WANAFUNZI WAPANGIWA UTARATIBU WA KUCHANGIA JAMII
WANAFUNZI wa kidato cha nne,tano na
sita katika shule binafsi ya Mtakatifu Costantine ya jijini Arusha wamepangiwa
utaratibu na uongozi wa shule hiyo wa kuchangia jamii inayowazunguka
kabla ya kupata cheti cha kuhitimu elimu yao.
Katika kuitia wito huo wanafunzi
wanne wa shule hiyo wa kidatu cha sita Novemba 16 mwaka huu wamechanga jumla ya
shilingi milioni 4,155,000 ambazo zitawasaidia wanafunzi wa nyumba tatu za
watoto yatima ambao wako sekondari wa Jijini Arusha
Wanafunzi waliojitoa na kuamua
kuonyesha njia na kuitikia wito wa uongozi wa shule ni pamoja na Aljawaad
Hassanali,Kush Lodhia ,Nuzhat Hatema na Shilia Patalia.
Akizungumza mara baada ya kukusanywa
kwa fedha hizo taslimu ,Hassanali alisema mbali ya kusaidia nyumba tatu za
watoto yatima pia fedha hizo zitapelekwa kwa wanafunzi 6 wa sekondari wenye
mtindo wa akili (kwenye shule maalumu za walemavu).
Alisema kuna wanafunzi 90 wa kidatu
cha nne, tano na sita katika shule ya Constantino na wote wametakiwa kusaidia
jamii vinginevyo huruhusiwi kupata cheti cha kumaliza shule mpaka utimize lengo
hilo ambalo sisi wanafunzi tunakumbushwa kusaidia jamii isiyi jiweza ambayo
inayotuzunguka.
‘’hatuna shida na kuchangia hilo
kwani ni jukumu la kina mwanadamu na uongozi wa shule ulipoamua na kupitisha
hilo hakuna mzazi wala mwanafunzi aliyebisha na kinachotakiwa ni kujipanga na
kuangalia wapi kwa kusaidia ‘’alisema
Mmoja wa wazazi wa mtoto anayesoma
katika shule hiyo ambaye aliombakutotajwa jina alisema kuwa mpango huo
unawajenga wanafunzi kuwa na ukarimu kwa jamii wakiwa wadogo na hiyo itasaidia
sana wanafunzi hao.
Alisema uongozi wa shule umebuni
mkakati mzuri sana kwa wanafunzi wanasoma katika shule hiyo wa vidatu hivyo
kuwa na ukarimu kwa jamii kwa kusaidia watoto wengine hususani wenye uwezo
mdogo,walemavu na yatima.
No comments:
Post a Comment