Mfawidhi jijini Mwanza ilitoa amri ya kutaka madiwani hao wasizuiwe
kuendelea na shughuli zao na watambuliwe kama wanachama halali wa
Chadema
Hata hivyo, Septemba 25, mwaka huu,
Chadema Wilaya ya Ilemela kilifanya mkutano wa uteuzi wa wagombea wa
nafasi ya Meya na Naibu Meya wa manispaa hiyo, hatua ambayo inaonekana
kuwa sababu ya Diwani Matata kuamua kufungua kesi dhidi ya baadhi ya
washiriki wa mkutano huo akiwamo Kigaila (Mkurugenzi wa Oganaizesheni)
akiwatuhumu kukiuka amri ya Mahakama kwa kutomshirikisha.
Oktoba 13 mwaka huu baadhi ya magazeti
yalichapisha habari kuhusiana na malalamiko ya Chadema Wilaya ya Ilemela
kwamba zipo njama zinazomhusisha Hakimu Mkazi wa Mahakama ya Mkoa wa
Mwanza, Angelo Rumisha, za kutaka kukihujumu chama hicho katika uchaguzi
wa Meya na Naibu Meya wa Manispaa ya Ilemela.
Chama hicho kilidai kwamba hujuma hiyo
inalenga kutaka kuwahukumu kifungo cha miezi sita jela madiwani wake
wawili ili wasipate fursa ya kushiriki uchaguzi wa Meya na Naibu wake
unaotarajiwa kufanyika hapo baadaye baada ya kuahirishwa katika
mazingira ya kutatanisha.
Kufuatia kuwepo kwa tetesi hizo, Chadema
kiliamua kumuandikia barua Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu Kanda ya Mwanza
kumtaka aingilie kati suala hilo na kuhakikisha haki inatendeka.
Katika barua hiyo yenye Kumbukumbu Namba
CDM/w.IL/2012/01 ya tarehe 11/10/2012 ambayo ilisainiwa na Mwenyekiti wa
Chadema Wilaya ya Ilemela, Yunus Chilongozi, kwenda kwa Jaji Mfawidhi,
chama hicho kilidai kwamba Madiwani wanaolengwa katika mpango huo ni Dan
Kahungu wa Kata ya Kirumba na Josephat Manyerere wa Kata ya Nyakato.
Mbali na madiwani hao, barua hiyo
iliwataja watu wengine wanaolengwa katika njama hizo kuwa ni Kigaila,
Anajus, Majura na Baraza la Wadhamini la chama hicho.
Chadema kimedai katika barua yake hiyo
kwamba Mahakama ya Hakimu Mkazi jijini Mwanza imeamua kukubali maombi
yenye lengo la kutaka kuwatia hatiani viongozi hao kama wafungwa wa
kimadai (civil prisoners) kwa kosa la kutotii amri ya Mahakama.
“Mheshimiwa jaji Mfawidhi, maombi hayo
yaliyowasilishwa na Henry Mtinda Matata kupitia mawakili wake, Magongo
na Matata, yakasajiliwa kama Misc.Application No.66/2012 yanaonekana
yamelenga hasa madiwani hao wawili kama njia ya kuwakomoa na
kuwasababishia kukosa nafasi ya kushiriki uchaguzi wa umeya wa Manispaa
mpya ya Ilemela,” inasema sehemu ya barua hiyo.
CHANZO:
NIPASHE
No comments:
Post a Comment