MKUU
WA MKOA WA DAR ES SALAAM SAID MECK SADIKI ATOA TAMKO KALI KUHUSU
MAANDAMANO YA WAISLAM YALIYOPANGWA KUFANYIKA SIKU YA IJUMAA MARA BAADA
YA SWALA.
Na Adrophina Ndyeikiza-Ofisi ya RC Dar es Salaam 1/11/2012.
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam,Said Meck Sadiki ametoa tamko kali la kuwataka Waislam kuacha mara moja kufanya maandamano yao yaliyopangwa kufanyika siku ya Ijuamaa ya tarehe 02/11/2012 mara baada ya swala ya Ijumaa.
Kwa mujibu wa vipeperushi vilivyoandikwa na kusambazwa na Jumuiya na
Taasisi za Kiislam (Tz),vimewataka waislam kufanya maandamano makubwa
kuelekea katika Ofisi ya Mhe.Waziri Mkuu kwa upande wa Dar es Salaam na
Mikoani maandamano hayo yataelekea kwa wakuu wa Mikoa aidha kwa upande
wa Zanzibar yataelekea Ofisi ya Makamu wa Rais.
Aidha,Sababu ya kuandamana kwao wameelezea kuwa ni kushinikiza Serikali
kutenda haki kwa wananchi wote bila ubaguzi kwani waislam wanabaguliwa
kwa mambo mengi kama vile;-
-Kudhalilishwa Masheikh wao kwa kukamatwa hovyo bila sababu za msingi
mfano,Sheikh Ponda na Sheikh Farid wakati wakristo hawafanyiwi hivyo.
Akijibu hoja hiyo mbele ya waandishi wa habari Mhe.Mkuu wa Mkoa amesema
kuwa Sheikh Ponda hakukamatwa kama Sheikh Ponda bali amekamatwa kama
mtu yeyote yule ambaye anaweza kutuhumiwa kwa kosa fulani.
Ameongeza kuwa
Serikali haikumkamata Sheikh Ponda kutokana usheikh wake/dini yake au
uislamu wake bali kutokana na kutuhumiwa kwake.Hivyo tuache vyombo vya
sheria vifanye kazi yake na haki itazingatiwa tu. “Alisisitiza Mkuu wa
Mkoa”.
-
Sababu nyingine ni pamoja na Kudhalilishwa matukufu ya Waislam huku
Serikali ikikaa kimya.
Akijibu hoja hiyo pia Mhe.Mkuu wa Mkoa amesema
kuwa jambo hili si kweli kabisa kwani Serikali ilikwishachukua hatua
stahiki kwa kumkamata kijana huyo aliyeyekojolea Koran na kumfikisha
katika vyombo vya sheria,hivyo kijana huyo alikwishakamatwa,hata hivyo
wale wote waliokwenda kuchoma makanisa,kupiga vioo vya magari ya watu na
kuiba vitu mbalimbali katika makanisa na ndani ya magari ya watu nao
pia wapo katika mikono ya sheria kwani uislam pia hauagizi hivyo.
Sababu ya tatu ni kuundiwa chombo cha kusimamia Waislam kwa nia ya
kuwadhibiti na kulazimishwa Waislam kukitii pamoja na ukweli kwamba
kinafisidi Uislam na Wislam.
Akijibu hoja hiyo Mhe.Mkuu wa Mkoa amesema
kuwa kamwe Serikali haiwezi kufanya hivyo,kwani kila chombo kinaundwa na
wanajamii husika na wala Serikali haina dini hivyo haiwezi kuunda
chombo chochote kile cha kidini.
Hata hivyo zipo taratibu maalumu za
namna ya kusajili taasisi yoyote ile kwani lazima kueleza mbele ya
msajili ya kuwa taasisi yenu ni ipi na ina malengo gani kwa jamii husika
na msajili akilizika na maelezo yenu basi huna budi kuisajili taasisi
hiyo.
Taasisi yoyote ile lazima isajiliwe na ifuate taratibu za sheria,na
Serikali inazisikiliza taasisi zote kama zinafuata sheria na taratibu
“Alisisitiza Mkuu wa Mkoa”.
Hivyo basi Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam,Said Meck Sadiki amesema kuwa
Waislam wote wapenda amani wasifanye maandamano yoyote siku hiyo ya
Ijumaa mara baada ya swala kwani kwa kufanya hivyo HATUA KALI ZA
KISHERIA DHIDI YA WATAKAOHUSIKA KATIKA KUYAANDAA NA KUSHIRIKI
ZITACHUKULIWA kwani maandamano hayo ni BATILI na hayajaruhusiwa na JESHI
LA POLISI. Sheria kali zitachukuliwa katika suala hili “Alisisitiza
Mkuu wa Mkoa”.
No comments:
Post a Comment